Serikali ina sukari ya kutosha, watakaouza sukari bei juu watafutiwa leseni zao

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,000
9,861
Mkurugenzi wa bodi ya sukari Prof. Kenneth Bengesi amesema serikali ina sukari ya kutosha, na serikali imeshagiza tani 40,000 imeshaingia nchini na imeanza kupakuliwa tangu Aprili 15 bandarini

Pia amewataka wafanya biashara kufuata bei elekezi, na wale watakaokiuka wakigundulika watafutiwa leseni za kuendesha biashara

Amesema serikali haiko tayari kuona watu wake wanapata shida kwa tatizo ambal limetengenezwa na wafanyabiashara. Zaidi ya tani 10000 zitaingia mtaani kuanzia Aprili 17

Serikali iachane tu na hili suala tutatumia hata asali, wakienda kuchokonoa hiyo bei itafumuka mpaka 7000 kwa kilo, maana walijaribu mara ya kwanza na kufeli
 
Serikali inateseka sana na sukari. Nilijua kosa si kosa ila kurudia kosa! kumbe hawakuona kosa la kipindi kile na limejirudia tena mara ya pili.
 
Mara wanasema tutumie asali mara tena wanasema serikali ina sukari ya kutosha tunashindwa kuelewa tufate kauli ipi sasa...?
 
Hawa kalumekenge pasua kichwa Sana Hawa; walituyumbisha na sukari kipindi kile Sana; wakayeyuka Kama ukungu wa asubuhi,

Saizi wameanza Tena porojo zao. Kimsingi sijaona la maana lolote kwa Hawa watu kwenye kushughulika na masuala ya kijamii.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hawa jamaa hua hawajifunzi kwa makosa yao,usishangae hata mwaka huu wakaingilia tena bei ya Korosho.
 
Sisi hapa moshi tunakiwanda cha sukari TPC,
Ila cha kushangaza sukar kg in 3500-4000
Je waluopo Kigoma huko na musoma ambao hawana viwanda itauzwa ela ngap?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkurugenzi wa bodi ya sukari Prof. Kenneth Bengesi amesema serikali ina sukari ya kutosha, na serikali imeshagiza tani 40,000 imeshaingia nchini na imeanza kupakuliwa tangu Aprili 15 bandarini

Pia amewataka wafanya biashara kufuata bei elekezi, na wale watakaokiuka wakigundulika watafutiwa leseni za kuendesha biashara

Amesema serikali haiko tayari kuona watu wake wanapata shida kwa tatizo ambal limetengenezwa na wafanyabiashara. Zaidi ya tani 10000 zitaingia mtaani kuanzia Aprili 17

Itakuwa upuuzi kununua kitu kilichopo kwa wingi kununua kwa bei ya juu. Ukiona kitu kinauzwa bei ya juu tambua kuna uhaba tuache blah blah kwenye maisha ya watu
 
Mkurugenzi wa bodi ya sukari Prof. Kenneth Bengesi amesema serikali ina sukari ya kutosha, na serikali imeshagiza tani 40,000 imeshaingia nchini na imeanza kupakuliwa tangu Aprili 15 bandarini

Pia amewataka wafanya biashara kufuata bei elekezi, na wale watakaokiuka wakigundulika watafutiwa leseni za kuendesha biashara

Amesema serikali haiko tayari kuona watu wake wanapata shida kwa tatizo ambal limetengenezwa na wafanyabiashara. Zaidi ya tani 10000 zitaingia mtaani kuanzia Aprili 17

Sukari ilikwisha haikuagizwa mapema wenyewe mmethibitisha imeingia tarehe 15/04, itakuwa uzembe ulifanyika kwani tangu malalamiko ya kupanda bei yalipoanza hatukuweza kupata maelezo haya.
 
Hiyo bei elekezi ni shilingi ngapi na imetangazwa lini? Kama ndiyo ile 1,800/= ya mwaka 2016 mbona tangu ilipotangazwa wafanya biashara wameendelea kupandisha na hakuna hatua iliyochukuliwa dhidi yao?
 
Mkurugenzi wa bodi ya sukari Prof. Kenneth Bengesi amesema serikali ina sukari ya kutosha, na serikali imeshagiza tani 40,000 imeshaingia nchini na imeanza kupakuliwa tangu Aprili 15 bandarini

Pia amewataka wafanya biashara kufuata bei elekezi, na wale watakaokiuka wakigundulika watafutiwa leseni za kuendesha biashara

Amesema serikali haiko tayari kuona watu wake wanapata shida kwa tatizo ambal limetengenezwa na wafanyabiashara. Zaidi ya tani 10000 zitaingia mtaani kuanzia Aprili 17

Awamu ya tano iliingia sukari ikiwa chini ya Shs 2,000 Kama kawaida, imepiga hatua kubwa sana. Sasa ni Shs 4,500.

Wengine mnisaidie ulinganisho wa:

1. Unga wa sembe kwa kilo moja
2. Maharage kilo moja
3. Mchele kilo moja
4. Mafuta ya kupitia Lita moja
5. Wastani wa nauli ya daladala
6. Thamani ya US $ 1

N.k
 
Mkurugenzi wa bodi ya sukari Prof. Kenneth Bengesi amesema serikali ina sukari ya kutosha, na serikali imeshagiza tani 40,000 imeshaingia nchini na imeanza kupakuliwa tangu Aprili 15 bandarini

Pia amewataka wafanya biashara kufuata bei elekezi, na wale watakaokiuka wakigundulika watafutiwa leseni za kuendesha biashara

Amesema serikali haiko tayari kuona watu wake wanapata shida kwa tatizo ambal limetengenezwa na wafanyabiashara. Zaidi ya tani 10000 zitaingia mtaani kuanzia Aprili 17

Kuna waziri sijui anaitwa nani
Amekurupuka eti tuache matumizi ya sukari kwa sababu wataalamu wanasema sukari sio nzuri
Badala yake anashauri tutumie sanitizer oooh sio sanitizer badala ya sukari tutumie asali
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom