Serikali imekiri kupokea taarifa ya kuzaliwa kwa watoto mapacha walioungana mkoani Kagera

tatum

JF-Expert Member
Jan 16, 2018
5,786
4,490
Serikali imekiri kupokea taarifa ya kuzaliwa kwa watoto mapacha walioungana mkoani Kagera, na kumtaka Mganga Mkuu wa Serikali kuwasiliana na Mganga Mkuu mkoani Kagera, kuweza kufanikisha kuletwa Muhimbili kuangalia uwezekano wa kuwatenganisha haraka iwezekanavyo. #Bungeni


=======

1.jpg

Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto , Ummy Mwalimu amemwagiza Mganga Mkuu wa Mkoa wa Kagera, kuhakikisha watoto waliozaliwa wakiwa wameungana wanafikishwa Muhimbili.

Waziri Ummy ametoa kauli hiyo leo bungeni wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Viti Maalumu, Suzan Lyimo ambaye alihoji je serikali ina taarifa kuwa kuna watoto wamezaliwa Kagera wakiwa wameungana.

Akijibu swali hilo, Ummy amesema: “Wanaozaliwa wakiwa na maumbile ya ajabu wapelekwe hospitali.“Na kuhusu watoto waliozaliwa wakiwa wameungana huko Kagera, namwagiza Mganga Mkuu wa Mkoa wa Kagera ahakikishe watoto hao wanafikishwa Muhimbili,”.


Chanzo: Presstz


Soma: Kiaka, Kagera: Mapacha wengine walioungana wazaliwa
 
Back
Top Bottom