Serikali imuondoe Paul Makonda haraka kabla mambo hayajaharibika. Tamko lijalo linaweza kuathiri nchi pakubwa

MO siku sio nyingi nae atazuiwa kuingia marekan maana yeye mshauri wake mkuu ni Makonda labda POMPEO asijue tuu
 
Siyo kwamba najigamba au kujidai. Ni ukweli tu. Ukweli kwamba, katika watu waliom-‘define’ huyu ‘Gavana’ wa Dar es Salaam humu jukwaani, basi mimi ni mmoja wa watu walio juu katika orodha ya watu hao.

Hizi siku mbili tatu nimejiuliza maswali mengi sana.

Mojawapo ni hili: hivi huyu Rais wetu anakwama wapi?

Manake haiingii akilini kabisa. Kuna watu wengi tu ambao kawatumbua ‘unceremoniously’ kwa makosa madogo kabisa yasiyo stahili hata kuwa sababu ya mtu kutumbuliwa.

Lakini ikija kwa huyu ‘Gavana’, licha ya makosa yake yote, Rais mpaka leo hajamtumbua.

Mpaka Wamarekani nao wameona. Si ajabu wameona siku nyingi tu lakini wakawa wanavuta muda kuona kama Rais atatumia madaraka yake na kutenda [kumtumbua], lakini wapi.

Wamesubiri mwishowe na wao wamechoka. Sasa wameamua kutenda kwa kadri wawezavyo.

Huyu Rais wetu huyu...kama somo halielewi, ina maana na picha nayo haioni?

Anakwama wapi huyu Rais wetu?

Haya, pale wizara ya mambo ya nje kamtoa waziri ambaye ni mwanadiplomasia mbobezi halafu kamweka Kabudi!

Huyu Kabudi ataweza kweli ku ‘navigate the murky waters of international diplomacy’?

Ona alivyoenda Kenya kwenye ule uzinduzi wa ripoti yao ya BBI!!

Kaenda katoa mahubiri utadhani huko alikotoka ni peponi.

Kilichotokea kwa ‘gavana’ sidhani kama kimewahi kutokea [unprecedented].

Ila sasa kimetokea. Chini ya utawala wa Magufuli.

Magufuli anakwama wapi? Hana hekima? Busara?
 
Kwa watu waliowahi kuandika tafiti nadhani wananielewa, huwezi kupata Alama nyingi kama vyanzo vya tafiti ni kwenye dawati tu, nakumbuka kiongozi wangu alikuwa hakubali kabisa tafiti zilizo kuwa cited kutoka kwenye online links, pamoja na kwamba zinaweza kuwa na ukweli lakini inaonyesha uvivu wa kutafuta taarifa sahihi
 
17353465_1346268955433008_6567779633624083107_n-1.jpg
 
Ulimwengu huu wa teknolojia ambapo kuna mambo kama utandawazi na mengineyo unanishangaza sana. Ni wakati ambapo mtu anawe za kuanzisha habari kubwa na kuisambaza.

Turudi kwenye hoja, Suala la RC Makonda na familia yake kuzuiwa kuingia Marekani. Binafsi nimeiona kwenye ukurasa wa Twitter wa Waziri wa Mambo ya Nje Marekani.

Pamoja na habari hizo kusambaa kwenye vyombo mbalimbali vya habari nchi na duniani, naomba niulize hivi:
  • Ndugu wanahabari, mmeshindwa kweli kwenda kwa ofisi ya inayowakilisha serikali ya Marekani (ubalozi) ambapo ndipo RC alipoombea visa?
  • Mmeshindwa kupata msemaji mwakilishi mpaka mtoe vyanzo vyenu vya habari kwenye mitandao ya kijamii au vyombo vya nje wakati nyinyi ndio nchi husika?
  • Mmeshindwa kumfuata RC Makonda pale Ilala Boma na kuomba azungumzie waraka huo uliosambaa?
  • Hamuoni ajabu ofisi wakilishi ya serikali ya Marekani ambayo ndiyo inahusika na kutoa vibali kukaa kimya mpaka sasa?
  • Mnapata wapi ujasiri wa kuweka habari kubwa na nzito kwenye ukurasa wa mbele wa gazeti lako kwa habari iliyoanzia kwenye mitandao ya kijamii?
Kwa huku tulipofikia inasikitisha.
kwani yanayotokea Iran kwa asilimia kubwa yamesababishwa na malumbano kupitia mtandao upi mtoa mada kama sio Twitter. na vipi je hauoni impact zake??? ukiacha Tanzania..kuanzia kenya na nchi zingine zenye Raia na viongozi Smart, Mtandao wa Twitter ndio reliable source of information. na ndio maana twitter wana word count ili ku limit contents za ku publish. only useful informations have a place in Twitter.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukitaka upepo ubadilike gusa maslahi ya elites-wale wenye nacho... Siku nyingi wanyonge wameongea sana humu kuhusu hizi dhulma lakini hakuna anayewasikiliza. Ila sasa wakina Pompeo wakiongea...wakaanza kuwanyima visa akina Mwanakijiji na wengine kama wao (pole mzee mwenzangu)....wenye nyumba na mapesa huko ulaya....utaanza kuona JF na kwingineko kunabadilika. Kwa sasa kila anayelalamika ni mpiga deal...mda utafika tutaongea lugha moja tuu. Na Pompeo anajua. Mwananchi wa Kazuramimba haendi Ulaya. Wanaoenda wapo na anawajua. Tutaelewana tuu.
 
Masanja....@Mzee Mwanakijiji kanyimwa viza?
 
kwani yanayotokea Iran kwa asilimia kubwa yamesababishwa na malumbano kupitia mtandao upi mtoa mada kama sio Twitter. na vipi je hauoni impact zake??? ukiacha Tanzania..kuanzia kenya na nchi zingine zenye Raia na viongozi Smart, Mtandao wa Twitter ndio reliable source of information. na ndio maana twitter wana word count ili ku limit contents za ku publish. only useful informations have a place in Twitter.

Sent using Jamii Forums mobile app
Sourcing news from Twitter is not professional
 
Back
Top Bottom