Serikali ina mpango wa kuifunga mikono na miguu Chama cha wanasheria nchini TLS, Rais wake hatakuwa na mamlaka tena

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,572
26,868
Kuna muswada umeandaliwa kwa lengo la kukinyamazisha Chama Cha Wanasheria Tanzania (Tanganyika Law Society). Kwa lengo la kujifunga miguu na mikono katika mambo ya kisheria na kuhakikisha wanakuwa chini ya board.

Hivyo Rais wa TLS hatakuwa na mamlaka ya Chama hicho bali mkurugenzi atakayeajiriwa ndio atapewa nguvu kisheria kuisemea taasisi hiyo.
 
Ngoja wajaribu hiyo taaluma watakuwa kama WALIMU muda sio mrefu, tutaanza kuwasikia nao wakilialia mitandaoni sasa.
 
Kinachoundwa Ni bodi ya wanasheria Kama zilivyo bodi za Mainjinia,wahasibu nk Chama Cha wanasheria kitabakia Kama club tu ya wanasheria.

Bodi kazi yake kusimamia taaluma na utendaji wa wanasheria hiki chama kilichopo Sasa Ni Kama kijiwe tu Cha wanasheria kupiga porojo.Hakisimamii taaluma ya Sheria Wala utendaji Ni genge la wahuni
 
Hivyo Rais wa TLS hatakuwa na mamlaka ya chama hicho bali mkurugenzi atakayeajiriwa ndio atapewa nguvu kisheria kuisemea taasisi hiyo.
sio kweli chama kitabaki kama chama hakitakuwa chini ya serikali kitakuwa ni chama tu cha wanasheria kujiunga kwa hiari.WAO WATAENDELEA KUJICHAGULIA VIONGOZI WAO wanaowataka hakitakuwa chini ya serikali wala mahakama .KITAKUWA TU KAMA CHAMA cha kufa na kuzikana au chama chochote cha hiari na kitaendelea kubaki hivyo hivyo na jina lake au wanachama wakiamua waweza kibadili hata jina wakitaka

kwa sasa hicho chama hakisimamii taaluma wala utendaji wa mawakili ni kama lichama tu la wapiga domo vijiweni .Taaluma na utendaji wa mawakili utakuwa chini ya bodi kama zilivyo za madaktari,mainjinia,na wataalamu wengine hicho kitabaki kama chama cha hiari kama vyama vya siasa nk waweza jiunga au la .KINAKUWA kama club ya wanasheria
 
Hili jina la board kwenye taaluma limetawala sana awamu hii

Kwa mfano sisi walimu mbali na kuwa na CWT na Tsd kwa pamoja tuliahidiwa kuundiwa Bodi ya Walimu yenye lengo hilo hilo la kuboresha na kusimamia taaluma ya ualimu.

Kama ilivyo kwenye taaluma nyingine za udaktari, uhasibu na maingeneer tunajaribu kuona labda hii bodi inaweza kutusaidia.

Maana kiukweli walimu tumekwama hasa karibu kila upande; mazingira duni sana ya walimu wenyewe hata ya kufundishia pia ingawa cwt na hata tsd wapo tu hatujui hata wanafanyaga nini?

Wanasheria nao wanaletwa kundi hili tunawakaribisha ila wakumbuke huku changamoto zinazidi fursa
Kazi ni kwao!!!
 
Hivyo Rais wa TLS hatakuwa na mamlaka ya chama hicho bali mkurugenzi atakayeajiriwa ndio atapewa nguvu kisheria kuisemea taasisi hiyo.
Kwani ni lini Rais wa hicho chama aliwahi kuwa na mamlaka nchi hii?
Hiko chama hakina tofauti na chama cha wapiga ngoma,tunaka kukipa nguvu ya kisheria kusimamia taaluma kiwe kama bodi ya wahasibu na wakaguzi wa hesabu au bodi ya maboharia
 
Hao Wavuta bangi eeghhhh wanaotaka kuibadilisha TLC??
TLC ilijisqhau ikaigiza usiasa ndani yake wakati ilitakiwa iwe neutral iweze kubalance masuala ya kisheria hapa nchini. Ni uendawazimu kuingiza mtu anayemtukana Rais wa nchi awe mwenyekiti. Alitakiwa mwenyekiti aweze kumnyooshea kidole Rais amsaidie kuwa hapa umepotoka au sheria hii ingefaa iwe hivi. Tunajisahau tunaendekeza u CCM na uchadema katika masuala ya msingi
 
Awamu ya tano ipo kwa ajili ya mapambano tuu na kila lililo zuri kwa Uhuru wa Raia ili kulizuia au kuliua.
Kwa wale wacha Mungu wanaelewa wakisikia "nguvu za mwovu shetani" ni nini katika ulimwengu.
Mie naamini Watanzania sasa wanapambana na NGUVU ZA MWOVU SHETANI
 
TLC ilijisqhau ikaigiza usiasa ndani yake wakati ilitakiwa iwe neutral iweze kubalance masuala ya kisheria hapa nchini. Ni uendawazimu kuingiza mtu anayemtukana Rais wa nchi awe mwenyekiti. Alitakiwa mwenyekiti aweze kumnyooshea kidole Rais amsaidie kuwa hapa umepotoka au sheria hii ingefaa iwe hivi. Tunajisahau tunaendekeza u CCM na uchadema katika masuala ya msingi
Una point nzuri sana sana but mbaya humaanishi unachosema! Huu ndio ukweli mchungu! Najua Rais wa TLC unayem-refer ni Tundu Lisu na Fatima Karume, TLC ya sasa iko na Rais mwingine hebu nambie hata unayosema yana ukweli kiasi gani??

Pili, kama tuna uwezo wa kubadilisha utendaji wa Taasisi nzima kisa ni individual views tu tena sana last kwa mwaka mmoja then tutakua na tatizo mahali. Asante
 
Back
Top Bottom