"Serikali 'Imeridhia' Nusu kwa Nusu, Ifikapo 2010!"

Buchanan

JF-Expert Member
May 19, 2009
13,199
1,969
Wapendwa WanaJF, kuna tangazo moja la TBC1 halinifurahishi sana, hasa linapodai kuwa Serikali "imesharidhia" kwamba mwaka 2010 wanawake na wanaume ni nusu kwa nusu kwenye nafasi ya uongozi! Swali langu la kwanza, huko nyuma Serikali ilikuwa imekataza uongozi kuwa na idadi ya nusu kwa nusu kijinsia? Pili, ubebwaji wa wanawake kwa nafasi nyeti una tija gani? Km udaktari, hivi plasmodium wanafahamu kwamba daktari anaye-deal nao ni mwanamke, kwa hiyo wata-give in? Nakaribisha mjadala!
 
mzee umeishajibu kila kitu. tz ni n pilitics kwa kwenda mbele!!!!!!!!!! sasa ukianza analysisi utaitwa mpinzani. angalia
 
sina imani na wabeijing tangu yule mama mkerewe alipotutia aibu wa tz kule bunge la afrika, loh.
 
Jakaya anawinda kura za wanawake kwa hiyo anajaribu kuwahonga vyeo hata mahala ambapo ubaguzi wa jinsia[ in this case wanaume] hauna faida kwa maendeleo ya nchi. Mwanamke au mwanaume apewe kazi/cheo kufuatana na uwezo wake na si kwasababu ya jinsia yake. Hii 50/50 ikipitishwa kama alivyoahidi muungwana itarudusha kasi ya maendeleo ya nchi nyuma; mfano ni hawa wabunge wa upendeleo wa viti maalum mchango wao bungeni ni negligible, imebakia kushindana kuvaa vitenge vya wax tu!!
 
mimi ni mwanamke na hii kitu ya nafasi za upendeleo na viti maalum (sijui vina sufi) naichukia kutoka moyoni.

uwezo wangu unipe majukumu and deliver the expected results!!! mnatudumaza bana hebu tuacheni tuwepo tunapotaka kuwa only and only if we deserve to be there!!! aaaah!!!
 
Sure, wakitaka 'usawa' waondoe kubebwa! Hivi mtu asiyebebwa ni sawa na aliyebebwa?

ukibebwa inamaana umeshindwa kutembea mwenyewe, obvious wewe si sawa na yule anayetembea mkuu!! mwenzio anajiweza!!!
 
mimi ni mwanamke na hii kitu ya nafasi za upendeleo na viti maalum (sijui vina sufi) naichukia kutoka moyoni.

uwezo wangu unipe majukumu and deliver the expected results!!! mnatudumaza bana hebu tuacheni tuwepo tunapotaka kuwa only and only if we deserve to be there!!! aaaah!!!

Kwanza heri ya Mwaka Mpya wenye baraka na mafanikio, 2010, Hongera sana kwa kuwa umeongea pointi tupu! Mtu akibebwa na kuingizwa kwenye uongozi atakuwa tegemezi kwa aliyembeba!
 
Kwanza heri ya Mwaka Mpya wenye baraka na mafanikio, 2010, Hongera sana kwa kuwa umeongea pointi tupu! Mtu akibebwa na kuingizwa kwenye uongozi atakuwa tegemezi kwa aliyembeba!

Heri na kwako mkuu!!!

na kwa uongozi wa aina hiyo bado watanzania tutegemee ufanisi na maendeleo kweli!!!
 
tatizo ni uvivu na tamaa ya madaraka ndo maana mtu anabuni mbinu ambazo anajua wazi zina madhara lkn kwa tija yake ya wakati huo,mi sioni sababu ya msingi 50 kwa 50 huu ni uvivu wa wanasiasa wetu wanatafuta kura za kinamama tu hawanalingine "ukiona mtu anakimbilia siasa jua uwezo wake wa kufikiri ni mdogo"
 
Naona kama vijineno vya mwisho viko 2 general!
 
Hizi ni propaganga za cheap politics. Kwani ni lini waliwahi kuzuiwa kushiriki kama wanakizi vigozo? Sasa kama ndio tunaanza hivi 50/50 ya kidini nayo inakuja na baadae 50/50 ya kikabila na pia ya vijana kwa wazee na wakati huo patakuwa hapatoshi maana silaha zote zitakuwazishatumiwa dhidi ya mmoja kwa mwingine.
 
...baadaye nusu kwa nusu ya walemavu/wasio walemavu! Baada ya hapo walemavu wenyewe kwa wenyewe: Albino kwa viwete, nusu kwa nusu, nk! Hapo kweli patakuwa hapatoshi!
 
Back
Top Bottom