Serikali imeunda kikosi maalumu kwa ajili ya kufuatilia na kuwasaka fisi katika Manispaa ya Shinyanga

Influenza

JF-Expert Member
Jul 1, 2018
1,272
2,000
KUTOKANA na kukithiri kwa matukio ya Fisi kushambulia wakazi wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga hususan watoto wadogo, serikali imeunda kikosi maalumu kwa ajili ya kufuatilia na kuwasaka fisi hao ambao katika siku za hivi karibuni wamekuwa wakiwasumbua wakazi wa manispaa hiyo.

Kwa takribani miezi sita sasa, kumekuwepo na matukio ya Fisi kuonekana katika maeneo mbalimbali ya mji wa Shinyanga ambapo huwashambulia watu na kuwasababishia majeraha huku ikiripotiwa watoto wasiopungua wanne kufariki baada ya kushambuliwa na fisi hao.

Tukio la hivi karibuni lilitokea katika kitongoji cha Relini mtaa wa Nhelegani Manispaa ya Shinyanga, mtoto aliyetambulika kwa jina la Kulwa Machiya (06) alikufa baada ya kujeruhiwa vibaya na Fisi aliyewavamia na kumshambulia wakati wakitokea machungani pamoja na watoto wenzake.

Kutokana na hali hiyo, Halmashauri imelazimika kuunda kikosi maalumu ambacho kitaendesha operesheni ya kuwasaka Fisi hao ili kuwaua na kuepusha wananchi kuendelea kuishi wa wasiwasi wa kushambuliwa.

Kiongozi wa kikosi hicho, Ezra Manjerenga amesema, operesheni hiyo inaendeshwa kwa ushirikiano wa pamoja kati ya Wataalamu wa Maliasili Kitengo cha Wanyamapori, Jeshi la Polisi, viongozi wa vijiji husika wakiwemo walinzi wa Jadi (Sungusungu).

Kwa mujibu wa maelezo ya kiongozi huyo, tayari operesheni hiyo imeanza leo saa 12 alfajiri kwa kufanya msako katika vichaka na mapori yote yaliyopo katika kijiji cha Nhelegani kwenye vitongoji vya Itogwanh’olo na Ibanza.

Hata hivyo kiongozi huyo ametoa wito kwa wakazi wote wa maeneo ambako Opresheni inafanyika kutoa ushirikiano wao kwa kuelekeza maeneo ambayo fisi hao wamekuwa wakionekana mara kwa mara ili kuweza kukabiliana nao.
 

The Elephant

JF-Expert Member
Dec 18, 2014
4,200
2,000
Inawezekana wakiwa kazini wanaonekana FISI ila wakati hawako kwenye shughuli maalum wanaoneka wajumbe std 7!!!!
 

Zero Hours

JF-Expert Member
Apr 1, 2011
12,334
2,000
Ao ni fisi watu...mbona sisi tumeishi na fisi kama mbwa tu. Shuda yao wanaharibu mazao kama tikiti au mifugo...ila watu????
 

Times9

JF-Expert Member
Mar 1, 2017
1,251
2,000
Serikali ikae ikijua inaenda kupambana na watu na sio fisi wa kweli....
 

GKado

JF-Expert Member
Oct 7, 2017
409
1,000
Maeneo ya Nghungumalwa walifanya operation kipindi Cha miaka kazaa iliyopita aisee walikamata fisi wengi kwa siku walikuwa wanakamata zaidi ya fisi 8.​

Note operation ilifanikiwa kwa kutumia wataalam maalumu siyo kuamuka kizembe kwenda kutafuta fisi hawapati hata mmoja.​
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom