Serikali ina chakujifunza kutoka sekta Binafsi

Mparee2

JF-Expert Member
Sep 2, 2012
2,580
4,262
Wote tunajua kuwa Serikali haina fedha na ndio sababu Mama Yetu mpendwa anajitahidi Kwenda huko nje kukopa ILA cha kushangaza kila mwaka unasikia Mabilioni yameibiwa….
Na kingine cha kushangaza, nikupata hizo taarifa za wizi ulifanyika baada ya miezi kadhaa napengine miaka kadhaa. Hii inatuonesha kuwa, hatuna mifumo thabiti ya kuthibiti fedha/mapato ya Serikali.

Cha kujifunza kutoka sector Binafsi

Sio kwamba Sector Binafsia hawaibiwi ila wanachofanya; pale kunapo tokea wizi, Nguvu kubwa hutumika kuziba mianya ya wizi ikiambatana na kununua technologia mpya na kuajiri wataalamu wa Ushauri na technologia kwa ajili ya kuhakikisha matukio kama hayo hayatokei tena.
Private sector hata ikiibiwa nusu B inaona umuhimu wa kutumia hata zaidi ya B kuzuia wizi usitokee tena

Kwa upande wa Serikali, nguvu kubwa hutumika kupambana na wezi na kuzungushana mahakamani ambapo baadae huhukumiwa huku wakiacha milango ya kuiba ikiendelea kubaki wazi na ndio sababu Wizi unaofanana fanana huendelea kutokea kila mwaka
Yapo mengi ya Kujifunza ila leo nimeona nichangie hilo
 
Back
Top Bottom