Serikali ina nia ya kulinda mazingira au ni yale yale tu?

MwanaHaki

R I P
Oct 17, 2006
2,401
707
Mwaka jana, katika kikao chake cha bajeti, Serikali ilitangaza kuondolewa kwa kodi zote kwenye chanzo cha nishati kijulikanacho kwa jina, Liquid Petroleum Gas (LPG). Nishati hii, kabla ya kuondolewa kwa kodi hizo, ilikuwa ikipatikana kwa bei mbaya, kwani ni nishati safi na nzuri zaidi kwa matumizi ya kupikia na kwenye maabara.

Wanamazingira na wachumi waliisifu Serikali kwa uamuzi wake huo, kwani Serikali ilifanya hivyo kwa nia ya kupunguza uharibifu wa mazingira unaotokana na ukataji wa miti kwa ajili ya kutengeneza mkaa wa kupikia. Wanamazingira waliisifu Serikali kwa kuonesha njia kwamba inawezekana kuweka mikakati thabiti ya kupunguza athari za uharibifu wa mazingira zinazotokana na mahitaji makubwa ya nishati.

Lakini cha kushangaza ni kwamba, bei ya reja reja ya LPG leo imepanda maradufu zaidi ya hata ilivyokuwa awali kabla ya Serikali kuondoa kodi. Je, hii ina maana kwamba Serikali imeamua kufuta uamuzi wake na kuanza kutoza kodi, au ni kwamba Serikali haina ubavu wa kuwahoji wausambazaji wa LPG kila wanapopandisha bei hiyo?

Kama kuna mwenye uwezo wa kutoa ufafanuzi katika jambo hili atusaidie kutupa mwanga zaidi, kwani kwa sasa, nachelea kurudia enzi za matumizi ya jiko la mkaa, wakati nilishazoea (na wengi pia waliingia kwenye mfumo huu) kutumia jiko la gesi. Nachelea litakuwa pambio lingine jikoni kwangu, kando ya jiko la umeme ambalo naogopa hata kuliwasha!

./Mwana wa Haki
 
Back
Top Bottom