#COVID19 Serikali imejipangaje kwa kadi feki za chanjo ya Corona?

SOPINTO

Senior Member
Oct 19, 2020
155
385
Ukiwasikiliza watanzania wengi wanaonekana wanahofu na chanjo ya Korona lakini hawana mpango wa kuchanja na unapomuuliza kuwa je endapo masharti ya nchi yakabadilika katika swala zima la kupata chanjo ya korona kama vile kukosa huduma za msingi pale ambapo utaonekana kuwa huna kadi ya Kovid 19 au hujapata chanjo ya Kovidi? asilimia kubwa ya majibu ni kwamba Bongo kila kitu kipo ukitaka original unapata na ukitaka feki unapata tu ni wewe kuamua.

Majibu haya yananipeleka mbali sana na kuamini kuwa kadi feki zitakuwa mkombozi kwa wale ambao hawataki kupata chanjo , kwa mfano nikikumbuka juu ya chanjo ya homa ya manjano (Yellow Fever) , kadi hii pia ni moja ya kadi iliyotumika kama moja ya vielelezo vya kupata baadhi ya huduma ndani na nje ya nchi , mfano ukitaka kusafiri kwenda nchi za magharibi ili upewe Visa ni lazima uwasilishe hiyo kadi , lakini wabongo kwa ujanja wao walifanikiwa kutoa kadi feki ambayo inafanana kwa asilimia 100 na ile yenyewe na kwa sababu serikali haipo makini ili jambo la kadi feki za yellow fever mpaka sasa kadi hizo zimefanikiwa kwa kiasi kikubwa sana.

Mtindo huu ndio unaoonekana kusubiriwa kwa hamu kubwa na watanzania wengi kuwa hawatachanja lakini kadi watapata, sasa sijui serikali imejipangaje juu ya hili swala tumbuke kuwa ukiacha hizo kadi feki kutoka kwa wajanja wa mjini pia kuna zile kadi zitakazokuwa zimeachwa na waliochanja aidha kwa wao kuhama eneo au kutokujali kuchukua hiyo kadi na wahudumu wa chanjo watageuza kuwa fursa kwao kwa kuwauzia wale wenye kuhitaji angali hawataki kuchanja.

Binafsi nimeona katika jicho la angalizo tu .

UKO NCHINI CANADA HALI IKOJE?
Waziri wa Uraia na Uhamiaji wa Canada Marco Mendicino, ametangaza kuwa wale ambao wamechomwa dozi mbili za chanjo dhidi ya corona (Kovid-19) watapewa hati ya chanjo itakayotumika katika safari za kimataifa.

Mendicino, ambaye hakutoa tarehe halisi, alisema kuwa mpango huo utatekelezwa katika siku za kwanza za msimu wa vuli.
Akielezea kuwa serikali yake inafanya kazi na nchi zingine kutambua hati za chanjo, Mendicino alisema kuwa watu wa Canada waliopata chanjo kikamilifu wataweza kupata hati ya serikali ambayo itathibitisha historia yao ya chanjo ya Kovid-19 kwa sababu za kusafiri kimataifa.

Mendicino pia alisisitiza kuwa hati ya chanjo itakayotolewa itajumuisha data juu ya aina, tarehe na mahali pa chanjo zilizotolewa, na kubainisha kuwa utumiaji wa hati iliyoandaliwa kwa safari za kimataifa baina ya nchi imeachwa kwa uamuzi wa serikali za majimbo.
Mfumo wa hati ya chanjo, ambao unaendelea kutumika Bulgaria, Jamhuri ya Czech, Denmark, Ujerumani, Ugiriki, Croatia na Poland, pia ulianzishwa huko Japan mnamo Julai.

Wale wanaotumia programu ya ArriveCAN, ambayo Canada ilizindua mnamo Julai, wameondolewa ulazima wa kukaa karantini wanapoingia nchini ikiwa watathibitisha maelezo yao na kujaza data zinazohitajika kwenye programu.
 
Zina security features ambazo scanner zinadetect. QR codes pia zikiscaniwa zina mpeleka anaye scan kwenye taarifa zako. Hadi picha kwa sababu id za nida zinahusika pia
 
asante kwa uafafanuzi mzuri

Hizo fake zitatolewa na wahudumu hao hao wa afya kwa maana mtu hakuchanjwa lakini anatoa mchango wa mafuta kidogo anapewa kadi, Afisa Elimu Arusha sikaonyesha mfano!
 
Hizo fake zitatolewa na wahudumu hao hao wa afya kwa maana mtu hakuchanjwa lakini anatoa mchango wa mafuta kidogo anapewa kadi, Afisa Elimu Arusha sikaonyesha mfano!
kwenye detection watafeli mana information na picha vitatofautiana
 
Hao watumishi ndiyo wataingiza taarifa zako lakini hutachanjwa
watumishi hao hao wanaweza kukupiga maji badala ya chanjo..

mbona mkuu huwaamini watumishi?
wale wana kiapo mkuu .. tafadhali usiwazushie . watumishi ni waaminigu na hawawezi kufoji kwa sababu unafanya booking then cheti chato kinatengenezwa.. labda uongee na nesi asikuchome sindano ila akupe tu kadi .. labda hicyo ila unamdanganya nani?

siku ikikupata ukifa utakuwa umemkomoa nani.\\anti vaxii mna mambo sana
 
Hujaona juzi hapa Arusha maigizo ya Afisa Elimu na Nurse?
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom