Serikali imelitaka Shirika la Wakimbizi(UNHCR) kuongeza kasi ya kuwarudisha kwao raia zaidi ya 34,000 wa Burundi

Kunguru Mjanja

JF-Expert Member
Aug 22, 2012
2,036
3,929
Waziri wa mambo ya Ndani Mh.Mwigulu Nchemba amelitaka Shirika la wakimbizi UNHCR kuongeza kasi ya kuwarudisha kwao raia wa Burundi zaidi ya 34,000 walioko kwenye kambi za wakimbizi za Nduta, Nyarugusu na Mtendeli zilizoko mkoani Kigoma ambao waliomba kwa hiari yao kurudishwa.

ITV
 
images (1).jpg
download.jpg

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dkt. Mwigulu Nchemba ameliagiza Shirika la Kuhudumia Wakimbizi Duniani (UNHCR) kuwaondoa wakimbizi 32,000 ambao wameomba kwa hiari yao kurudi katika nchi yao ya Burundi haraka tofauti na wanavyofanya sasa.

Mwigulu ameyasema hayo wilayani Ngara alipotembelea kituo cha mapokezi ya wakimbizi cha Lumasi kujionea shughuli zinazoendela katika vituo vya mapokezi ya wakimbizi ambavyo serikali ikishaagiza vifungwe mara moja.

Amesema UNHCR wanafanya kazi saa 24 katika kuwapokea wakimbizi kuingia nchini lakini wanakuwa wazito pale wakimbizi wenyewe wanapotaka kwa hiari yao kurudi kwao baada ya kujiridhisha kuwa kuna amani nchini kwao.

“Tunaanza kupata wasiwasi kuwa mnafaidika na hawa wakimbizi kubaki hapa nchini wakati wao wanaitaji kurudi makwao, naagiza muwaandikie barua leo hii kuwa hao wakimbizi ambao wapo katika kambi za Nduta, Nyarugusu na Mtendeli waondolewe haraka sababu hatuwezi kaa na watu ambao wanaitaji kurudi kwao wakajilete maendeleo,” amesema Mwigulu.

Waziri Nchemba aliongeza kuwa hatakaa kikao cha pande tatu kujadili kuhusu kuondoka kwa wakimbizi hao kwani wamesha kaa mwaka jana wakakubaliana jinsi ya kuondoka kwa wakimbizi hao nchini kwani mda huu ndii mda wa kilimo na kuwapeleka mwezi wa nne huko nikiwafanya wakaishi maishi magumu zaidi.
 
Na keshokutwa na sie tutaenda wapi manake kwa hali ninayoiona hatuna muda na sie tutakuwa wakimbizi, sasa kama tunawarudisha sie tutaenda wapi
Kwa Tanzania kama suala la ukimbizi sahau kabisa kamwe halitatokea mpaka ukamilifu wa dahari.
 
Jipe moyo, kwa tunapoelekea, tuombe uhai na uzima, we unadhani watu wamekaa kimya tu, subiri siku zijazo, mambo ya sporadic battle yatakavyokuwa yanaibuka, hakuna mtu alitegemea kuwa chama pinzani kitakuja kuwa na nguvu mpaka chama tawala sasa hivi ni full kutesa, kiteka, kuua, ili tu wabaki madarakani, sikulitegemea, nilioma vyama vya upinzani vinajisumbua, muda leo umesema mpaka kijani wanaweweseka, wanaona watumie ujambazi na udhalimu ili wabaki madarakani, sidhani kama ulilijua hilo mkuu, na hilo la kongo ndio linalofata, hakuna mtu anayefurahia ndugu na jamaa zao kuteswa, kutekwa, kuuliwa, nk
 
Uko sawa mkuu. Ccm wanafikiri watanzania hawana akili timamu.
 
Yanii Mwigulu naee hili la Huyu mtoto wa watu kupigwaa risasi hajaliona????? This shthole country this is too much...
 
Jipe moyo, kwa tunapoelekea, tuombe uhai na uzima, we unadhani watu wamekaa kimya tu, subiri siku zijazo, mambo ya sporadic battle yatakavyokuwa yanaibuka, hakuna mtu alitegemea kuwa chama pinzani kitakuja kuwa na nguvu mpaka chama tawala sasa hivi ni full kutesa, kiteka, kuua, ili tu wabaki madarakani, sikulitegemea, nilioma vyama vya upinzani vinajisumbua, muda leo umesema mpaka kijani wanaweweseka, wanaona watumie ujambazi na udhalimu ili wabaki madarakani, sidhani kama ulilijua hilo mkuu, na hilo la kongo ndio linalofata, hakuna mtu anayefurahia ndugu na jamaa zao kuteswa, kutekwa, kuuliwa, nk
Labda kama wewe ni wa juzi juzi kuzaliwa ....CUF ilitisha sana miaka ya 90s mara tu baada ya vyama vingi kuanzishwa 1992 mpaka damu ikamwagika huko Pemba.Na hapa Dar ukisikia mkutano wa CUF lazima tu siku hiyo mabomu ya machozi yatatumika uatawala wa Mkapa kama Rais wakati huo.

Sasa hakuna chama chenye nguvu kama unavyofikiria sema tukio dogo tu linasikika haraka sana kwasababu ya mitandao na wingi wa vyombo vya habari ila hakuna nguvu kubwa ya chama chochote kama ilivyokuwa wakati ule.

Wengi wamebaki tu kulumbana kwenye mitandao lakini mitaani huko watu wanahangika na maisha yao wale nini wavae nini basi.

Kutokea sijui vita ya wenyewe kwa wenyewe au sijui wakimbizi hilo sahau kabisa HALIWEZI kutokea ndani Tanzania.Na Mungu ana makusudi na hili Taifa na watu wake.

Nimetembea mikoa yote ya bara na visiwani watanzania wa zamani wa kizazi kipya nawafahamu vizuri sana ndani na nje HAKUNA VITA Tanzania na kamwe halitatokea.
 
Unatumia vigezo gani kusema vita haiwezi kutokea?
Hiyo miaka unayosema ni upande wa visiwani tu ndiyo walikua wanafanya vurugu bara hakuna aliyeanzisha.

Kungekua na organized movement kati ya bara na visiwani nini kingefuata?

kwa viongozi wa upinzani wanaokwenda kunywa juisi ikulu na wengine bado wana kadi za chama tawala ni kweli vita haiwezi kutokea.
 
Na haitatokea vita ndani ya nchi yetu ya Tanzania kama wengi wanavyoongea ongea tu...wakati ikipigwa risasi moja tu wengi wanakimbiza roho zao.

Tatizo la watanzania maneno mengi vitendo hakuna ujasiri wa watanzania ni wakati wa kumpiga na kumchoma moto kibaka aliyeiba simu au bodaboda kumfukuzia dereva aliyemgonga mwenzao basi.

Watanzania wengi ni waoga hawana misimamo ni vigeugeu tu leo wako ccm kesho chadema keshokutwa tena wako ccm.
 
Na keshokutwa na sie tutaenda wapi manake kwa hali ninayoiona hatuna muda na sie tutakuwa wakimbizi, sasa kama tunawarudisha sie tutaenda wapi
Umetoka usingizini nini na kuanza kuropoka!??? Kawe mkimbizo mwenyewe!! Kazi kuombea mabaya taifa letu!! Anza kuwa mkimbizi Nyumbani kwako kaishi mitaani hukose mahali pa kulala na kujisitiri ndo utatia adabu
 
Umesema ukweli na hao ndiyo wachawi wa maendeleo ya nchi hii
 
Back
Top Bottom