Status
Not open for further replies.

kurlzawa

JF-Expert Member
Jan 23, 2018
16,703
20,606
Habari za mchana huu wakuu,

Moja kati ya habari zinazogagaa mitandao mbalimbali ni suala la aiyekuwa mbunge wa zamani Tundu Lissu kuonekana katika majina ya watu wanaotakiwa kulipwa stahiki zake.

Je, Job Ndugai atajisikiaje maana alikuwa anaongoza hadharani kumkashifu Tundu Lissu ilihali alikuwa anajua kabisa anaumwa yuko nje kimatibabu.

Je, wale watukanaji wa Lumumba mtajisikiaje?

NAKUPONGEZA MAMA KWA KUSIMAMIA HAKIA. HAKI HUINUA TAIFA.

=====
20210625_063410.jpg

#SIASA: Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la #SingidaMashariki, Tundu Antipas Lissu ameorodheshwa kwenye Tangazo la Wizara ya Fedha na Mipango kama moja ya watu wanaotakiwa kulipwa madai yao ya mishahara baada ya kutokulipwa na Serikali.

Katika Tangazo hilo lilitolewa leo na Wizara hiyo limeonesha majina yaliyohakikiwa ili kulipwa na jina la Mbunge huyo mstaafu likiwepo.

Baada ya kupata nafuu, Lissu aliwahi kulalamika malipo yake ya mishahara kusimamishwa akiwa mgonjwa na hivyo alihitaji kulipwa madai yake.

=====

UPDATES:

======
Hii taarifa imekanushwa. Zaidi soma;

1). Tundu Lissu Akanusha kuorodheshwa kwenye malimbikizo yake
JamiiForums2015348585.jpg
 
Katika siku 100 za uongozi wa Rais wa JMT Samia Suluh Hassan, tumeshuhudia mageuzi makuu ya aina ya siasa zinazofuata sheria na kuheshimu utu wa mtu, tofauti kabisa na utawala wa kimabavu na roho mbaya ya mtangulizi wake.

Leo hii Tundu Lissu ametajwa kuwa mmoja wa wanaostahili kulipwa madai yake kama inavyojielezwa kwenye link hapo chini

Serikali imetoa majina ya watumishi wa umma wanaostahili kulipwa madai ya malimbikizo yao baada ya uhakiki. Ofisi ya Spika ina majina 394 likiwemo jina la Mh. @TunduALissu https://t.co/qS2U9QrNIV

Hakika nuru inaonekana hatimaye.
 
Taarifa bila attachment ya hayo majina ni sawa tu na kudemka! Mbaya zaidi unademka mchana kweupe!

Na hili jua kali basi ndo balaaa tupuuu. Jombaa hebu ipe nyama ya attachment ya hayo majina ndo taarifa itakuwa kamili.
 
Sijaelewa, halafu mhe radio huyu wa sasa si ndio huyu huyu aliyemfukuza? Ni mambo mawili tu kwake, either ajiuzuru nafasi aliyonayo au afanye declaration kwamba alikua anapokea maelekezo, haikua kwa UTASHI wake, Watanzania tutamsamehe maana maneno yake ya kumfukuza Lissu ubunge na hata kumnyima haki zake bado yapo youtube
 
Sijaelewa, halafu mhe radio huyu wa sasa si ndio huyu huyu aliyemfukuza? Ni mambo mawili tu kwake, either ajiuzuru nafasi aliyonayo au afanye declaration kwamba alikua anapokea maelekezo, haikua kwa UTASHI wake, Watanzania tutamsamehe maana maneno yake ya kumfukuza Lissu ubunge na hata kumnyima haki zake bado yapo youtube
Sasa hela mmepewa kwanini hamfungi mdomo? hivi mmezaliwa mnaongea?
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom