Serikali imewakatia huduma walio kumbwa na mafuriko

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,492
54,890
Baada ya mkuu wa mkoa wa dar es salaam bwana Meck sadick kuwataka wale wanao ishi mabondeni kuhama, Tanesco na dawasco wameamua kuwakatia umeme na maji wale wanao ishi mabondeni ili wahame. na kwamba nyumba zote zitabomolewa.
MY TAKE;
Wanasema wamesha waandalia viwanja watakapo hamia, je kila mtu kashagawiwa kiwanja chake? je hivyo viwanja ndo nyumba? je wapangaji waende wapi, wamesha wapa hela ya kupangisha nyumba sehemu zisizo za bondeni?. Mimi naona hapa serikali haitendi haki. Mia
 
Ndio na mimi ninapoishangaa hii serikali tena kwa mbwembwe inajifanya inajali wananchi wake?
Si bora mtu umuache palepale msimbazi atakimbia maji siku mbili tatu, maisha yanarudi vilevile kuliko kumtekelekeza Wazo maporini kule.
Alafu mtu umejiziki miaka mitano kujenga vyumba vyako viwili, leo mtu anakuambia kiwanja hicho hamia huko, nakupa siku tano.
 
Big up Serkali!!! Imefanya maamuzi magumu!! Huwezi ukajenga popote tu,, hata mahali hatari!!
 
Ishu ya watu kuhamishwa mabondeni ilianza kitambo toka enzi za Makamba ni RC. Maafa yametokea kutokana na baadhi ya Wanasiasa kukwamisha zoezi hilo. Vyovyote iwavyo, lazima watu wa mabondeni wahame kwa usalama wao.
 
Mkuu "MIA"!
Yaani leo nimeangalia gazeti la Mwananchi kuna picha ya maofisa wa serikali na askari wanahakiki na kufanya hilo zoezi la kutimua hao wakazi wa "mabondeni"....
Yaani mwanangu ukiwaangalia hao maafisa ni full wamekaa kidili-dili tu na ulaji, moja kwa moja nimepoteza matumaini na zoezi hilo...
Tutayasikia lakini!!
 
Tusitarajie huruma toka ktk siri kali ya nyinyiemu aka magamba.swala la kuhamisha watu mabondeni si jepesi kama linavyofikiriwa,kama bwana busara hatoalikwa tunatarajia mateso na kunyanyasika zaidi,lakini kwa kuwa hapa ni ktk kisiwa cha amani twendeni kimyakimya.
 
ni uamuzi sahihi.yaani nawafanananisha na vibaka wanaofanya kosa kwa makusudi ili aende jela AKAPATE MLO BURE!
 
Ni uamuzi sahihi ktk muda/wakati usio sahihi.Kuna maandalizi yapi ya msingi yaliyofanywa na serikali ktk maeneo wanayohamishiwa ili yafae watu kuishi hasa huduma za kijamii?Hata kambi za dharula hazija jengwa huko shule zikifunguliwa watakwenda wapi?!
 
Back
Top Bottom