Serikali imeshindwa kuwadhibiti waganga wa kienyeji na wapiga ramli chonganishi?

Coloneli

Member
Aug 24, 2020
35
151
Ukikaa chini na kufikiri sana, unashanga kwa namna ambavyo tumekuwa ni taifa la ovyo, linaloruhusu mambo ya ovyo kufanywa ovyoovyo na watu wa ovyo.

Tunalo jeshi la Polisi, tunao Usalama wa Taifa, tunao watu wa makosa ya mtandao, tunao TCRA, lakini ETI hawaoni ujinga huu, ni mambo ya ovyo sana.

Kuna watu wanaojiita waganga wa kienyeji, wapiga ramli. Wanabandika matangazo yao bila uoga wakitamba kwamba eti wanaweza kumrudisha kazini mtu aliyefukuzwa, wanaweza kumfanya ashinde kesi mahakamani.

Hivi mtu aliyefukuzwa kazi kwa makosa ya kikanuni, ambaye taratibu zote zimefuatwa na kuzingatiwa, huyu mganga anamrudishaje? Katika kufanya hivi, hakuna jinai hapa?

Huyu tapeli, anamshindishaje mtu kesi ambayo ina ushahidi usio shaka kwamba mlalamikiwa alitenda kosa analotuhumiwa nalo? Je hapa napo hakuna jinai?

Kwa nini mamlaka zinazohusika hazichukui hatua kwa watu wa namna hii, ambao wanaweka hadi namba zao za simu ili kurahisisha upatikanaji wao?

Katika kipindi ambacho hali ni ngumu, ajira hazipatikani na mtaani kila mmoja analalamika, watu wanatafuta njia rahisi za kutoka. Kuna wenzetu ambao wamekataa kufikiri vizuri, wanaamini unaweza kutoka kimaisha kama utajiunga na freemason. Freemason yao wao, siyo ile ya mzee Chande (RIP). Wao yao ni ile ya kutoa kafara.

Sasa kuna mabango mengi sana huko mitaani, yakitoa nambari za simu za kuwasaidia watu kujiunga na ufreemason. Polisi wanaona, Usalama wanaona, viongozi wa kisiasa wanaona na hata watu wa kawaida kwenye jamii wanaona, lakini kila mmoja anadhani siyo tatizo lake.

Kwanza hawa wanaotoa haya matangazo ni matapeli. Wangeweza kushtakiwa tu kwa utapeli wao, lakini mbaya zaidi, utapeli huu unaambatana na vitendo vya kihalifu ikiwemo mauaji ya kuusaka utajiri. Hawa ndiyo wanaowaweka hatarini watu wenye ulemavu wa ngozi.

Njoo katika mitandao, Cyber Crime na TCRA wako bize kuangalia katika page za wasanii, wanasiasa na wanaharakati nini wanaandika, lakini wanajifanya hawaoni jinsi majina ya watu maarufu yanavyotumika kutapeli watu.

Kuna Taasisi ya mikopo huko Facebook inayomilikiwa na Mo Dewji, inatoa eti mikopo ya chapchap. Picha ya tajiri huyo imewekwa kwenye page, lakini mwenyewe anakataa hatoi mikopo hiyo.

Wale matapeli wametoa hadi namba za simu. Siyo Mo tu, majina mengi sana ya watu maarufu yanatumika na wenyewe wanakataa, lakini hatusikii vyombo vyetu vikituambia juu ya kukamatwa kwa watu hao kama wanavyotupa taarifa za kina Giggy Money. Vituo vya daladala, kwenye nguzo na kila penye nafasi, kumejaa matangazo ya waganga wa kienyeji wenye uwezo wa ajabu, lakini hakuna anayejali, bila kujua kuwa tunao wenzetu ambao walipofikia, wanahitaji waganga hao ambao huwatoza fedha nyingi lakini tatizo lao haliishi.

Unajisifu umepunguza ujambazi wakati watu wanakabwa kwa ustaili nyingine? Lakini ukisikika unasema tuna IGP wa ovyo, tuna Mkurugenzi Tiss wa ovyo kwa kuruhusu haya mambo ya ovyo, utasakwa na ukinaswa utafanyiwa mambo ya ovyo.

A�ɴ`��
 
Hivi utamshtaki vipi mganga kwa kufanya manyanga kwa mtu aliyevunja kanuni za kazi na kufukuzwa kisha kurudishwa kazini

Utaiambia nini mahakama ili iprove jinsi mganga alivyofanya kufanikisha huyo mtu kurudi kazini ili imtie hatiani mganga

Kuhusu utapeli hiyo inawahusu watapeliwa na watapeli wao
Kama umetapeliwa nenda kwenye vituo vya sheria katoe malalamiko ikionekana umeonewa haki itatendeka

Lakini huwezi kumkamata mganga kwamba yeye ni tapeli kukiwa hakuna aliyetapeliwa na kama wako waliotapeliwa basi kesi zitakuwepo kwenye vituo vya polisi na mahakamani huko lakini ukiona kimya ujue watu wanaridhika na huduma wanazopata huko
 
Maandishi yako ya hovyo; mwandiko wa hovyo; hisia za hovyo; kila kitu umekisema kwa namna ya hovyo. Umemwiga kauli yule Mr Mzungu wako wa hovyo
 
Kwa taarifa yako watu wanao ongoza kwenda kwa waganga hapa Tanzania ni polisi kutaka kupangiwa trafik, kupandishwa vyeo na kupangiwa mikoa mizurii. Wakifuatiliwa na wanawake walioolewa kutaka kuwafunga Waume zao wasichukue michepuko.
Ukiona trafik mzee mzee kakupiga tochi ujue kiunoni ana bonge ya hirizi.
 
Ukikaa chini na kufikiri sana, unashanga kwa namna ambavyo tumekuwa ni taifa la ovyo, linaloruhusu mambo ya ovyo kufanywa ovyoovyo na watu wa ovyo.

Tunalo jeshi la Polisi, tunao Usalama wa Taifa, tunao watu wa makosa ya mtandao, tunao TCRA, lakini ETI hawaoni ujinga huu, ni mambo ya ovyo sana.

Kuna watu wanaojiita waganga wa kienyeji, wapiga ramli. Wanabandika matangazo yao bila uoga wakitamba kwamba eti wanaweza kumrudisha kazini mtu aliyefukuzwa, wanaweza kumfanya ashinde kesi mahakamani.

Hivi mtu aliyefukuzwa kazi kwa makosa ya kikanuni, ambaye taratibu zote zimefuatwa na kuzingatiwa, huyu mganga anamrudishaje? Katika kufanya hivi, hakuna jinai hapa?

Huyu tapeli, anamshindishaje mtu kesi ambayo ina ushahidi usio shaka kwamba mlalamikiwa alitenda kosa analotuhumiwa nalo? Je hapa napo hakuna jinai?

Kwa nini mamlaka zinazohusika hazichukui hatua kwa watu wa namna hii, ambao wanaweka hadi namba zao za simu ili kurahisisha upatikanaji wao?

Katika kipindi ambacho hali ni ngumu, ajira hazipatikani na mtaani kila mmoja analalamika, watu wanatafuta njia rahisi za kutoka. Kuna wenzetu ambao wamekataa kufikiri vizuri, wanaamini unaweza kutoka kimaisha kama utajiunga na freemason. Freemason yao wao, siyo ile ya mzee Chande (RIP). Wao yao ni ile ya kutoa kafara.

Sasa kuna mabango mengi sana huko mitaani, yakitoa nambari za simu za kuwasaidia watu kujiunga na ufreemason. Polisi wanaona, Usalama wanaona, viongozi wa kisiasa wanaona na hata watu wa kawaida kwenye jamii wanaona, lakini kila mmoja anadhani siyo tatizo lake.

Kwanza hawa wanaotoa haya matangazo ni matapeli. Wangeweza kushtakiwa tu kwa utapeli wao, lakini mbaya zaidi, utapeli huu unaambatana na vitendo vya kihalifu ikiwemo mauaji ya kuusaka utajiri. Hawa ndiyo wanaowaweka hatarini watu wenye ulemavu wa ngozi.

Njoo katika mitandao, Cyber Crime na TCRA wako bize kuangalia katika page za wasanii, wanasiasa na wanaharakati nini wanaandika, lakini wanajifanya hawaoni jinsi majina ya watu maarufu yanavyotumika kutapeli watu.

Kuna Taasisi ya mikopo huko Facebook inayomilikiwa na Mo Dewji, inatoa eti mikopo ya chapchap. Picha ya tajiri huyo imewekwa kwenye page, lakini mwenyewe anakataa hatoi mikopo hiyo.

Wale matapeli wametoa hadi namba za simu. Siyo Mo tu, majina mengi sana ya watu maarufu yanatumika na wenyewe wanakataa, lakini hatusikii vyombo vyetu vikituambia juu ya kukamatwa kwa watu hao kama wanavyotupa taarifa za kina Giggy Money. Vituo vya daladala, kwenye nguzo na kila penye nafasi, kumejaa matangazo ya waganga wa kienyeji wenye uwezo wa ajabu, lakini hakuna anayejali, bila kujua kuwa tunao wenzetu ambao walipofikia, wanahitaji waganga hao ambao huwatoza fedha nyingi lakini tatizo lao haliishi.

Unajisifu umepunguza ujambazi wakati watu wanakabwa kwa ustaili nyingine? Lakini ukisikika unasema tuna IGP wa ovyo, tuna Mkurugenzi Tiss wa ovyo kwa kuruhusu haya mambo ya ovyo, utasakwa na ukinaswa utafanyiwa mambo ya ovyo.

A�ɴ`��
Wanajua jinsi ya kucheza na akili za watu ni wasanii na hata hao wa Serikali na wasomi wanatepeliwa vizuri tu na hao Jamaa.
 
Kwa taarifa yako watu wanao ongoza kwenda kwa waganga hapa Tanzania ni polisi kutaka kupangiwa trafik, kupandishwa vyeo na kupangiwa mikoa mizurii. Wakifuatiliwa na wanawake walioolewa kutaka kuwafunga Waume zao wasichukue michepuko.
Ukiona trafik mzee mzee kakupiga tochi ujue kiunoni ana bonge ya hirizi.
....Tujiulize: MTU kafukuzwa Kazi kwa Kosa LA Kuiba Hela kutoka Vifungu vya Ofisi yake.
Amefukuzwa kwa Ushahidi Kamili.
Halafu anaaminishwa na Mganga huyo kwamba anaweza kumrudisha kazini.
Kuna hasara mbili hapo:

Moja, Mhusika kuliwa hela yake na mganga kwa kuaminishwa kuwa atarudishwa kazini..

Mbili, Kwa Taifa kula Hasara kwa Mwizi wake huyo kurudishwa Kazini, kwa mazingaombwe yoyote, ili akaibe tena!!!

Haya, unagombana na Mkeo/mumeo ama mpenzi wako....anarudi kwao Kigoma.
Mganga ana advertise kuwa anaweza kumrejesha Aliyekukimbia chini ya Massa Mawili tu...na mjinga wewe unakubali, na kuliwa visenti vyako vya ngama ... wakati unajua fika kwamba Dar hadi Kigoma ni Safari ya Masaa 24!!
Tumerogwa??!!
 
Unamkumbuka Mapunda?
 
Nadhani kutapeliwa kunatokana na unafiki wetu kuhusu tiba. Matapeli wanapitia humo humo...
 
7BBE7FCE-780A-427B-AA7B-797EDA6792F9.jpeg
 
Ukiwafungia hao waganga, pia manabii, wachungaji, maaskofu wanaoombea watu na kuchukua sadaka nao uwafungie.

Maana wote utapeli wao ni ule ule tu.

Ama uwaachie wote kwa minajili ya uhuru wa kuamini, ama uwafungie wote kwa utapeli.
 
Waganga wa kienyeji wako kundi moja na manabii na wanasiasa. Wote Ni wachumia tumbo na waongo. Tena Bora hata waganga maana wanaweza kukusaidia kumshusha adui yako shipa
 
Back
Top Bottom