LWENYI
JF-Expert Member
- Jul 4, 2013
- 1,784
- 2,097
Salaam wana jukwaa wenzangu
Moja kwa moja niende kwenye maada
Sote tunajua pamoja na matamko na ushauri mbalimbali wa wanasiasa pamoja na wasomi wengine kuhusu wanataaluna hasa vijana kujiajiri, hakuna wa kupinga kwamba wengi wa watu hao wamefunzwa kuajiriwa, na serikali ndiye muajiri mkuu hapa nchini
Kitendo cha serikali yetu kusitisha ajira serikalini na kufukuza wasiokidhi vigezo katika taasisi zake ni wazi kimeleta madhara makubwa kwenye soko la ajira nchini
Hali ilipofikia hivi sasa kijana mwenye shahada na ufaulu mzuri kabisa sasa hv anaombwa kutoa ujuzi wake katika taasisi za binafsi kwa mpaka chini ya kima cha chini cha mshahara na wanachangamkia kwa wingi ajira za namna hiyo
Je, huu si udhalilishaji wa taaluma na thamani za wataalamu wetu? Je huku si kushusha morali ya watanzania wengi kuwekeza katika elimu za watoto na wajukuu zao? Je serikali imeridhika na hali hii kwa wasomi wa nchi hii?
Ifahamike kuwa Sitaki kuifundisha kazi serikali lakini inauma kuona taaluma hazina tena thamani na hata ukiajiriwa vijana wengi wanaishia kutumikia vitengo na fani ambazo hawakuzisomea hivyo kupunguz ufanusi na uweledi wao. Kwa leo ni hayo tu
Wenu mwananchi wa kawaida.