Serikali imesitisha uhamisho kwa watumishi wa umma 2017 mpaka itakapoamuliwa vinginevyo

Mwaka 2016 umeisha na sintofahamu,na huu mwaka naona unaanza bila kueleweka,namwonea mtumishi wa umma huruma hasahasa mwalimu.
 
Connect dots: mapato ya mwezi hayatangazwi tena, wanafunzi kukosa mikopo, field kwa wanafunzi mwaka wa kwanza kuzuiwa na sasa uhamisho......
 
25081c3aea9540a7aa5d68104a2a4b19.jpg
Nimelipenda jina la DED, mahera........! Masalu, masanja, mabula, maduhu........ Still researching
 
Kuna kila sababu ya kuviomba vyama vya wafanyakazi vitoe tamko ili serikali ipewe shinikizo vingenevyo huu mwaka unaweza ukapita pasipo kuruhusu uhamisho kama mwaka jana,, maana Hawa viongozi wamepoteza kabisa utu wanaangalia maslahi yao tu. Kiukweli inauma sana kuona watu wanaishi mbali na familia zao pasipokuwa na sababu za msingi halafu wanajifanya wapo kutetea maslahi ya wanyonnge,, tunaomba mamlaka zinazohusika zituweke wazi kama uhamisho upo ama haupo ili tujue nini cha kufanya maana kuendelea kuishi mbali na familia zetu ni ngumu au mnataka kutuvunjia ndoa zetu? Kuweni na utu kidogo na tangulizeni maslahi ya watu mnaotuongoza hatukuwachagua ili mje mtuongoze kwa kutumia utashi wenu ulio na chuki na dharau bali kwa kutumia kanuni, sharia na taratibu zilizopo hayo mnayotufanyia kama ninyi mngalifanyiwa hivo mngeridhika? Tambueni hivyo yveo ni vya kupita tu hakuna sababu ya msingi ya kuzuia uhamisho na kama ipo tunaomba mtuambie, inauma sana kwa yeyote mwenye mawasiliano na mbunge yeyote maana ndo watetezi wetu pia maana vyama vya wafanyakazi vimeamua kutusaliti naomba tupate fursa ya kuwaomba wabunge ambao wapo tayari kututetea waipeleke hii haja bungeni ili waziri husika atoe ufafanuzi kuhusu suala la uhamisho,,
 
Back
Top Bottom