Serikali imesimamisha usajili wa magazeti mapya

Sheikh

Member
Aug 22, 2008
13
0
Wizara ya Habari kupitia Idara yake ya Maelezo imesimamisha Usajili wa magazeti kwa sababu ambazo mpaka sasa hivi hatuzijui.

Tofauti na Kenya ambako unaweza kuanzisha gazeti halafu baadaye kuliandikisha kibiashara hapa Tanzania huwezi kuanzisha gazeti bila kusajiliwa na Idara ya Maelezo.

Hii ni mojawapo ya sheria ambazo haifurahiwi na wawekezaji katika sekta ya habari -wa ndani na wa nje.

Huu ni msimu wa watu wengi wenye uchu na uroho wa ukubwa nchini kuanzisha magazeti uchwara ambayo muda wake wa kuishi ni kati ya kabla kidogo tu ya uchaguzi mkuu na mwisho wa uchaguzi mkuu.
 
Tuwekee chanzo cha habari. Hao jamaa ni wa ' Idara Maelezo' hivyo hawawezi kufanya kitu bila kutoa maelezo!
 
magazeti yamekuwa tishio kwa serikali na hii ndio njia pekee ya kuyanyamzisha!!!! kazi ipo kama hii habari ni kweli
 
Wizara ya Habari kupitia Idara yake ya Maelezo imesimamisha Usajili wa magazeti kwa sababu ambazo mpaka sasa hivi hatuzijui.

Tofauti na Kenya ambako unaweza kuanzisha gazeti halafu baadaye kuliandikisha kibiashara hapa Tanzania huwezi kuanzisha gazeti bila kusajiliwa na Idara ya Maelezo.

Hii ni mojawapo ya sheria ambazo haifurahiwi na wawekezaji katika sekta ya habari -wa ndani na wa nje.

Huu ni msimu wa watu wengi wenye uchu na uroho wa ukubwa nchini kuanzisha magazeti uchwara ambayo muda wake wa kuishi ni kati ya kabla kidogo tu ya uchaguzi mkuu na mwisho wa uchaguzi mkuu.
 
Ndani ya kipindi cha mwaka mmoja tumeshuhudia wenye vijisenti wakianzisha na kutumia Magazeti kama silaha ya kuchafua na kujisafisha....hivyo sishangai uamuzi huu.

Baadhi ya magazeti mengi kwa sasa hayafuati maadili ya uandishi bali matakwa ya mmiliki.
 
Nadhani hii ni kuvitishia vyombo nya habari esp. Mazeti ili kuvinyima nguvu. Uchaguzi mkuu umekaribia kwa hiyo serikali inaokuwa mambo ya Ufisadi yatazidi kuwekwa hadhari.
 
Sheria inawaruhusu kuzuia kusajiliwa kwa magazeti?

Hii ni woga wa Kitoto, kwanza wamefungia MwanaHALISI, sasa wako kwa Mengi wanazuia usajiri kisha waanze kuyafungia magazeti fulani. hizi ni jana za mafisadi tu.
 
magazeti yamekuwa tishio kwa serikali na hii ndio njia pekee ya kuyanyamzisha!!!! kazi ipo kama hii habari ni kweli

Siku hizi kuna Citizen Journalism. Kinachoshindikana kupitia Mainstream Journalism tunakipata kupitia Citizen Journalism kama jamiiforums.com nk. Haiwezekani kumwekea mtu mwenye akili timamu sheria za kunyima habari. Hata wafunge magazeti yote, still Watz watapata njia ya kuwasiliana hata kama ni oral.
 
Ni katika harakati za kum-bana Rostam and Lowassa!

Kama hilo ndio lengo lao, naona watakuwa wamechelewa. RA na EL wana vijigazeti vyao tayari na vinaendelea kuwasafisha na kuandika habari za kizushi kila kukicha. Si ajabu hata ule utaratibu wa kununua wahariri na waandishi wa habari ukarudi tena pindi jamaa wakiona kuna umuhimu wa kuwatumia kwa ajili ya maslahi yao.
 
Wizara ya Habari kupitia Idara yake ya Maelezo imesimamisha Usajili wa magazeti kwa sababu ambazo mpaka sasa hivi hatuzijui.

Tofauti na Kenya ambako unaweza kuanzisha gazeti halafu baadaye kuliandikisha kibiashara hapa Tanzania huwezi kuanzisha gazeti bila kusajiliwa na Idara ya Maelezo.

Hii ni mojawapo ya sheria ambazo haifurahiwi na wawekezaji katika sekta ya habari -wa ndani na wa nje.

Huu ni msimu wa watu wengi wenye uchu na uroho wa ukubwa nchini kuanzisha magazeti uchwara ambayo muda wake wa kuishi ni kati ya kabla kidogo tu ya uchaguzi mkuu na mwisho wa uchaguzi mkuu.

Kinachodaiwa ni kuwa CCM imeamrisha Maelezo kusimamisha usajili wa magazeti mapya ili kuzuia kuandikishwa kwa magazeti ya wapinzani wakiwemo mafisadi ambao sasa hivi wanasubuliwa na serikali ya chama hicho!
 
Back
Top Bottom