Serikali ina mgogoro na Mwananchi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Serikali ina mgogoro na Mwananchi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kasheshe, Jan 15, 2009.

 1. Kasheshe

  Kasheshe JF-Expert Member

  #1
  Jan 15, 2009
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 4,690
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Kazi kweli kweli!!!!

  Kamata hiyo !!!!
  ==================================================

  Hokororo: Serikali ina mgogoro na Mwananchi

  Salim Said

  MKURUGENZI msaidizi wa Maelezo, Raphael Hokororo ameieleza Kamati ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii kuwa, serikali ina mgogoro na kampuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL), inayochapisha magazeti ya Mwananchi, The Citizen na Mwanaspoti, kuhusu umiliki wake.

  Akizungumza kwenye semina ya kamati hiyo iliyofanyika ofisi za Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Hokororo alisema serikali ina mgogoro na kampuni hiyo kwa vile inamilikiwa kwa kiasi kikubwa na wageni, kitu ambacho alisema hakitakiwi.

  Hokororo, ambaye alikuwa akichangia suala la ukamilishwaji wa sheria mpya ya habari, ambayo pia inazungumzia umiliki wa vyombo vya habari, alisema sheria inataka wageni wasimiliki chombo cha habari kwa zaidi ya asilimia 50, lakini kampuni ya Mwananchi inamilikiwa na wageni kwa asilimia 60.

  "Tumebaini kuwa mwekezaji wa kigeni anamiliki hisa nyingi zaidi kuliko mzawa mzalendo," alisema mkurugenzi huyo.

  “Wageni wanamiliki hisa nyingi zaidi ya asilimia 60 kuliko mzawa na hii ni kwa sababu wazawa waliokuwa na hisa katika kampuni hiyo waliamua kuuza hisa zao kwa wageni. Kutokana na hali hiyo, gazeti la Kingereza la The Citizen linalochapishwa na kampuni hiyo, linahaririwa jijini Nairobi Kenya na kuchapwa Tanzania, lakini wenyewe hawaoni taabu. Jambo hili hatukubaliani nalo."

  “Gazeti la Kingereza la TheCitizen linalochapishwa na kampuni ya mwananchi linahaririwa jijini Nairobi Kenya na kuchapwa Tanzania na wala wenyewe hawaoni tabu,” alisistiza.

  Hata hivyo, sheria inayounda tume huru ya ushindani wa kibiashara nchini inamruhusu mwekezaji wa kigeni kumiliki hata asilimia 98 ya hisa katika kiwanda chochote nchini, ingawa sera ya habari inataka wageni wasimiliki chombo cha habari kwa zaidi ya asilimia 50.

  Akizungumzia kauli hiyo, Mhariri Mtendaji wa magazeti ya Mwananchi, Theophil Makunga alisema amesikitishwa na kauli hiyo ya mwandishi huyo mkongwe, akisema kuwa mzungumzaji huyo anatoka ofisi ya msajili wa magazeti na anajua usajili wa The Citizen ulivyo.

  Alisema taarifa hizo ni za kusikitisha kwa kuwa hazina ukweli wowote kutokana na ukweli kuwa, gazeti hilo liko mikononi mwa Watanzania ambao ni wazawa.

  Alisisitiza kuwa gazeti la The Citizen si tu kwamba halihaririwi Nairobi, bali hata mhariri wake mtendaji, mhariri wa habari, msanifu mkuu, wahariri wengine na waandishi wote ni Watanzania na kazi zote za kuandaa, kuhariri na kuchapa gazeti hilo zinafanyika Dar es Salaam.

  Kuhusu muswada wa sheria ya habari, Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, Joel Bendera alisema marekebisho ya sheria hiyo namba tatu ya mwaka 1976 ya magazeti ipo jikoni na itawasilishwa bungeni kujadiliwa wakati wowote itakapokamilika.

  Akihitimisha semina ya kamati hiyo ya bunge, Bendera alisema: “Kwa sasa rasimu iko jikoni inachapwa kwa wataalamu wa ICT na ikimaliza hapo itapelekwa wizarani na baadaye bungeni kwa ajili ya kujadiliwa na hatimaye kupitishwa kama sheria.”

  Alisema vyombo vya habari ni kama bomu na kwamba kama umakini hautakuwepo katika marekebisho ya sheria hiyo, nchi haitatawalika.

  "Hebu tuangalie nchi za Rwanda na Burundi, mauaji yote ya kimbari yaliyotokea ni kazi ya vyombo vya habari tu. Hivyo tusipokuwa makini wabunge nchi haitatawalika," alisema.

  Alisistiza kuwa wao wabunge kwa kuwa wana dhamana kubwa kwa wananchi, hawapaswi kuachia mambo nyeti yaende ovyo ovyo kwa kuwa wakifanya hivyo nchi haitatawalika.

  "Najua kuwa sheria hii imepitwa na wakati na ndio maana tunataka kuileta bungeni ijadiliwe. Lakini kuna watu wanataka tupigane, hivyo tumieni busara zenu ili sheria hii iweze kuwa nzuri," alisisitiza Bendera.

  Miongoni mwa mambo yaliyo kwenye sheria hiyo ni uanzishwaji wa baraza la habari la serikali, ambalo linapingwa na wadau wa habari kwa kuwa wanaliona halitakuwa huru kama lilivyo baraza la sasa. Pia sheria hiyo inazungumzia kuwepo kwa viwango vya elimu kwa waandishi, na umiliki wa vyombo vya habari.

  Wadau wa habari pia wanadai kuwa hawakushirikishwa katika kuandaa muswaada huo na hivyo wanauona kuwa utazaa sheria ambayo itaendeleza mapungufu yaliyo kwenye sheria ya sasa.

  Katibu mkuu wizara hiyo, Dk Florens Turuka aliridhia kufanyika kwa vikao vya ziada baina ya wabunge wa kamati, serikali na wadau wa habari lakini akataka kusiwe na shinikizo kutoka kwa wadau na wanaharakati.

  "Tutakaa na kuangalia vipengele vyote vilivyo na udhaifu halafu tutavijadili na kuvirekebisha, kikiwemo hichi cha nguvu ya waziri," alisema Dk Turuka.

  Kaimu mwenyekiti wa kamati hiyo ya bunge ya Maendeleo ya Jamii, Haroub Said (Mbunge) alisisitiza umuhimu wa kuwashirikisha wadau katika kujadili marekebisho ya sheria hiyo.

  "Hatujakaa na serikali na wadau kujadili na kutoa mapendekezo ya sheria hii... ikiwa tutakutana hakutakuwa na mashaka... wala serikali isiwe na wasiwasi lakini kama itapelekwa bungeni bila ya kuwashirikisha wadau tutakuwa hatujawatendea haki," alisisitiza.

  Kama idara haina fedha ya kufanya vikao hivyo, basi mkurugenzi aandae bajeti kwa katibu wa kamati hii na yeye atajua ni jinsi gani ya kupata fedha za kufanyia vikao na wadau.

  Naye mkurugenzi msaidizi wa Idara ya Habari (Maelezo), Habib Nyundo alikiri kuwepo kwa upungufu na changamoto katika sheria hiyo na kuongeza kwamba kuna haja kubwa ya kuifanyia marekebisho.

  Alisema sheria hiyo haiweki utaratibu wa kutekeleza maelekezo ya Ibara ya 18 ya katiba ya Jamhuri ya Muungano ya 1977.

  "Sheria pia haifafanui mambo kadhaa muhimu yanayohitajika katika uendeshaji wa sekta nzima ya habari nchini," alisema Nyundo.

  Nyundo alisema changamoto nyingine inayowakabili ni kuwa sheria hiyo haipendwi hata kidogo na wadau wa habari nchini, hususan vyombo vya habari.

  "Vyombo vya habari haviitaki kabisa sheria namba 3 ya 1976 kwa sababu vinadai serikali imepewa uwezo mkubwa wa kuviingilia, kuvifungia na hata kuchukua mali zao pindi vinapokosea," alisema. Semina hiyo inaendelea tena leo kwenye ukumbi wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora uliopo jijini hapa.
   
 2. M

  Magobe T JF-Expert Member

  #2
  Jan 16, 2009
  Joined: Mar 19, 2008
  Messages: 2,945
  Likes Received: 357
  Trophy Points: 180
  Sishangai any developments against MCL. Tangu 2006 nilisikia tetesi kuwa kuna nia ya kuikaba koo kampuni ya MCL na hatimaye kuifunga kabisa au kuinunua. Je, kama inamilikiwa na wageni asilimia 60, kwa nini ilisajiriwa au msajiri wa magazeti hakuona hayo mwanzoni?

  Kwa bahati mbaya sheria zetu nyingi ni 'fluid' - zina tabia ya kimiminika - they can take any form depending on who says what and in what position.

  Kwamba The Citizen linahaririwa Nairobi hata hili nilianza kulisikia before 2006 na nilifanya kazi pale na kazi zote tulikuwa tukifanya sisi na kesho yake wakati wa postmorterm tulikuwa tukibaini makosa tuliyoyafanya. Je, kama lilikuwa linahaririwa Nairobi si hayo makosa tusingeyakuta?

  Sijui labda baadaye kulikuwa na mabadiliko lakini what I know gazeti linahaririwa pale News Room MCL Tabata Relini.

  Kama MCL ilisajiriwa kihalali kwa nini sasa isiwe halali au uhalali wake ume'expire'? Ninahisi kuna mbinu chafu zinapikwa dhidi ya vyombo vya habari hapa Tanzania. Everytime wakubwa wazua hoja hii au ile: nia ni kuvinyamazisha vyombo vya habari hasa vile vinavyofanya kazi zake vizuri.
   
 3. A

  August JF-Expert Member

  #3
  Jan 16, 2009
  Joined: Jun 18, 2007
  Messages: 4,509
  Likes Received: 723
  Trophy Points: 280
  na mbona hizi sheria zetu za uwekezaji hazipo uniform , bali zipo kiuchonganishi, kama mbona investment nyingine za foreignoirs siwe za hiyo 50% kwa 50%, eg trl, barick gold etc
   
 4. Japhari Shabani (RIP)

  Japhari Shabani (RIP) R I P

  #4
  Jan 16, 2009
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 721
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Tatizo la mwananchi na serikali sio uwekezaji au kitu kingine lengo la serikali ni kutaka kuvidhibiti vyombo vya habari katika uchaguzi 2010 .Hiii imethibitishwa na jitihada za serikali kutaka kumdhibiti Mengi na vyombo vyake vya habari kutokana na vyombo vyake vya habari hivi karibuni kubadiri mkondo na kuwaunga mkono walalahoi na si viongozi na CCM kamavilivyokua vikifanya hapo awali.Hapa serikali inapashwa kuangalia na kujifunza kwa vyombo vyake vya habari ambavyo vinamilikiwa kwa asilimia 100 na serikali ni vyombo dhaifu habari zake hazivutii ni propaganda hakuna zaidi.Nashangaa kuona vyombo vya habari vya serikali kama TBC,Radio Tanzania n.k havina hata web site.Ukiingia mwananchi au citzen kila siku utapata habari mpya bila kubagua kutoka CCM au wapinzani hoja zote ruksa.Hii ni changamoto kubwa katika maendeleo ya nchi.Na sio kuendelea kunyweshwa kauli za viongozi watawala zisizo na kichwa wala miguu ambazo nyingi inabidi waadishi wa habari wa vyombo hivyo ubidi kuwatafunisha viongozi wetu habari kwani zikiandikwa kama zilivyo ni aibu!Kwa mwandishi wa vyombo hivyo vya serikali hakuna hata aja ya kufuatana na kiongozi cha muhimu kufahamu nini alikua anatakakiwa akiseme katika mikutano hiyo na mwandishi kukaa na kutunga hadithi ya kauli za kiongozi muhusika.MUNGU IBARIKI TANZANIA.Advocate Jasha
   
 5. Japhari Shabani (RIP)

  Japhari Shabani (RIP) R I P

  #5
  Jan 16, 2009
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 721
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Hapa sio tatizo kati ya Mwananchi na serikali,hizi zote ni jitihada za serikali kutika jitihada zake kuvinyamazisha na kuvizidhibiti vyombo vya habari kabla ya uchaguzi.Kunamaovu mengi yanayotendeka wizi,ufisadi ,rushwa,viongozi wasio na sifa zauongozi katika CCM na serikali kwa vyombo kuyaweka mambo haya hadharani ni pigo kubwa kwa viongozi hao.Gazeti la mwananchi ni miongoni mwa magaziti ambayo yamekua yakitoa habari bila kupendelea upande wowote kitu ambacho ni hartari kwa CCM kwani wamezoe habari za upande mmoja kutoka CCM.Kwa sababu hizo hizo hivi karibuni tumeshuhudia vitisha kwa Mengi na vyombo vyake vya habari baada ya kubadiri mkondo na kuwaunga mkono walalahoi.Kwani alipokua akiinga mkono CCM hakukua na tatizo baada ya kuwageuka tatizo!Inaskikitisha kuona vyombo vya habari vya serikali mbali na kuendeshwa kwa kodi ya walala hoi bado ni dhaifu habari zake hazivutii ni nukuu kauli za viongozi wao matatizo ya wananchi hayazungumziwi.Vyombo kama TBC radio Tanzania havina hata web-sites.Mwishoni tuonana kuibuka magazeti kama uyoga yanayomilikiwa na mafisadi.Haya ni maandalizi ya mafisadi kuhakikisha wanafanya kila mbinu kubaki madarakani.TUWE MACHO MUNGU IBARIKI TANZANIA .Advocate Jasha
   
 6. D

  DURU JIPYA Member

  #6
  Jan 16, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 8
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  Ingekuwa haya yanasemwa kuhusu maeneo mengine ya Uchumi wetu/Biashara, nafikiri tungekuwa tumepiga hatua.

  Kuhusu huo mgogoro, mie naona wapambane tu.
  DJ
   
 7. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #7
  Jan 16, 2009
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,566
  Likes Received: 18,532
  Trophy Points: 280
  Hiyo sera mpya ya habari tunayoisubiri, ndio mwanzo wa yale tuliyokuwa tunayasema kuhusu wazawa, kama kweli itahitaji umiliki wa wazawa uwe zaidi ya asilimia 51% (majority share holder) na wageni wamiliki chini ya asilimia 49% (minority), serikali ilitakiwa ifanye hivyo kwenye sekta zote ukiwemo uwekezaji, viwanda, madini na ubinafsishaji. kinyeme cha hapo serikali inataka kafanya unafiki na double standard kwa kuibania sekta ya habari na kuachia sekta nyingine zote.

  leo Mkuu wa nchi ametembelea shirika la reli TRL na na kuamuru maamuzi makubwa yoyote yasifikiwe bila ridhaa ya serikali. Hii ni kauli ya ubabe wa JK ambayo haiendani na kanuni za umiliki. Wahindi wanamiliki 51% na serikali inamiliki 49%. Kwa mijibu wa kanuni za umiliki mwenye share kubwa ndio mwenye final say. Kama serikali ilitaka kubakiwa na final say, kwanini serikali ilikubali kuachia majority ishikwe na wahindi alafu leo inatoa amri kuwa na final say. 'You can't eat your cake and have it' its the same with 'you can't give away your cake and have it'.
   
 8. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #8
  Jan 17, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Nadhani serikali na watumishi wake wamechoka
   
Loading...