Serikali imuondoe Paul Makonda haraka kabla mambo hayajaharibika. Tamko lijalo linaweza kuathiri nchi pakubwa

USA huwa wanadeal na mtu specific ndiyo maana ameguswa yeye
Kama huwa wanadeal na mtu specific iweje wazuie raia wasio na hatia kucheza bahati nasibu ya green card lottery!? Hawa raia wana kosa gani?.
 
Atumbuliwe kwa kosa gani wewe wakati mtu anafanya kazi nzuri. Hebu nieleze biashara ya madawa ya kulevya iko kama zamani? Vijana wamenusurika wangapi. Wauzaji awamejaa korokoroni ndio hao wanalilia kichwa cha makonda. Kuna hospitali kule chanika imejengwa kwa juhudi za makonda..kuna mambo mengi ukurada hautoshi. Mwacheni makonda afanye kazi.
Jibuni hoja ya wamarekani .kwani wewe wangekupa URC. Wa DSM.vyombo vyote vya ulinzi vyako ungeshindwa dhibiti madawa ya kulevya? Jibuni hoja kimkakati!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukifuatilia vizuri utaona Magufuli plan zake zote toka mwanzoni zinalead sehemu moja tu, anataka Tanzania igeuke kua kama China under communist party. One man controls the party, one man controls the entire country, anareplace mtu yeyote ambaye anapinga kitu chochote regardless anachopinga ni sahihi au la anaweka watu ambao kazi yao ni kusifia 24/7 hata kama hawafit kazi wanayopewa. So far his plan is working perfectly.
 
Atumbuliwe kwa kosa gani wewe wakati mtu anafanya kazi nzuri. Hebu nieleze biashara ya madawa ya kulevya iko kama zamani? Vijana wamenusurika wangapi. Wauzaji awamejaa korokoroni ndio hao wanalilia kichwa cha makonda. Kuna hospitali kule chanika imejengwa kwa juhudi za makonda..kuna mambo mengi ukurada hautoshi. Mwacheni makonda afanye kazi.
Mbona huandiki na wangapi wamepoteza maisha kwa sababu yake? Usijitie macho kumchuzi kuona upande mmoja tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yaani mnataka kutuaminisha kuwa Makonda ni One man army?? Hao wenzake ni kina nani?? Tulieni tu jamani mambo haya yatakwisha ni upepo wa kisulisuli tu utapita
Nigeria na Elitrea wamezuiliwa nchini nzima wao wafamyeje?
 
Baada ya tangazo la Serikali ya Marekani kumzuia Makonda na familia yake kupata visa ya Marekani Kuna uwezekana mkubwa huo ndiyo ukawa mwisho wa Makonda kisiasa.

Tangazo hilo halijatoa Picha nzuri kwa uongozi wa awamu ya tano na ili kurudisha heshima na mahusiano hayo tena ni Makonda kuondolewa katika nafasi ya Mkuu wa mkoa haraka Sana.

Wamerakani watakawa wametuma makachero wao ndani ya nchi Kama majasusi bila tz kujua na uwezekano wamekuja Kama watalii na kukusanya habari nyingi Sana za ndani ya mifumo ya Serikali.

Ni wakati umefika RC aondoke haraka katika nafasi hiyo.

Ni aibu kubwa sana kwa nchi kwa tangazo hilo.
Uhitaji kuwa mtalii ili ujue siri za nchi social media ni good source ya information yeyeto ya nchi yeyeto uitakayo.Sasa mtalii ajui lugha,pia Simu zote kumbuka zinarekodiwa jiulize kwanin Osama alikuwa atumii Simu.Kama wanawezayanasa mawasiliano ya siri ya magaidi sembuse ya washamba.
Kikwazo cha utumbuzi ndie mbeba siri,na TV bila remote haitowezawaka
 
Tatizo ni pale unapouliza Magufuli anakwama wapi kwa huyu Makonda, wakati Magufuli hajawahi kuwa na consistent and coherent agenda popote.

Hapa atakwambia anapiga vita rushwa, kule kauza nyumba za serikali nje ya utaratibu mpaka kwa hawara zake. Pia anasema trafiki kupewa rushwa ni "hela ya kupiga viatu brashi tu".

Hapa atakwambia yeye ni rais wa wanyonge, na maendeleo hayana vyama, pale atakwambia atapiga wapinzani mpaka shangazi zao.

Hapa atamfukuza kazi Kangi Lugola kwa kupiga dili ambalo halijapitia bungeni, kule atanunua ndege bila idhini ya bunge, tender ya wazi wala kuruhusu ukaguzi wa CAG ATCL.

Hapa atasema anawakilisha maslahi ya wakulima wanyonge, halafu hapo hapo ataingilia manunuzi ya korosho na kuharibu soko kwa namna ambayo inaangusha mapato ya mazao ya kilimo kwa asilimia 55 katika mwaka mmoja tu unaoishia Agosti 2019, kwa mujibu wa ripoti ya Bank of Tanzania ya Oktoba 2019.

Sasa mtu kama huyu utategemea vipi ajielewe zaidi ya wholesale politics?

Na watu waliokuwa sane serikalini waliotaka kummdhibiti Makonda na kufanya "damage control" kama kina Dr. Mahiga ndiyo wanaondokewa kwenye prominence. Go figure.

Wizara ya Mambo ya Nje sasa hivi tungehitaji sana watu wenye busara na uzoefu wa kimataifa. Lakini wameondolewa, wamewekwa die hard ideologues waimba sifa. Clear mesage kwamba hatutaki watu wa busara, tunataka watu wa kujikomba kwa mkuu.

For all I know yeye Magufuli na Makonda hawajapishana sana katika kufikiri, na sasa wanaandaa vita dhidi ya "mabeberu".

Sent using Jamii Forums mobile app

Bandiko Murua kabisa hili. Watanzania wengi wana good will na JPM. Swali gumu labda ni kama haiwezekani kufanya yoooote anayoyafanya bila kuhangaishana na wakosoaji wake. Kwa mwenye akili anajua.....Raia 55 million hatuwezi kuwa na fikra sawa. Never! Kuandika yasipoandika magazeti ya ndani..ya nje yataandika. Na hiyo ndo mbaya Zaidi.

JPM asiporudi nyuma aka-focus kwenye agenda zake akaacha kukimbizana na wapinzani na wakosoaji wake..he will fail na historia itamkumbuka kwa mabaya..wakati miradi mikubwa kama SGR ingemuweka kwenye sehemu sahihi ya historia ya nchi yetu.

Huwezi kuendesha nchi kubwa kama Tanzania kama mtu mmoja na marafiki wajinga wachache kama akina Makonda. Lazima ukubali hulka ya binadamu ni tofauti. Haiko hivyo. Tumeumbwa kuhoji. Tumeumbwa kuudhi. Tumeumbwa na madhaifu mengi sana. Kikubwa usitoke kwenye reli. Ukisema uwapige risasi kwa sababu ya kuudhi..utawapiga wangapi??? ukisema uwafunge, utawafunga wangapi?

Eti Umuue Zitto kwa faida ipi? Risasi za Lissu zitaendelea kuwa kwenye doa jeusi kwa awamu hii. Was it worth it? Not sure!
 
Anakwama hapo
masoudkipanya_20200203_1.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
CCM wanamtegemea huyu Makonda, nyie mnataka atoke.
Ataenda wapi?!

Mkimvua madaraka simtamuua kama kibaka?!

Huyo nchi hii hatosalimika akiachwa bila ulinzi atauwawa labda akatunzwe mahabusu au magereza for a long time.
 
Marekani imesema: Makonda ni mkandamizaji wa haki za kibinaadamu ikiwemo haki ya kuishi (kwa tafsiri isiyo rasmi ni kuwa anahusika na mauaji ya raia); haki ya kidemokrasia na nyinginezo. Anapaswa kuwekwa kando haraka!

Marekani imetega mtego usio na magego. Mtego mkali. Mtego wao unaanzia kwenye swali la kiudadisi: Makonda amefikiaje kukandamiza haki za kibinaadamu hadi kupigwa marufuku ya kuingia Marekani akiwa amezungukwa na wakuu wake(ukiwemo Mwenyekiti wangu) waliopaswa kumdhibiti?

Marekani imeamua kukusaidia kujitenga na Makonda. Marekani imekutega Rais na Mwenyekiti wangu Dr. John Pombe Magufuli. Imekusaidia na kukupa nafasi adhimu. Jitenge na Makonda kabla ya mambo mrama kwenda!

Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam
 
Back
Top Bottom