Serikali imezipiga marufuku taasisi zote za Umma nchini kujenga mifumo ya fedha ya kieletroniki bila ridhaa ya Wizara ya Fedha

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,797
11,959
Peter Haule na Farida Ramadhani, WFM, Dodoma

Selikali imezipiga marufuku taasisi zote za Umma nchini kujenga mifumo ya fedha ya kieletroniki bila ridhaa ya Wizara ya Fedha na Mipango na Mamlaka ya Serikali Mtandao (eGA).

Agizo hilo limetolewa Jijini Dodoma na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James, wakati akizundua Mfumo wa Malipo ya Serikali kwa njia ya Kielektroniki (GePG) toleo la simu za mkononi (GePG App), hafla iliyowakutanisha Wizara ya Fedha na Mipango na Idara, Wakala, Taasisi, Bodi, Mashirika ya Umma yaliyo katika Kanda ya Kati.

Bw. James alisema kuwa Taasisi zote za Umma nchini zinatakiwa kutekeleza matakwa ya Waraka namba tano (5) wa Hazina unaozitaka taasisi zote kuhakikisha zinapata ridhaa ya Wizara ya Fedha na Mipango na Wakala wa Serikali Mtandao (eGA) kabla ya kufanya ununuzi, uandaaji, usimikaji na utumiaji wa Mfumo wowote wa kielektroniki wa usimamizi wa Fedha za Umma.

“Imebainika kuwa kuna baadhi ya taasisi za umma ambazo zinakiuka maelekezo hayo ya Serikali kwa sababu wanazozijua wao, nitumie fursa hii kutoa onyo kwa taasisi hizo kutoendelea na vitendo hivyo kwa sababu ni ukiukwaji wa maelekezo”, alisema Bw. James.

Akizungumzia kuhusu GePG App, Bw. James alisema kuwa, uboreshaji wa Mifumo ya Kielektroniki inayoandaa Ankara itawezesha kukusanya fedha kwa wakati na kutoa huduma bora kwa Umma.

“Baadhi ya faida za Matumizi ya Mfumo huo ni kuongezeka kwa uwazi na udhibiti katika ukusanyaji wa fedha za umma, kupata taarifa sahihi na kwa wakati zinazohusu makusanyo na kuwa na viwango na utaratibu unaofanana katika ukusanyaji wa fedha za umma kwa taasisi zote za umma”, alisema Bw. James.

Alisema faida nyingine ni pamoja na kuchochea ubunifu katika ukusanyaji wa pesa za Serikali na sekta ya fedha kwa ujumla kwa kuweka mazingira rafiki na ya usawa kwa wakusanyaji, kutoa huduma bora na rahisi ya malipo ya fedha za umma hivyo kuchochea ongezeko la makusanyo na kufika haraka katika akaunti kuu za makusanyo za taasisi.

“Kwa kutofanya usuluhishi wa miamala kwa wakati kunaweza kusababisha upotevu wa fedha nyingi za Umma na pia kuwa na taarifa za fedha zisizo sahihi, hivyo nawaagiza nyote kuhakikisha mnafanya usuluhishi wa miamala inayopitia Mfumo wa GePG kwa usahihi na kwa wakati, na kufanyia kazi kwa wakati changamoto mbalimbali zitokanazo na matokeo ya usuluhishi wa Miamala husika”, alisisitiza Bw. James.

Aidha alimpongeza Mkurugenzi wa Mifumo ya Usimamizi wa Fedha wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. John Sausi pamoja na timu yake ya wataalam wabobezi kwa kutengeneza Mfumo wa Kieletroniki wa Kukusanya Mapato ya Serikali (GePG) sambamba na toleo la simu za mkononi (GePG App) ambao umerahisisha ukusanyaji wa mapato ya Serikali pamoja na kuwawezesha wadau kupata huduma kwa wakati.

Aliahidi kuwa Wizara yake itaendelea kuiwezesha Idara hiyo ili iweze kutekeleza majukumu yake ya kubuni mifumo kama hiyo kwa faida ya Serikali na wananchi kwa ujumla.

Aidha, Bw. James ambaye pia ndiye Mlipaji Mkuu wa Serikali, alisema kuwa Wizara kupitia Idara ya Mifumo ya Usimamizi wa Fedha inaandaa mfumo mwingine utakaotumika kwa ajili ya matumizi ya Serikali ujulikanao kwa kifupi kama MUCE.

“Mfumo huu umeshaanza kufanyiwa majaribio kwenye taasisi chache za umma na baadae utasambazwa kwenye taasisi zote na kwamba Mfumo huu utakuwa mwarobaini wa matumizi yasiyo sahihi ya fedha za Umma”, aliongeza Bw. James.

Alisema Mfumo huo utakuwa suluhisho la matumizi yasiyofaa ya umma na kuongeza kuwa watendaji wengi Serikalini hawataufurahia mfumo huo lakini hilo haliihusu Serikali. Watajua wenyewe! Alisema huku washiriki wakiangua kicheko ukumbini.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Mifumo ya Fedha, wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. John Sausi, alisema kuwa kabla ya kuwa na Mfumo wa Malipo kwa njia ya Kielektroniki (GePG) ilikua inafanyika miamala 10 kwa siku na baada ya mfumo huo inafanyika miamala milioni moja kwa siku.

Alisema kuwa miongoni mwa mafanikio ni kuongezeka kwa Taasisi zinazotumia Mfumo wa GePG, kutoka taasisi 300 muda mfupi uliopita hadi kufikia taasisi 620 hivi sasa.

Bw. Sausi alisema kuwa Mfumo wa GePG kwa njia ya mtandao wa simu za mkononi uliozinduliwa utasaidia watumiaji kupata huduma mbalimbali kama vile kununua umeme, kulipia Ankara mbalimbali zikiwemo za makosa ya usalama barabarani, maji na nyingine nyingi ndani ya sekunde 30.

Ametoa wito kwa wananchi wanaotumia simu janja (android au IPA App) kupakua application hiyo kupitia play store au App Store na kutafuta neno GePG Tanzania tayari kwa matumizi yao ambayo amesema wananchi watafurahia huduma hiyo.

Naye Mwakilishi wa Benki katika Mkutano huo, Bi Domina Tarimo na Mwakilishi wa kampuni za Simu, Bw. Alafat Ibrahim, walisema kuwa Mfumo wa GePG umezisaidia kwa kiasi kikubwa kurahisisha kazi zao, na kuboresha huduma kwa wateja wao na wameipongeza Wizara ya Fedha na Mipango na Serikali kwa ujumla kwa jitihada zake za kuhakikisha kuna mifumo imara ya fedha inayoongeza uwazi na uwajibikaji.
1.JPG

Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipasngo, Bw. Doto James (wa pili kulia), akizundua Mfumo wa Malipo ya Serikali kwa njia ya Kielektroniki (GePG) toleo la simu za mkononi (GePG App), katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dodoma
2.JPG

Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James Selikali akiziagiza taasisi zote za Umma nchini kutojenga mifumo ya fedha ya kieletroniki bila ridhaa ya Wizara ya Fedha na Mipango na Mamlaka ya Serikali Mtandao (eGA), wakati wa hafla ya uzinduzi wa Mfumo wa Malipo ya Serikali kwa njia ya Kielektroniki (GePG) toleo la simu za mkononi (GePG App), katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dodoma.
3.JPG

Mkurugenzi wa Mifumo ya Fedha wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. John Sausi, akielezea mafanikio ya Mfumo wa Malipo ya Serikali kwa njia ya Kielektroniki (GePG) ambapo awali miamala 10 ilikua ikifanyika kwa siku na sasa miamala milioni moja inafanyika baada ya matumizi ya mfumo huo.
4.JPG

Baadhi ya wajumbe wa Benki nchini, wafuatilia kwa makini maagizo ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipasngo, Bw. Doto James (hayupo pichani), wakati wa hafla ya uzinduzi wa Mfumo wa Malipo ya Serikali kwa njia ya Kielektroniki (GePG) toleo la simu za mkononi (GePG App), katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dodoma.
5.JPG

Mwakilishi wa Benki nchini Bi. Domina Tarimo, ), akieleza faida ya Mfumo wa GePG katika kuongeza ufanisi na uwazi katika shughuli za kibenki, wakati wa uzinduzi wa toleo la simu za mkononi (GePG App), Jijini Dodoma.
6.JPG

Wataalam wa Mfumo wa Malipo ya Serikali kwa njia ya Kielektroniki (GePG) toleo la simu za mkononi (GePG App), wakiwa katika hafla ya uzinduzi wa Mfumo huo Jijini Dodoma.
7.JPG

Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James (katikati), akiwa katika picha ya pamoja na Wakurugenzi na wataalamu wa mifumo ya fedha na wengine, baada ya uzinduzi wa Mfumo wa Malipo ya Serikali kwa njia ya Kielektroniki (GePG) toleo la simu za mkononi (GePG App), katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dodoma.

(Picha na Peter Haule, WFM)
 
View attachment 1320573
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipasngo, Bw. Doto James (wa pili kulia), akizundua Mfumo wa Malipo ya Serikali kwa njia ya Kielektroniki (GePG) toleo la simu za mkononi (GePG App), katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dodoma
View attachment 1320575
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James Selikali akiziagiza taasisi zote za Umma nchini kutojenga mifumo ya fedha ya kieletroniki bila ridhaa ya Wizara ya Fedha na Mipango na Mamlaka ya Serikali Mtandao (eGA), wakati wa hafla ya uzinduzi wa Mfumo wa Malipo ya Serikali kwa njia ya Kielektroniki (GePG) toleo la simu za mkononi (GePG App), katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dodoma.
View attachment 1320582
Mkurugenzi wa Mifumo ya Fedha wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. John Sausi, akielezea mafanikio ya Mfumo wa Malipo ya Serikali kwa njia ya Kielektroniki (GePG) ambapo awali miamala 10 ilikua ikifanyika kwa siku na sasa miamala milioni moja inafanyika baada ya matumizi ya mfumo huo.

Baadhi ya wajumbe wa Benki nchini, wafuatilia kwa makini maagizo ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipasngo, Bw. Doto James (hayupo pichani), wakati wa hafla ya uzinduzi wa Mfumo wa Malipo ya Serikali kwa njia ya Kielektroniki (GePG) toleo la simu za mkononi (GePG App), katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dodoma.

5.

Mwakilishi wa Benki nchini Bi. Domina Tarimo, ), akieleza faida ya Mfumo wa GePG katika kuongeza ufanisi na uwazi katika shughuli za kibenki, wakati wa uzinduzi wa toleo la simu za mkononi (GePG App), Jijini Dodoma.

6.

Wataalam wa Mfumo wa Malipo ya Serikali kwa njia ya Kielektroniki (GePG) toleo la simu za mkononi (GePG App), wakiwa katika hafla ya uzinduzi wa Mfumo huo Jijini Dodoma.

7.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James (katikati), akiwa katika picha ya pamoja na Wakurugenzi na wataalamu wa mifumo ya fedha na wengine, baada ya uzinduzi wa Mfumo wa Malipo ya Serikali kwa njia ya Kielektroniki (GePG) toleo la simu za mkononi (GePG App), katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dodoma.

(Picha na Peter Haule, WFM)
Kwenye Automation kutoka analojia kwenda digitali hii Serikali ya Rais Magufuli iko vizuri sana!
Zama za Upigaji wa Pesa za Serikali zimefikia MWISHO!
 
Hii wanaongelea malipo ya LUKU au Maji ya DAWASCO?! Au malipo ya kodi TRA ?!
 
Bangaladesh mfumo wake wa Fedha ulivamiwa na Wahuni wakahamisha Mzigo karibia wote wa Central Bank yao wakaupeleka kuchezea Kamari kwenye Makampuni ya Kamari huko Lasvegas kabla ya Majasusi Bobezi wa US kuingilia kunusuru

Tukikimbizana kwenda kwenye Technolojia ya Mawasiliano tukimbie kwa tahadhari maana .....
 
Wataalam wetu wa TEHAMA wajue kabisa hii mifumo pia inahitaji ulinzi zaidi ya Vifaru na Mabomu, tuwekeze haswaaa kwenye CYBER SECURITY kwa gharama yoyote ile vinginevyo tutakuja kulia, rejeeeni Maxmalipo na Mwendokasi, Max Malipo na TFF, Rejeeni TANESCO walivyopigwa na wahuni. Lakini pia hivi majuzi huko South Afrika imebainika Kijana msomi wa IT kajiajiri Serikalini kupitia mifumo kama hii na kuingia kwenye Orodha ya malipo ya Mishahara kaja kubainika zaidi ya miaka mitatu. Akina Assange wako duniani kote, hiii kazi nzuri mnayofanya hakikisheni tunailinda kwa nguvu zote. Viva Tanzania
 
Asante sana kwa mchngo wako. Akina Dotto wanatakiwa wajuwe hatari ulizoonesha kwa mifano hai. Majini mamba, nchi kavu simba na mtini nyoka! Fedha zitapigwa tu wasipozingatia haya!
 
Hazijafika mwisho ndg,mbona huku kitaa pesa zinazokusanywa znapigwa tu na viongozi wa serikali za mitaa!.
Zile pesa znazolipwa pale mtu anapokuwa na shughuli nyumbani kwake.
Dotto tuma watu wilaya ya Temeke jamaa wanapiga tu.
Kwenye Automation kutoka analojia kwenda digitali hii Serikali ya Rais Magufuli iko vizuri sana!
Zama za Upigaji wa Pesa za Serikali zimefikia MWISHO!
 
Hazijafika mwisho ndg,mbona huku kitaa pesa zinazokusanywa znapigwa tu na viongozi wa serikali za mitaa!.
Zile pesa znazolipwa pale mtu anapokuwa na shughuli nyumbani kwake.
Dotto tuma watu wilaya ya Temeke jamaa wanapiga tu.
Unabishana na watu ambao hawashirikishi akili zao? kazi yao ni kuimba mapambio ya kupongeza kila siku
 
Na hiyo Ni ile pesa wanayoenda kuchukua wakati watu Bado wapo au pale kagiza Giza kanapo Anza kuingia.

Akiweza kudhibiti Hadi huku chini,chaguzi zote zijazo nitakuwa nawapa kura yangu.

Nashauru wakusanya ushuru wawe watu wa upinzani na wao wawe waangaliaji,wakifanya hivo watafaulu maana upinzani watakusanya kwa weledi ili kuwakomoa CCM ambao walikuwa wanajineemesha kwayo,na hata wao CCM watahakikisha pesa yote inatumwa kunako husika ili isiliwe na watu wa upinzani.
 
Back
Top Bottom