Serikali imeongeza Deni la ndani kwa TZS 1.5T kati ya Mwezi Mei na Juni 2018: Ni ‘overdraft’ ya BoT kwa Serikali? BoT imechapisha Noti mpya?

Mwezi Juni mwaka 2017 (https://www.bot.go.tz/Publications/MonthlyEconomicReviews/MER July 2017 Final Approved.pdf ) Serikali ilikuwa na nakisi ambayo ilizibwa kwa kukopa kutoka sokoni ( T Bills and Bonds ) kwa TZS 550 bilioni. Hata hivyo ongezeko la sasa la deni la Serikali Kuu la TZS 1.5T linatia mashaka sana kwani halina maelezo ya kutosha kutoka kwenye Taarifa ya Mwezi ya Benki Kuu na Umma wa Watanzania haujaelezwa mahala popote kuwa Serikali imechukua mkopo mkubwa namna hiyo ndani ya mwezi mmoja kwenye Benki au mabenki yeyote ya ndani. Inabakia uwezekano mmoja tu, nao ni ‘overdraft’ ya Benki Kuu.

Nadharia za Uchumi zinatueleza kuwa Serikali inapokopa kwenye Benki Kuu yake ili kuziba nakisi (deficit financing) hupelekea ama Benki Kuu kutumia akiba zake ‘reserves’ au kwa kuchapisha noti mpya. Ukitazama ‘reserves’ za Benki ya Tanzania kutoka kwenye Taarifa yake ya Hesabu zilizokaguliwa za Mwaka unaoishia Juni, 2017 utaona kuwa akiba pekee ambayo ingeweza kutumika ni ya gawio TZS 300 bilioni. Akiba hii tayari Serikali imekwisha itumia tangu mwanzoni mwa mwaka huu. Kinachobakia ni kuchapisha noti (printing additional currency).

Ni muhimu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania atoke wazi kuueleza Umma, ni wapi BoT imezitoa pesa TZS 1.5T za kuipa Serikali kufanya matumizi yake. Kama hali ya uchumi ni mbaya kiasi cha Benki Kuu imechapisha noti mpya na kuziingiza kwenye mzunguko ni muhimu Watanzania waelezwe na ni nini madhara ya uamuzi huo wa Serikali kuchapisha noti mpya.:oops::oops::oops:
 
Naiona Tanzania yetu ikielekea kusikojulikana, nasa mifumo yetu, taasisi zetu, viongozi wetu, wanasiasa wetu, wataalam wetu na makundi mengine ya kijamii pale wanapo iachai nchi kwa mtu mmoja!.
Kama anaing'ang'ania UNAFANYAJE?
 
Muda huo wa kuandamana utakapofika, watakao andamana sio Wasukuma!, tena unaweza usiamini, watakao anza kuongoza maandamano hayo ni Wachagga!.
P
IMG_20180910_080030.jpg
 
P, miaka 7 ya nini? Nyota njema huonekana asubuhi na tumeshauona 'wema' wake. Miwili iliyobaki inatosha sana!
Mkuu Msenga, japo kwa sasa nalaumiwa kwa kuusema ukweli kuwa Magufuli is there to stay, lakini ninachokifanya ni kitu kizuri sana, kuwaandaa watu kisaikolojia kuwa kama hali ni hivi hii miaka 3 tuu, bado kuna miaka mingine 7 ahead!.

P.
 
uoga hofu taharuki imetamalaki ktk nchi

wako wapi kile kizazi cha kuhoji

wako wapi wanaharakati waje waseme

hivi kweli tunaacha taifs liangamizwe kwa kuhofia kufa
 
Maprofessa Wabobezi mfano Prof.Wangwe, Prof. Ngowi, Prof. Osoro na Prof. Ndullu mko wapi ili kuishauri Serikali juu ya mwenendo wa uchumi.
 
Tokea alivyokutukana kuwa unanjaa ulivyokuwa unamuhoji maswali ya kitoto ubongo wako umesinyaa mithiri ya sura ya mr.slow slow
Wewe nawe kiwqngo chako cha ustaarabu ndo kimekomea kwenye kumuatak mtu binafsi badala ya kushughulika na hoja yake. Huo ndo utoto wa kifikra!
 
Nchi inaangamia hii!!

Niliwahi sema,huyu bwana atatuachia ndege,fly overs,SGR,madaraja, n.k lakini huku wananchi wakiwa "hoheha" na uchumi umevurugika kiasi kwamba mwananchi hatoweza kuitumia miundombinu hii kujiletea maendelea maana mfukoni atakuwa mkavu kutokna na hali ya uchumi, hakopeshiki(biashara haziendi, pia wengi kutokuwa na ajira na hivyo kutokopesheka,n.k) na wanaokopesheka nao wanalipa mikopo yao kwa tabu na kuna hatari hata lending institutions nazo zika-collapse.

Pia tufahamu japo kukopa hakukwepeki, lakini kukopa kupita kiasi kunafanya deni la Taifa kukua na ili tuendelee kukopesheka inatubidi tuwe na nidhamu ya kulipa lakini unapolipa deni la Taifa linalokua kila kukicha ili uendelee kukopesheka, tafsri yake ni kutumia sehemu kubwa ya mapato ya nchi kuhudumia deni la Taifa na matokeo ni kupunguza uwezo wa serikali kuhudumia wananchi wake katika nyanja mbalimbali kama elimu,maji,kutoa ajira,mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu,kuongeza mishahara ya watumishi,n.k.

Kibaya zaidi, miradi tunayoikopea(na hata ile tunayoitekeza kwa kutumia fedha zetu za ndani) ili kuikamilisha kama ujenzi wa reli,ununuzi wa ndege,meli,ujenzi wa fly overs,kuhamia Dodoma,n.k mingi sio miradi ya kuzalisha fedha hivyo ni mzigo kwa serikali tu japo ni kweli tunaihitaji ila ilipaswa kutekelezwa kwa awamu na kushirikisha sekta binafsi kwa baadhi ya miradi ili kuipunguzia serikali mzigo.

Kwa mfano,kuhamia Dodoma(kujenga mji wa kiserikali) tu kunahitaji zaidi shilingi za kitanzania zaidi ya trilioni 10(ingia site ya manispaa ya jijji la Dodoma uthibitishe maana taarifa hii iko wazi).

Sasa kwa nchi masikini kama hii na huu mzigo wa gharama kama hizi tena ndani ya muda mfupi tu kweli tutabaki salama?

In short,kuna uwezekano tukawa kama raia wa Ethiopia unless wanachukua tahadhari sasa.

Anyway,labda vyanzo vya mapato navyo vinaongezeka sambamba na matumizi.


kwahiyo ulitaka nini kifanyike mbona hujatoa suluhisho
 
Mkuu uliwahi kusema fisadi lowassa asipochukuwa nchi utageuzwa kinyume na maumbile vipi umeisha timiza ahadi yako na kama bado unasubiri nini?
Nishakwambia wewe hama toka hapo mtongani rudi kwenu karagwe wewe mushuti
 
Acha kulisha watu matango pori. Hiyo ni dalili kuwa fedha zetu za ndani zimepungua sana kwenye mzunguko na ni matokeo ya jiwe kufanya mamiradi yake haya kwa kutumia fedha za ndani. Madhara yake ni makubwa sana.
Hivi wew una unachokijua kweli? Govt ecpenditure ni sehem ya pesa kuwa kwenye mzunguko
Ina maana kama gvt ikiwa na projects nying, maana yake ni kuwa govt expenditure ipo juu na pesa itakuwa kweny mzunguko. Kilichofanya pesa ipotee kwa sasa ni kwa sababu serkali inakusanya more tax than its expenditure ndo maana pesa imepungua. Hiyo ni fiscal and monetary policy inaitwa. Na pia inflation inapungua.
 
Chakubanga atakuja na ukokotoaji wake,utasikia ukichukua hii jumlisha na ile ,halafu unakopa hapa unatoa kule!!.Chakubanga ni mzigo jamani.
 
Kuhamia dodoma, hamahama ya wanasiasa na marudio ya uchaguzi kila mara havitoacha nchi salama. Gharama zake ni kubwa mno
 
Ukizungumzia dola mimi na machozi hunitoka. Pesa ya bongo imekuwa makaratasi tu. We are heading to 2500tsh per dollar very soon.
Hii pia ina uzuri wake mkuu kwenye international trade iskutoe machozi. Angalia usa kila siku wanapiga kelele china wa devalue pesa yao against dollar yaani wanshusha thamani hela yao. Ushajiuliza kwanini
 
mimi husema
USISHANGILIE TU MAENDELEO YA JAMBAZI
jaribu kutafakari pia ni wangapi kawapiga risasi, wangapi kawateka na kuwapoteza, wangapi kawanyang'anya, vingapi kaviweka rehani..
Wangapi kawarudisha nyuma kulikopelekea yeye kwenda mbele..
Baada ya tafakuri hiyo, sasa amua kumuunga mkono jambazi aliyenunua BMW na kukupa lift au kumpotezea kama mimi ninavyokosaga muda kufyagilia wanyang'anyi hadi wa kura !
 
Back
Top Bottom