Serikali, imulikeni shule ya Dare Intergrated English Medium

Ikinena

New Member
Mar 19, 2019
4
13
Wahusika hapo juu naomba muimurike shule hiyo ipo Kimara. Walimu wananyanyaswa sana hamna mikataba, wanalazimishwa kuripoti saa kumi na moja alfajiri wanatoka saa tatu usiku.

Juzi juzi wakaguzi walikuja wakahongwa wakaondoka bila ukaguzi wowote. Hakuna mwalimu anayelipwa laki nne wote ni chini ya hapo.

Kuna manyanyaso ya kufa mtu pale sema ajira hamna watafanyaje!

Watanzania tumefikia hatua ya kulia kazini mpaka tunajuta kwanini tulisoma.

Mishahara japo midogo lakini inalipwa tarehe 37 au 38 au mwezi mzima hamna mshahara ukiuliza tu unafukuzwa na mshahara hupewi tena unaambiwa nenda popote.
 
Nadhani umewasilisha vyema na kwa hisia hii kero. Tatizo hili lipo katika shule nyingi. hakuna mikataba, mishahara kiduchu isiyojulikana inalipwa lini, saa za kazi hazi zingatiwi hata kidogo. Nadhani kama waziri hawezi fuatilia hizi ajira katika shule hizi ni sawa na wizara kumshinda. Katika hili tupaze sauti. Lahama kuna shule nyingi nazifahamu kufanya hivi.
 
Iko hivi. Anachosema mtoa mada kina ukweli mtupu tatizo na yeye kaishia kwa walimu tu lakini waajiri wanaotoa mikataba ya kazi sidhani kama wanafika hata asilimia 30 hapo nchini.

Unakumbuka mwaka 2005 madereva karibu nchi nzima hawakuwa na mkataba wa kazi.

Hata waandishi wa habari na watangazaji wa Televisheni vituo vingi havina mkataba wa kazi tena vingine wanalipwa kwenye bahasha na hata NSSF au kodi yaani PAYE hawapeleki!
Ukiachilia mbali mikataba ya kazi yaani Employment Contract waajiri karibu asilimia 80 hawatoi Job Description na wafanyakazi hawajui kama ni document ya muhimu kuliko hata Employment Contract.

Solution ni kwamba Waziri atangazae kila mwajiri ndani ya miezi sita au chini ya hapo ahakikishe amegawia wfanyakazi wake Employment Contract na Job Description na hivyo ukaguzi ukifanyika na mwajiri akakutwa hana faini atakayopigwa kwa kila mfanyakazi itamfanya asirudie uzembe huo.
 
Shule nyingi za private zinanyanyasa walimu. Hamna mikataba na anaweza kukufukuza hata kwenye simu usiku. Saa za kazi hazieleweki. Mhagama kwani kazi yako ni kujibizana na wapinzani bungeni tu? Au jpm anakulinda tu yawezekana mnakutana kitandani
Ni binadamu aliyesoma mpka akaitwa mwalimu anashindwa kukabiliana ha hali kama hiyo mpaka anategemea waziri ndiyo aje amfundishe kusaini mkataba mzuri wa kazi na haki zake katika kufukuzwa kazi? Basi huyu siyo mwalimu bali ni kinyago kinachofanana na mwalimu!
 
Nadhani huyu ndugu Mwita Mura Waitara angepaswa kuhakikisha shule hizi zinatoa mikataba jaman. Kwanza mda mwingne mwanamke akishika mimba akipewa maternity leave ndo jumlaa,,harudi. Mwitaaaaaa toka ofisini tembea ukawaone hawa watu,
 
Wenye AKILI wamemuelewa aliposema tarehe 38! Amehesabia mpaka imefika tarehe 31 kwa matumaini na kuwaahidi wengine " kimya!" Kukumbuka kuwa tarehe zina rudi nyuma kuna kazi.
 
Nawe ni mwalimu hapo?, kama ndio uandishi huu hukustahili kuwa mwalimu.

Hadi kuna tarehe 38 kumbe?

Acha kazi mzee, sio lazima uendelee kufanya kazi sehemu yenye manyanyaso.

Sent using Jamii Forums mobile app
tar. 38 ni lugha ya picha kuonesha mishahara inachelewa badala ya tar. 25 unakuja pokea tar. 13 ya mwezi ulio fuata.

nimeshangaa sana kuchukulia tar.38 kama kuna tar. iyo nawe una tatizo kwenye uelewa wako.
 
Tatizo la ajira limefanya waajiri kuwa na viburi. Mwenye shule akiangalia barua za maombi zinatosha kuajiri walimu mara tatu ya mahitaji ya walimu shuleni kwake. kinachofuata kuporomosha elimu.
 
Back
Top Bottom