Babu wa Kambo
JF-Expert Member
- May 2, 2016
- 559
- 808
Kwa muda mrefu sasa toka kuingia kwa Utawala mpya, tumeshuhudia Mazingaombwe na Vituko vingi vinavyofanywa na Serikali "sikivu" ya CCM kuhakikisha Upinzani unadhibitiwa, hii ni aibu kubwa
Lakini je tunachojiuliza, kama lengo lao ni kuhakikisha Chama kimoja tu na Serikali yake ndivyo vinaendelea kusikika Nchini, sasa ni kwa nini Serikali hii isiamue kupeleka hoja Bungeni ili kufanya Marekebisho ya Katiba (Constitutional Amendments) wakafanya mabadiliko na kuturudisha katika Mfumo wa Chama kimoja wanaoutaka tofauti na sasa wanavyokiuka maelekezo ya Katiba?
Japo hili haliwezekani, kwa nini msifanye tu marekebisho ya Katiba tukajua moja kwa moja mmeamua kuturudisha "Monopartism"? Humuoni kama mnapoteza nguvu zenu na Rasilimali zetu katika kufanya hizi Sarakasi zenu?
Ushauri wangu; Dunia imebadilika, mawazo yenu hayawezi kufanya kazi katika ulimwengu wa leo, "Waacheni watu watoe ya moyoni, wapeni uhuru wao, ninyi ni watumishi tu". Ubabe hautasaidia kitu zaidi ya kuchochea chuki
Kama mnataka hayo, badilisheni Katiba kama iliyopo haikidhi matakwa yenu, ndiyo utaratibu sahihi na si kutumia mabavu bila msingi, msituvunjie Katiba yetu, taratibu mnazoziingiza haziko katika "Principles of Democracy" mlizosaini mwaka 1992, labda kama hamsomi Katiba ya Nchi