Serikali imuondoe Paul Makonda haraka kabla mambo hayajaharibika. Tamko lijalo linaweza kuathiri nchi pakubwa

Acheni uoga, msidhani kwamba huyu dogo ataondolewa kwa presha za mzungu mmoja anayeishi Washington ambaye anao vibaraka wake humu nchini.

Hakuna kitu kama hicho.
 
brother ukimuona jirani yako anampiga mtoto wako Kama mbwa mwizi mbele ya macho yako, Jua wazi kuwa anaetafutwa hapo ni wewe mkubwa mwenzie.
Hicho ndicho kinachofanyika, hayo ni maneno tu ya kidipromasia ni aibu ya kuwaambia wazee wa baraza hadharani Kuwa wako uchi.
Kama watashupaza Shingo ujue wazi mabeberu hawatakomea hapo, lao ni Moja si umewasikia marafiki wetu wa jadi waswiss, baadae watapiga Pigo la pamoja baadae EU na wengine watafuata.
Tunasema wana maslahi kwetu tumeyakata na sasa wanatuadhibu!
Huo ni upande mmoja, je upande wa pili nao tunauzingatia?Tunaupa uzito gani?Maana sisi watanzania tunalo tatizo la kutaka kuangalia upande tunao upenda!
Vipi kuhusu Lisu? Tumesahau kuwa sisi ndio tumemfanya aanze kutangatanga huko duniani?
Nani anajari kuhusu maumivu yake?
Sio sisi tuliosema ni msaliti na asulubiwe na kweli akasulubiwa na maadui zetu, Ili sisi tuonekane mbele ya macho ya umma tumemsulubisha na lengo la maadui zetu kutuchafua litimie.
Ni sawa tumeshindwa kuwajibika kidogo hatuekuenda mbali kutaka kumjua Adui wa Adui yetu, hivyo tukamrahisishia adui yetu kutupaka matope huko duniani.
Tukawa tunasikia ataongea na kamati za EU, bunge la marekani na kwingineko sisi tukasema acha azulule! na tena Sisi Kwa hasira tukasema acha tumtekelezee haki zake za kibinadamu,timua ubunge, kataa kumtibia kwa sababu hatukujua alikokuwa.
ee sisi ni nchi huru bwana hatuingiliwi kwani nini?
Hatukutaka hata kujua wasio julikana ni akina Nani ili mladi wanatusaidia kwa kiwango Fulani.
Sababu kuwa tunapuuza haki za watu kuishi ni uongo na kipuuzi?
Sababu kuwa tumeviza haki zetu za kidemokrasia ni uongo? Uhuru wa sisi kukutana uko sawa na wawenzetu kukutana?
Hawa ni marafiki wa kweli wanaposema tuko uchi tuchutame harafu tusubiri Kama watatuomba dhahabu.

Ayo yote wapumbavu hawayafikirii waafrika sisi ni tatizo


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mi sioni kwanini aondolewe...hata wakitususa tuna utajiri wa kutosha ndiyo maana wao wanajipendekeza kwetu hata kama tuna madeni kibao hatujalipa bado wanatukopesha...Mwache Makonda afaidi zama zake hizi mpaka mwisho
Daaaah.!!! Hebu tutajie huo utajiri ni wa kiasi gani? Mbona analaumiwa Zito kwa kuzuia msaada? Hata matajiri wanalilia msaada? Hivi kumbe bajeti tunajitegemea 100% na zile 46% za msaada zinaliwa na machadema duuuuu!!!

Aisee wewe ni genius kweli!!!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndugu wana JF, kila mmoja amesoma tamko la hasira la Marekani juu ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam ndugu Paul Makonda.

Kwa desturi za USA, mlengwa mkuu hapo ni Rais Magufuli na serikali yake, walichofanya ni kuipima serikali yetu itamfanya nini Makonda baada ya wao kutangazia Dunia kuwa hawataki akanyage Marekani.

Makonda asipoondolewa, tujiandae kususiwa na Dunia nzima, maana Marekani ndio taifa lenye nguvu za kila aina Duniani.

Hata mataifa yanayojitegemea Kiuchumi yana ufyata kwa Marekani, sembuse sisi tunaojitegemea kwa asilimia 56%? Huku 44% tukitegemea kusaidiwa na Mabeberu?

Kama unajua trend reading, Ubalozi Marekani walikuwa wanatoa taarifa inayofanana na balozi nyingine kama ubalozi wa Ulaya, Uingereza nk.

Usishangae ndani ya siku chache ukawasikia washirika wa Marekani nao wakimpiga marufuku Makonda kukanyaga huko.

Kama serikali ikizembea kumfukuza Kazi Makonda ili kujisafisha, usishangae likatoka tamko la kuzuia misaada kwa Tanzania, halafu tuwekewe na vikwazo ikiwa ni pamoja na kuzuia watalii wasije Tanzania kwakuwa ni nchi hatari kiusalama.

Wazungu wanaweza kutukumia vyovyote, hambo la msingi na haraka ni kumuondoa Makonda ofisini na kuteua mtu mwingine atakaefanya tofauti.

Chonde Chonde washauri wa Rais Magufuli, tunawapenda sana na tunaipenda serikali yetu, Makonda Mmoja asiingize nchi kwenye mgogoro wa Kidiplomasia.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mboleko aliyobebewa imetoboka, ajiandae kuanguka.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Du! Basi akazane sijui kusali au kuroga maana ndani na nje kote kuchungu.
Hapana.

Kumpa ubalozi mtu mwenye madoa hivi ya haki za binadamu ni kuushusha hadhi ubalozi wa Tanzania.

Nawaheshimu mabalozi wa Tanzania kama watu wenye weledi. Hata kama wana mapungufu, si kama haya ya kusababisha diplomatic war na Marekani.

Nazungumzia mabalozi kama balozi Benjamin William Mkapa, balozi Ali Hassan Mwinyi, balozi Salim Ahmed Salim, balozi Augustine Philip Mahiga, balozi Ami Mpungwe, balozi Jaka Mwambi, balozi Mustapha Nyang'anyi, balozi John Samuel Malecela, balozi Nsilo Swai, balozi Paul Milyango Rupia, balozi Abbas Kleist Sykes, balozi Crispin Mbapila, balozi George Magombe, balozi Wilbert Kumalija Chagula, balozi Juma Volter Mwapachu, balozi Juma Maharage na mabalozi wengine wengi wa kada hiyo.

Sasa unataka kumuweka Makonda kwenye kada hiyo baada ya uchafuzi alioufanya, hawa wazee wote wenye heshima zao duniani nao wawe kundi moja na Makonda?

Utaushusha hadhi sana ubalozi wa Tanzania.

Najua ubalozi wa Tanzania ushahuka hadhi, lakini usitake kuushusha zaidi.

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naomba kujua Elimu yako plz
Ulimwengu huu wa teknolojia ambapo kuna mambo kama utandawazi na mengineyo unanishangaza sana. Ni wakati ambapo mtu anawe za kuanzisha habari kubwa na kuisambaza.

Turudi kwenye hoja, Suala la RC Makonda na familia yake kuzuiwa kuingia Marekani. Binafsi nimeiona kwenye ukurasa wa Twitter wa Waziri wa Mambo ya Nje Marekani.

Pamoja na habari hizo kusambaa kwenye vyombo mbalimbali vya habari nchi na duniani, naomba niulize hivi:
  • Ndugu wanahabari, mmeshindwa kweli kwenda kwa ofisi ya inayowakilisha serikali ya Marekani (ubalozi) ambapo ndipo RC alipoombea visa?
  • Mmeshindwa kupata msemaji mwakilishi mpaka mtoe vyanzo vyenu vya habari kwenye mitandao ya kijamii au vyombo vya nje wakati nyinyi ndio nchi husika?
  • Mmeshindwa kumfuata RC Makonda pale Ilala Boma na kuomba azungumzie waraka huo uliosambaa?
  • Hamuoni ajabu ofisi wakilishi ya serikali ya Marekani ambayo ndiyo inahusika na kutoa vibali kukaa kimya mpaka sasa?
  • Mnapata wapi ujasiri wa kuweka habari kubwa na nzito kwenye ukurasa wa mbele wa gazeti lako kwa habari iliyoanzia kwenye mitandao ya kijamii?
Kwa huku tulipofikia inasikitisha.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom