Serikali imeliagiza TANESCO kutoagiza transfoma kutoka nje ya nchi

Queen V

JF-Expert Member
Jan 19, 2012
775
1,332
Serikali imeliagiza Shirika la Ugavi wa Umeme Tanzania (TANESCO) kutoagiza transfoma nje ya nchi na badala yake kutumia zinazotengenezwa hapa nchini na kampuni ya Tanalec.

Agizo hilo limetolewa leo Bungeni Dodoma na Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Mhe. Dkt. Medard Kalemani alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Tunduru Kusini, Mhe. Daimu Iddi Mpakate aliyetaka kujua ni lini Serikali itatoa pesa kukamilisha miradi ya umeme wa Wakala wa Umeme Vijijini (REA).

Dkt. Kalemani alisema uzalishaji wa transforma ni mkubwa ikilinganishwa na mahitaji ya bidhaa hizo kwa mwezi, hivyo hakuna sababu ya kuagiza transforma hizo kwa bei kubwa wakati zinapatikana hapa nchini.

Kuhusu suala la kugharamia nguzo kwa Mpango wa REA Dkt. Kalemani alisema mteja hatakiwi kutozwa gharama yoyote ziadi ya Tshs. 27,000 fedha ya kuunganishiwa umeme kwa mpango huu.Dkt. Kalemani alisema kuwa Serikali inatekeleza Mradi wa REA Awamu ya II katika Wilaya ya Tunduru na kazi hii inategemewa kukamilika mwishoni mwa mwezi Juni, 2016.

Alisema Kazi ya kupeleka umeme katika wilaya hiyo ni pamoja na ujenzi wa njia ya umeme msongo wa kilovoti 33 yenye urefu wa Kilomita 293. 2, na ujenzi wa njia nyingine yenye msongo wa kilovoti 0.4 yenye urefu wa kilomita 76.1 na ufungaji wa transfoma 38 pamoja na kuwaunganishia umeme wateja wa awali 3,330

“Gharama ya Mradi kwa Mkoa wa Ruvuma ikiwemo Wilaya ya Tunduru ni Tsh. Bilioni 32.56,” alisema Dkt Kalemani na kuongeza kuwa mkandarasi amekwishalipwa bilioni 27.22 sawa na asilimia 83.6 ya fedha.
Dkt. Kalemani amesema kuwa katika Wilaya ya Tunduru ni vijiji vinne ambavyo vimeunganishiwa miundombinu ya umeme na kufanyiwa majaribio kabla ya kuwashiwa umeme.

Kwa mujibu wa Dkt. Kalemani mkandarasi anaendelea kufunga transforma na Mita za Luku katika vijiji 34 vilivyosalia kwa Wilaya ya Tunduru ili viweze kupatiwa huduma ya umeme ifikapo tarehe 30 Juni, 2016.
 
Hatutaki maneno maneno haya ila tunachotaka kuona ni tanesco kutoagiza transformer kutoka nje tunahitaji kuona na sio kuishi kwa hisia...
 
Hivi kwanini TANESCO haijaorodheshwa kwenye soko la hisa Dar es Salaam?
 
LEMA LEMA LEMA LEMA kawaeleza ukweli na wamefuata maagizo ya UPINZANI tunavyosema wanafuata ILANI YA UKAWA wanatubeza kisha wanatuiga hahaha ccm ni ile ile.


swissme
 
Nimenza kuamini..
Lema ni kichwa na hua apindishi maneno..
tunakushukuru Mh.Lema kwakuokoa Kodi zetu..
 
Mh. Lema matokeo ya mchango wako kuhusu Tanalec imetekelezwa.Asante Mbunge wangu Arusha hatukutuma utetee jimbo tu bali Tanzania nzima.Akili yako imewaacha mbali wanaotaka kujenga masanamu badala ya maendeleo kwenye majimbo yako.Keep it up.
 
Yale yale ya sukari! Mtaona kama TANESCO itaweza bei za TANALEC. Lesson: Do not trust watu wanaojiita "wanyabiashara wazawa" Biashara huwa hazina "uzawa". Biashara zote zinatumia zaidi neno "faida". Hawa wanaojiita wazawa kwa kuficha neno "faida" ni waongo, na wala hawana huruma kwa watanzania. Kwa nini hatujifunzi kutokana na suala la sukari? ukiamua kuwasaidia hao "wazawa" (kwa kuzuia bidhaa toka nje), lazima utawaumiza wananchi (kwa kununua bidhaa hiyo kwa bei ya juu zaidi). Mtu yeyote makini, hawezi kuchukua option ya kwanza. Tutaendelea kukosoa hizi sera za hovyo hovyo.
 
Back
Top Bottom