Serikali imezitaka kamati za ulinzi na Usalama nchini, kuwakamata watoto wote wanaozagaa wakiombaomba

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,492
54,890
Salaam Wakuu,

Naibu Waziri TAMISEMI Joseph Kakunda, ameagiza wakuu wa Wilaya wote nchini kukamata watoto wanaozagaa mitaani wakiombaomba na Wazazi wao kisha wafikishwe mahakamani.

"Nawaagiza wakuu wa wilaya, wakurugenzi wa Halmashauri chini ya usimamizi wa wakuu wa mikoa kupitia kamati za ulinzi kuwakamata watoto wote ambao huzagaa wakiombaomba, wawakamate pamoja na wazazi wao na washtakiwe mahakamani" amesema Kakunda.

Hii si mara ya kwanza tamko kama hili. Walemavu ambao ni wapiga kura wa Magufuli ndo mara nyingi wamekuwa wakipinga jambo hili kwani hupokea uamuzi huo kwa shingo upande huku baadhi ya raia wakisema kwamba uamuzi huo unakuwa na lengo la kukandamiza walemavu na watu maskini.

Mimi nashauri, hawa watoto wakamatwe na kupelekwa mashuleni na vituo vya kulelea watoto yatima. Mahakamani na Magerezani tuwaachie Wahalifu na Watuhumiwa.

Serikali inakimbia majukumu yake kama vile haikusanyi kodi. Serikali inatakiwa iweke mikakati ya kuwakusanya hao watoto na kuwasaidia. Itenge ruzuku kwa lengo hilo kama wanavyofanya kwa kaya Masikini sababu hawa watoto ni watoto wa masikini.

Mkakati wa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umaskini Tanzania, MKUKUTA na mpango wa kurasimisha rasilimali za wanyonge kwa lengo la kuhakikisha wanazitumia kuukimbia umasikini Mkurabita, ndo kazi yao hii. TASAF tuseme hawawaoni hawa watoto?. Ruzuku wanayopata inaenda wapi

Tuache kufanya kazi kisiasa badala yake tujikite kutatua tatizo. Tuwasaidie Watanzania wenzetu badala ya kuwapelega Gerezani.

Tanzania mbona inasaidiwa na nchi wahisani, kuna ubaya gani kuwasaidia hawa ombaomba? Serikali ifanye Tathimini kujua wapo wangapi, wasaidiwe then ndo tuanzie hapo kuwadhibiti tukiwa tushawajengea mazingira mazuri.

======

Dodoma. Serikali imewaagiza wakurugenzi wa halmashauri na majiji kuwakamata watoto wanaombaomba mitaani ili washtakiwe kwa mujibu wa sheria inayokataza utoro shuleni.

Agizo hilo limetolewa bungeni leo na Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tamisemi, Joseph Kakunda ambaye amesema ombaomba bado ni tatizo katika jiji la Dar es Salaam.

Kakunda alikuwa akijibu swali la Ibrahim Raza Mbunge wa Kiembe Samaki, ambaye alihoji ni lini serikali itachukua hatua kuwaondoa ombaomba katika jiji la Dar es Salaam.

Naibu Waziri alisema ombaomba wengi wanakwenda katika jiji hilo kwa sababu kuna vivutio vingi vinavyowapa nafasi ya kupata fedha kama sehemu ya ibada.

Hata hivyo, alisema mara nyingi ofisi ya mkuu wa mkoa imekuwa ikichukua hatua za kuondokana na tatizo hilo kwa kuwarudisha makwao.

"Mfano Septemba 2013, ombaomba 253 na watoto 135 walirejeshwa kwao, ambapo watoto 32 walirejeshwa shuleni na hii inathibitisha kuwa wapo watu wazima wanaowatumia kuomba, nawaagiza wakurugenzi kuwakamata watoto wote wanao ombaomba mitaani ili washtakiwe kwa mujibu wa sheria inayokataza utoro mashuleni,” alisema Kakunda.

Chanzo: Mwananchi
 
Back
Top Bottom