Serikali imeshindwa kuajiri vijana wenye vyeti halali, inarudisha kazini wenye vyeti feki

The lost

JF-Expert Member
Jul 3, 2017
2,695
8,209
Wakati mwingine mpaka unahisi kuna laana juu ya nchi yetu. Vijana wasio na mbele wala nyuma but wakiwa na taaluma zao mmegoma kuwapa ajira lakini cha kushangaza mnawarudisha wazee 4000 walioshutumiwa na kuondolewa kazini kwa udanganyifu wa taaluma zao.

Watu hao kama walionewa waseme walienda lini mahakamani kushitaki na mahakama iliamuru wapi kwamba warudishwe makazini.

Inauma na kukatisha tamaa sana na ofcourse vijana wetu wapo disapointed sana na serikali yao. Kwanini watoto wa wafugaji, wakulima na masikini wa taifa hili mnawanyanyasa lakini?

Anyway, kijana pambana upate riziki yako na uwapambanie ndugu zako kwa namna yoyote iwe halali ama kwa shari. Go my son.
 
Kauli ya Majaliwa imefanya jinai isiwe kosa tena, sasa ni halali, kama taifa naona tumeshapoteza muelekeo, hao kwa kuwatendea haki wangetakiwa kulipwa stahiki zao then wawapishe vijana wenye vyeti halali, lakini sio kuwarudisha kazini wakazibe nafasi za wenye haki.
 
ACHA WIVU DOGO. KUNA JAMAA ALIFUKUZWA KAZI WAKATI KILA MWAKA ALIKUWA ANAIBUKA MFANYAKAZI BORA.

KUNA DOGO MMOJA ALIKUWA DEREVA MAKINI SANA HAJAWAHI HATA KUPATA AJALI, MSAFI, MSTAARABU, ANAWAHI KAZINI, ANATUNZA SIRI ZA OFISI, ANATUNZA GARI LILILONUNULIWA NA KODI ZA WANANCHI ILA ALITUMBULIWA. LEO HII ANAENDESHA BASI KWA RAHA ZAKE. SASA JIULIZE KAMA CHETI FEKI MBONA HAANGUSHI ABIRIA?
 
Wakati mwingine mpaka unahisi kuna laana juu ya nchi yetu. Vijana wasio na mbele wala nyuma but wakiwa na taaluma zao mmegoma kuwapa ajira lakini cha kushangaza mnawarudisha wazee 4000 walioshutumiwa na kuondolewa kazini kwa udanganyifu wa taaluma zao. Watu hao kama walionewa waseme walienda lini mahakamani kushitaki na mahakama iliamuru wapi kwamba warudishwe makazini. Inauma na kukatisha tamaa sana na ofcourse vijana wetu wapo disapointed sana na serikali yao. Kwanini watoto wa wafugaji, wakulima na masikini wa taifa hili mnawanyanyasa lakini?
Anyway, kijana pambana upate riziki yako na uwapambanie ndugu zako kwa namna yoyote iwe halali ama kwa shari. Go my son.
# You've carried a pen for long time, Now it's a time to carry a gun. Go

ukisikia roho mbaya ndiyo izi sasa
 
Tuwape nafasi kuona UVCCM walioko vyuoni watatoa tamko gani kwa vijana wezao walioko mtaani, utasikia UVCCM UDSM, UVCCM UDOM.
Hawa UVCCM sijuih wana kazi gani vyuoni .
 
Sijaelewa, serikali ilithibitisha kuwa hawana sifa stahiki, wakawaondoa! Wakakubali kuwa hawana sifa stahiki na wamefanya udanganyifu.

Kwahiyo sasa hivi serikali inasema udanganyifu na kutokuwa na sifa stahiki sio kosa?

Mwenye cheti halali anaweza kupata UZOEFU akipewa nafasi kama hao wanaidhani walikuwa ajirani kwa sababu ya uzoefu wao. Ila kama una UZOEFU tu, kupata cheti itategemea na hali yako.

UELEWA/UJUZI - CHETI - MAFUNZO KAZINI - UZOEFU
 
Ukisoma huu uzi ndio utajua wabongo walivyo na roho mbaya.

Mimi nashauri wenye vyeti feki warudishwe au walipwe stahiki zao pia vijana wasio na ajira nao wapewe kazi.

Uhaba wa watumishi serikalini ni mkubwa mno. Kuna shule ina wanafunzi 500 halafu walimu 5. Ukimtoa mwalimu mkuu wanabaki 4.
 
ni sisi watanzania tuliolalamika sana enzi za mwendazake juu ya hili suala....
 
ACHA WIVU DOGO. KUNA JAMAA ALIFUKUZWA KAZI WAKATI KILA MWAKA ALIKUWA ANAIBUKA MFANYAKAZI BORA.

KUNA DOGO MMOJA ALIKUWA DEREVA MAKINI SANA HAJAWAHI HATA KUPATA AJALI, MSAFI, MSTAARABU, ANAWAHI KAZINI, ANATUNZA SIRI ZA OFISI, ANATUNZA GARI LILILONUNULIWA NA KODI ZA WANANCHI ILA ALITUMBULIWA. LEO HII ANAENDESHA BASI KWA RAHA ZAKE. SASA JIULIZE KAMA CHETI FEKI MBONA HAANGUSHI ABIRIA?
Kwa hio tufoji vyeti?

Hivi una akili timamu?
 
Kwa hio tufoji vyeti?

Hivi una akili timamu?
Ninazo nusu. Wewe mwenye cheti original umeifanyia nini nchi?

Magofool alikuwa anafukuza wenzie wakati yeye na toto lake Bashite ndio mabingwa wa kufoji.

PhD ya maganda ya korosho wakati hata kutamka sentensi mbili kwa lugha ya malkia hawezi.

R.I.P Ben Saanane.
 
Back
Top Bottom