Serikali imeunda Tume maalumu kuchunguza Ufisadi wa Fedha za Uviko kwenye halmashauri zote nchini

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,901
141,838
Waziri mkuu mh Majaliwa amesema kutokana na harufu ya ufisadi mkubwa wa fedha za Uviko kwenye Halmashauri nchini kote, serikali imeunda tume malumu kufanya uchunguzi.

Source: ITV habari

 
CCM, CHAMA CHA MAJIZI.
Hawa jamaa mpaka waondoke madarakani watawaacha watanzania hoi kwa umaskini.
 
Kama madarasa yalikamilika chenji iliyobaki ilipimwa kwenye mzani ili...........tujipimie.
 
Fedha zenyewe za mkopo zimeliwa ,Kisha tume imeundwa kula fedha tena.

Hapa tuliwatahadharisha TAMISEMI kuwa wakurugenzi wa halmshauri wameingilia taratibu za manunuzi huko mashuleni waziri wa TAMISEMI na watu wake wakaweka pamba masikioni.

Endeleeni tu maana mitandao ya kijamii mnaiona kama haina umuhimu wakati humu ndo Kuna usalama wa taifa Bora kwa maoni yangu watu wanatoa taarifa za kulisaidia taifa.
 
daa zimeliwa pesa zetu za mkopo??? hao waliokula wakati tutakuwa tunalipa deni hawatakuwa na maumivu sana ya deni
 
mkopo ulikuwa tri 1.3= bili 1300 ...ila pesa hiyo inasikika zaidi kwenye ujenzi wa madarasa kuliko eneo jingine zilikofanya kazi...takwimu wanazosema ni madarasa elfu 15 ambapo walitoa mil 20 kwa kila darasa..jumla ni bil 300, zanzibar wanasema zilienda zaidi ya bil 200.. ukijumlisha ni sawa na bil 500... hizo bil kama 800 zilizobaki nazo zingetangazwa kazi zilizofanya kama matangazo ya madarasa yalivo ili watu wasibaki na maswali juu ya serikali yao
 
Fedha zenyewe za mkopo zimeliwa ,Kisha tume imeundwa kula fedha tena. Hapa tuliwatahadharisha TAMISEMI kuwa wakurugenzi wa halmshauri wameingilia taratibu za manunuzi huko mashuleni waziri wa TAMISEMI na watu wake wakaweka pamba masikioni...
Waanze na halmashauri ya CHAMWINO ILIPO IKULU YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, location manunuzi😎
 
Huyo jamaa PM aliyemroga kafa.

Maana kila kitu yeye ni kuunda tume ambazo hazinaga mchangao wowote wala hazijulikanagi zinakoishia,
ni bora abaki kimya tu ama kuwashughulikia wale walioshindwa kufikia malengo kwa kuchakachua miradi

hayo matume yake yakipuuzi anapoteza muda
 
Back
Top Bottom