Serikali imeongeza Deni la ndani kwa TZS 1.5T kati ya Mwezi Mei na Juni 2018: Ni ‘overdraft’ ya BoT kwa Serikali? BoT imechapisha Noti mpya?

broo
pesa hushuka thamani kwa njia mbili..
1- Kuishusha thamani pesa yako ili kuvutia wanunuzi wa nje kuja ndani kununua bidhaa kwa wingi..
2-Pesa hushuka thamani kutokana na uchumi wa nchi kuwa mbovu..
Kwa mawazo yako kipindi Zimbabwe wanabadilisha dola moja ya Marekani kwa dola laki mbili za kwao, uchumi wao ulikuwa bomba..
kkkkk !
Tanzania bado tuna safari ndefu, nyufa huitwa urembo..
Kwa hiyo wew unaamini Tz inashusha thamani kwa sababu ipi
 
Ndugu zitto nimesoma uchambuzi wako hakika unafikirisha na hata tusiokuwa wataalamu wa mambo ya fedha na uchumi tunapata muda wa kujua mambo mapya na kuchukua muda kujisomea zaidi.

Ila kwa kuwa swali lako limejiegemeza kwa BOT lakin umeliweka public na mimi kama Mtanzania nimeona nitoe maoni.

Maoni yangu yanaweza kumalizika kwa maswali pia kama wewe ulivyomaliza.

Kwanza mara nyingi umekuwa ukituhumu vyombo vyetu vya vinapika "data" ili kuisifu serikali sasa nashangaa msingi wa swali lako kwa hao unaoamini wanapika "data".

Pili huwa nasoma uchambuzi wako wa masuala ya uchumi na fedha ila nikienda kutazana ulichosema nakuta kuna facts umezikwepa kwa makusudi.

Kama nilivyosema mimi sio mtaalamu wa uchumi na fedha lakin baada ya uchambuzi wako nimejibidiisha kutafuta fact.

Msingi wa swali lako limejiegemeza kwenye upatikanaji wa 1.5T sasa twende moja kwa moja kwenye ripoti ya BOT 2016/17 ukurasa wa 128 unaonesha Currency in circulation na currency in custody.

Sasa ukiangalia as per report tuna custody ya 4T(notes) na 52B(coins).
Serikali inashindwa kukopa kwenye custody as an immediate source of fund?
View attachment 861952

Pia nimepitia monthly Economic review ya june 2017 kwenye government bugetary operation inaonesha revenue zilikuwa 1.2T na expenditure 1.4T bila kuonesha ongezeko lilitoka wapi.
Je unadhan na mwaka jana waliprint pia?
View attachment 861947

La mwisho kabisa umeibua maswali yako ukijua wazi ripoti ya mwisho ya BOT itaonesha lakin umewawahi kwa maswali ili kabla ya final report.

Kwa kuongezea tu ni kweli unatusaidia watu tunaopenda kujisomea hadi na sisi tusiojua mambo ya uchumia na fedha tunajitahidi kurudisha maswali kwako lakin unaibua tension kubwa kwa wavivu na wasio na ufahamu.

Ukiangalia hata mijadala inayoendelea ni kama watu wameshaamini kuna printing na hakuna anayetaka kujadili kwa fact.

Innocent Nyika
Makambako-Tanzania
Nadhani zitto anajua fika kuwa watz ni wavivu kutafuta facts au kudadavua mambo, kwa hiyo ana take advantage of that. Watu wanashindwa kwenda kwenye report husika ndipo akaja hapa ki comment
 
Ningependa kufahamu thamani ya Mali za serikali ni kiasi gani na pia Mali hizo zina reflect vipi ktk deni letu la ndani .
 
This is good news, print more money, pump to the circulation and let people enjoy the life.
 
Kwa mfano,kuhamia Dodoma(kujenga mji wa kiserikali) tu kunahitaji zaidi shilingi za kitanzania zaidi ya trilioni 10(ingia site ya manispaa ya jijji la Dodoma uthibitishe maana taarifa hii iko wazi).
Tatizo la nchi hii kila mtu anapanga. Kazi ya kupanga mipango ina specialists wake. Lakini kwa bahati mbaya zaidi mfumo wetu wa uchumi unatumikia siasa na sio siasa kutumikia uchumi.

Such a bad abnormality
 
Pia tufahamu japo kukopa hakukwepeki, lakini kukopa kupita kiasi kunafanya deni la Taifa kukua na ili tuendelee kukopesheka inatubidi tuwe na nidhamu ya kulipa lakini unapolipa deni la Taifa linalokua kila kukicha ili uendelee kukopesheka, tafsri yake ni kutumia sehemu kubwa ya mapato ya nchi kuhudumia deni la Taifa na matokeo ni kupunguza uwezo wa serikali kuhudumia wananchi wake katika nyanja mbalimbali kama elimu,maji,kutoa ajira,mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu,kuongeza mishahara ya watumishi,n.k.
Kwa bahati mbaya sana, nidhamu ya kulipa madeni yetu kwa kweli iko chini. Tuna madeni ya mifuko ya hifadhi ya jamii ambayo sidhani kama yanaendelea kulipwa. (Maybe wanaojua watusaidie). Tuna kasma ya matumi ya kawaida ya lazima kama mishahara na uendeshaji wa serikali ambayo haikwepeki na ni lazima tuifanye. Licha ya hayo, uwezo wetu kimapato ni mdogo na ndio shida inapoanzia.

Nonetheless, Miradi hii kwa kweli ingependeza kama tungeifanya kwa kushirikiana na sekta binafsi kama mdau alivyosema kwa sababu katika uhalisia wake miradi hii ni mikubwa mno ukilinganisha na uwezo wa serikali yetu kimapato
 
Niliwahi sema,huyu bwana atatuachia ndege,fly overs,SGR,madaraja, n.k lakini huku wananchi wakiwa "hoheha" na uchumi umevurugika kiasi kwamba mwananchi hatoweza kuitumia miundombinu hii kujiletea maendelea maana mfukoni atakuwa mkavu kutokna na hali ya uchumi, hakopeshiki(biashara haziendi, pia wengi kutokuwa na ajira na hivyo kutokopesheka,n.k) na wanaokopesheka nao wanalipa mikopo yao kwa tabu na kuna hatari hata lending institutions nazo zika-collapse.
Ndege, flyovers na kadhalika ni vitu katikati ya maendeleo ya watu. Ufanisi mkubwa wa maendeleo ya watu ni maisha wanayoyaishi. Hatupingi anayoyafanya, lakini kinachotakiwa ni kujenga uwezo wa kimaisha kwa wananchi ili hata akiondoka hizo ndege na SGR tuzifaidi vizuri
 
Mkuu Msenga, japo kwa sasa nalaumiwa kwa kuusema ukweli kuwa Magufuli is there to stay, lakini ninachokifanya ni kitu kizuri sana, kuwaandaa watu kisaikolojia kuwa kama hali ni hivi hii miaka 3 tuu, bado kuna miaka mingine 7 ahead!.

P.
duuuhhh . . . . . . . mkuu hii kauli yako hii . . . . . .
 
Mfalme jiwe amebakiza miaka miwili ,usiulize kwanini ila utajua muda ukifika. Hata adolf hitler alikuwa na mipango na programs tofauti mpaka 2050 lakini hakufika huko.amini usiamini jiwe atatoka kiulaini kuliko unavyodhani
mmmmhhhh . . . . . . . . unasemaje ???? atatoka kiulaini ? ? ?
 
Zitto amenukuu taarifa ya BOT, hayo maswali yote waulize BOT,ndio maana Zitto ameweka hadi rejea ya taarifa yake
mkuu . . . naomba nikusaidie hapo. Ni kawaida kwa miezi ya kufunga robo au mwaka wa fedha kuwa na makusanyo makubwa kuliko unavyodhani maana watu hulipa kodi stahiki pamoja na madeni ya nyuma ndio maana mwezi wa sita takwimu za makusanyo zina shoot
 
Back
Top Bottom