Serikali imetoa onyo kwa wafanyabiashara wa mafuta watakaopandisha bei ya bidhaa hiyo kinyume na bei elekezi

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,495
9,275
Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe Geofrey Mwambe amewaonya wafanyabiashara wa mafuta watakao pandisha bei ya bidhaa hiyo kinyume na bei elekeze kuwa watachukuliwa hatua kali za kisheria ikiwemo kufutiwa leseni zao za biashara.

Waziri Mwambe ametoa onyo hilo leo jijini Dodoma wakati akizungumza na wandishi wa habari juu ya mfumuko wa bei ya mafuta ambao umekua mkubwa kwa siku za hivi karibuni.

Amesema kuna uhaba wa mafuta nchini na kubainisha kuwa changamoto hiyo itakoma baada ya kuwasili kwa meli mbili ndani ya kipindi cha mwezi mmoja ambazo zimeshusha mafuta takribani Tani 48,000 na uhitaji ukiwa ni mafuta Tani 30,000 kwa mwezi.

"Kwa sasa changamoto ya bei haitakuwepo na tayari tumeshawapunguzia waagizaji baadhi ya gharama za kushusha mafuta pale bandarini lakini pia niwahakikishie watanzania uhaba wa mafuta hauwezi kuendelea kwani Februari 17 kuna meli ya mafuta itawasili na nimeagiza isichukue muda mrefu kushusha pale bandarini hadi Februari 20 meli hiyo iwe imeshashusha mafuta" amesema.

Amewataka watanzania hususa ni vijana kuchukulia changamoto hiyo kuwa fursa kutokana na kuwa na ardhi inayokubali mazao ya mafuta amesema ni wajibu kwa wakulima kulima kwa wingi mazao hayo.

"Nchi yetu ina ardhi ambayo inakubali kilimo cha mazao ya mafuta, wajiunge kwenye vikundi vidogo vidogo wapatiwe mikopo ile ya kwenye Halmashauri na wajikite kwenye kilimo hiko," amesema Waziri Mwambe.

Aidha waziri Mwambe ametoa maelekezo kwa Tume ya Ushindani kuhakikisha wanafuafitilia mwenendo wa mafuta nchini huku akiwataka kumuandalia ripoti ya hali ya bidhaa hiyo hapa nchini nchini.

Amewataka Wakuu wa Mikoa ambao mikoa yao ina ardhi inayokubali mazao ya mafuta kama michikichi, alizeti na karanga na mazao mengine ya mafuta kuhamasisha Wananchi wao kujikita kwenye kilimo hicho ili kuweza kujikwamua kiuchumi wao wenyewe lakini pia kuzalisha mbegu ambazo zitatumika na viwanda vya ndani na kupunguza uagizwaji wa mafuta nje ya nchi.
 
Kila siku wanatoa matamko lakini utekelezaji wake ni wa kusuasua! Tulianza na sukari, ikaja cement, na sasa mafuta ya kula!!

Halafu mwisho wa siku tunaambiwa hakuna mfumuko wa bei! Bidhaa zinapanda bei, wananchi wakiwemo watumishi wa umma wanalazimishwa kuishi maisha yale yale tangu 2015!

Hakuna kupandishwa madaraja, wala kuongezewa mishahara!

Magufuli, maliza muda wako upumzike!! Wafanyakazi tulio wengi, tumekuchoka! Umejenga na unaendelea kujenga miundombinu ya kila aina! Katika hilo, utakumbukwa sana. Ila kwenye ishu ya haki za wafanyakazi, utabakia katika historia kama Rais mkatili kwa wafanyakazi kuliko watangulizi wako wote.
 
Kila siku wanatoa matamko lakini utekelezaji wake ni wa kusuasua! Tulianza na sukari, ikaja cement, na sasa mafuta ya kula!!....
Nchi yetu bado changa kama unamsifia kwa kujenga miundombinu sawa vizuri,ila kama kipato chako cha kawaida huwezi kujenga ,kusomesha watoto na ukataka kuishi maisha yaleyale ambayo uliishi kabla hujaanza ujenzi na husomeshi
 
Hayo mazao ya kukamua mafuta yana stawi baada ya wiki ngap? Maana hadi Feb. unasema mafuta yatakuwepo alafu unasema vijana waitumie fursa wakati wajua ni ya muda mfupi?

Kwanini wewe na mawaziri wakubwa mlio na mitaji msilime mashamba makubwa ya mazao ya kukamua mafuta.
 
Back
Top Bottom