Serikali imejiandaa kuhudumia maabara zinazojengwa?

Sibonike

JF-Expert Member
Dec 23, 2010
16,647
2,000
Kumekuwa na kelele nyingi kuhusu ujenzi wa maabara ulioamriwa na Rais Kikwete. Mwelekeo unaomnyesha kuwa tafsiri ya maabara kwa upande wa serikali ni majengo. Kwanza sipingi wazo la wananchi kuchangia maendeleo yao lakini hili la maabara limekuwa kero kwa wananchi mabao wanalazimishwa kuchangia hadi kuwekwa ndani baadhi ya maeneo.

Lazima tutambue kuwa maabara si majengo pekee. Lazima kuwe na wafanyakazi (sio waalimu), yaani watu (Laboratory Technicians) wa kuendesha hizo maabara. Je hao watu wapo? Hao wanasomeshwa kufanya kazi hizo. Hata katika shule kongwe za serikali ni wachache sana. Swali lingine muhimu ni vifaa na madawa ya kutumia kwenye hizo maabara. Serikali imejiandaa kwa hili? Kwa mfano kwenye maabara za kemia, kunahitajita vitu kama beakers, pippetes, burners pamoja na kemikali kama sulphuric acid nk. Uwepo wa vitu hivi unahitaji Laboratory Technician kuvitumia na kutayarisha na si kazi ya mwalimu wa somo husika. Mwalimu hana utalaamu wa kuchanganya madawa hayo!

Serikali yetu hii itatoa fedha kununua vitu hivyo kama inashindwa kununua madawati? Nina wasiwasi watu watahenyeshwa na mwisho wa siku hizo maabara zitakuwa ni white elephants tu. Kwanza ujenzi wake hauwezi kuwa na sawa na darasa la kawaida. Ni vyumba vyenye design na mahitaji maalumu kabisa. Sina uhakika kama yote haya yamezingatiwa. Inaelekea mheshimiwa alitamka tu kuwa hadi tarehe fulani kila shule iwe na maabara lakini hakuna mwenye ujasiri wa kumweleza kuwa kuna mambo kadhaa ya kuzingatiwa ili kufanikisha malengo hayo. Pia tukumbuke kuwa kila somo la sayansi linahitaji maabara yake. Ya kemia haiwezi kuwa ya fizikia!

Tumeingiza mno siasa kwenye elimu na gharama zake ni kubwa mno kwa taifa letu. Mimi naona maabara zinazojengwa ni nyongeza tu ya madarasa! Ujenzi wa maabara unahitaji serikali ijipange na kutenga fedha za ujenzi, vifaa na madawa na baadaye iendelee kuzihudumia kila mwaka.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom