Serikali imesema haifanyi kazi kwa maoni ya wananchi

masalia

Member
Dec 20, 2012
24
26
Akijibu hotuba ya Upinzani ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Bungeni Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Januari Makamba amesema wao Serikali hawafanyi kazi kwa maoni ya upinzani,hila mipango ya chama chao.

Hii ni kufuatia hotuba ya kambi ya upinzani kusema kuna maswala ambayo kambi rasmi ya upinzani tulihoji mwaka jana na hamjayafanyia kazi. na hivyo kambi rasmi ya upinzani inaitaka ipate ripoti ya utekelezaji (progressive report).

Hakijibu hoja hiyi Makamba akajigamba kwamba wao hawafanyi kazi kwa maoni ya upinzani.

Hii ni sawa na kusema hatutaki maoni ya wananchi kwani, Kambi Rasmi ya Upinzani ina wabunge 49 ambao wanawakilisha wananchi...hivyo kukataa kufanya kazi kwa maoni ya kambi ya upinzani ni kukataa maoni ya wananchi wanao wakilishwa na kambi hiyo.

Tujadili Wakuu!:behindsofa:
 
Updates:Serikali aina majibu ya hoja za upinzani. Waziri Mbarawa nae kasema hawezi kujibu hoja zote za upinzani, amechagua baadhi tu!:target:
 
Updates:Serikali aina majibu ya hoja za upinzani. Waziri Mbarawa nae kasema hawezi kujibu hoja zote za upinzani, amechagua baadhi tu!:target:
Kioja cha mwaka kwani hayo aliyoyachagua katoa wapi?
 
Kazi kweli kweli ila tutafika tu, naona wanaendesha nchi ki chama zaidi
Mkuu baba wa taifa alitengeneza sera ya KUJITEGEMEA sasa watawala wetu wana sera ya WAWEKEZAJI tena wa nje! Hivo hawasikii mwadhini wala nani hapa.
 
Ni kweli kuwa serikali haiwezi kufanyia kazi maoni ya upinzani, hasa pale ambapo hayaendani na utekelezaji wa sera za chama tawala. Mfano, serikali haiwezi kufanyia kazi suala la utawala wa ki-majimbo, kwa kuwa sera za chama tawala ni utawala kupitia serikali kuu. Hivyo, chama ambacho hakiko madarakani, kazi yake ni kueleza wananchi faida watakazopata kwa kukichagua chama hicho, ili 2015 wananchi wakipe ridhaa ya kushika dola.
Hongereni kwa rasimu ya Katiba mpya kukubali tume huru ya uchaguzi (ingawa kazi kubwa itakuwa katika kulinda kura zenu)
 
kalewa madaraka huyo dogo na ana bahati fitina ilfanikiwa sabu babake alikuwa katibu mkuu wa chama ajipange kwa uzuri zaidi anaweza asirudi tena mjengoni
 
Akijibu hotuba ya Upinzani ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Bungeni Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Januari Makamba amesema wao Serikali hawafanyi kazi kwa maoni ya upinzani,hila mipango ya chama chao.

Hii ni kufuatia hotuba ya kambi ya upinzani kusema kuna maswala ambayo kambi rasmi ya upinzani tulihoji mwaka jana na hamjayafanyia kazi. na hivyo kambi rasmi ya upinzani inaitaka ipate ripoti ya utekelezaji (progressive report).

Hakijibu hoja hiyi Makamba akajigamba kwamba wao hawafanyi kazi kwa maoni ya upinzani.

Hii ni sawa na kusema hatutaki maoni ya wananchi kwani, Kambi Rasmi ya Upinzani ina wabunge 49 ambao wanawakilisha wananchi...hivyo kukataa kufanya kazi kwa maoni ya kambi ya upinzani ni kukataa maoni ya wananchi wanao wakilishwa na kambi hiyo.

Tujadili Wakuu!:behindsofa:
Asanye mkuu kwa hoja nzuri marekebisho tu kwenye lugha : tumia "ila" badala ya "hila" na "akijibu " badala ya "hakijibu"
 
Tunakoenda kunahatari ya kutokea watanzania na wapinzani.!!
 
Back
Top Bottom