Serikali imeombwa kuhamasisha ufugaji wa Ngamia hasa kwenye maeneo ambayo yamekuwa na migogoro kati ya wafugaji na wakulima


D

davimsu

Member
Joined
Mar 28, 2019
Messages
14
Points
45
D

davimsu

Member
Joined Mar 28, 2019
14 45
Serikali imeombwa kuhamasisha ufugaji wa Ngamia hasa kwenye maeneo ambayo yamekuwa na migogoro kati ya wafugaji na wakulima , ili kupunguza migogoro hiyo ikiwemo

Akizungumza na waandishi wa habari leo mfugaji wa wanyama hao Dahir Jama Yussuf mkazi wa kijiji cha Mtakuja kata ya Kia, wilayani Hai mkoani waliomtembelea kijijini hapo, kufahamu namna alivyo weza kuwafuga wanyama hao bila ya kuwepo kwa migogoro kati ya wakulima na wafugaji.

Yusufu,alisema wanyama hao ni rafiki na wakulima kwani wakipita shambani hawali mazo kama walivyo wanyama wengine kama Mbuzi na kondoo

Ngamia ni rafiki wa mazingira kutokana na kwamba wanyama hao hawali mimea ya kupandwa isipokuwa miti ya majani ya asilia na kwamba hawana kwato ambazo zingesababisha aridhi kuchimbika na kusababisho lisema Yusufu.

Ili kuamliza au kupunguza migogo hiyo nashauri watu wafuge mnyama huyo kwa hana ngarama kubwa ya kumtunza na wala hali mazao ya wakulima''alisema


Akizungumzia kuhusu maziwa ya ngamia yametajwa kuwa moja ya chakula muhimu chenye virutubisho vingi vyenye kinga ya magonjwa mbalimbali mwilini yakiwemo magonjwa ya ukimwi , kisukari vidonda vya tumbo, fizi kutoa damu upungufu wa vitamin C,”alisema

Na kwamba ngamia mmoja anauwezo wa kutoa lita ishirini kwa siku moja na maziwa hayp lita moja inauzwa sh,3000,ambapo alisema soko lipo baadhi ya mikoa ikiwamo Arusha ,Dodoma na Daar salaam

Changamoto kwamba baadhi ya watu wanamuamko mdogo kuhusu unywaji wa maziwa hayo hivyo kusababisha soko kuwa dogo la bidhaa hiyo nimeanza kufuga wanya hao toka 1996 na sasa nina ngamia 80

Alisema mbali na kuwa na faida hiyo ya kutoa maziwea yenye virutubingamia ni mnyama anayeweza kutumika kubebea mazao shambani , usafiri wa kubebea wagonjwa au kama usafiri wa kawaida kutoka eneo moja hadi jingine.

Kwa upande wake Mkurungenzi wa Kituo cha utafiti wa Mifugo Kilichopo Westi Kilimanjaro Wilayani Siha,Nguluma Athumani ,alisema maziwa ya Ngamia ni mazuri mbali na Kinywaji na Dawa ya vidonda vya tumbo pia inasaidia kuongezeza nguvu za kiume

“Maziwa ni mlo kamili kwani yamebeba virutubishoi vya aina zote vinavyohitajika katika mwili wa binadamu, kwani unapokunywa maziwa kwa wingi yanafaida ya kuujenga mwili pamoja na kinga ya magonjwa,”alisema Athumani

Mwisho.Sent using Jamii Forums mobile app
 
B

bagamoyo

JF-Expert Member
Joined
Jan 14, 2010
Messages
5,966
Points
2,000
B

bagamoyo

JF-Expert Member
Joined Jan 14, 2010
5,966 2,000
Picha tafadhali ili kukamilisha habari hii ya kutoka KIA wilayani Hai mkoani Kilimanjaro.
 
MIXOLOGIST

MIXOLOGIST

JF-Expert Member
Joined
Mar 1, 2016
Messages
3,585
Points
2,000
MIXOLOGIST

MIXOLOGIST

JF-Expert Member
Joined Mar 1, 2016
3,585 2,000
Sijawahi kusikia utendaji wa ngamia kwenye tendo letu pendwa, natia shaka kama hayo maziwa yao yana input yoyote kwenye nguvu pendwa
 

Forum statistics

Threads 1,284,199
Members 493,978
Posts 30,816,961
Top