Serikali imefuta usajili wa magazeti 473, hayakuchapishwa kwa miaka mitatu mfuluizo

Hearten

Member
May 17, 2016
46
54
Habari wakuu,,

Leo Serikali kupitia Wizara ya Habari iliyochini ya Nape Nnauye imesema kuwa imefuta usajili wa magazeti 473 kupitia tangazo lililochapishwa katika gazeti la serikali lenye namba 195, baada ya kutochapishwa kwa miaka mitatu mfululizo.

Magazeti hayo hayataruhusiwa kuchapishwa au kusambazwa kwa njia ya nakala ngumu au kielektroniki, ikiwa Mmiliki wa gazeti lililofutiwa usajili angependa kuendelea na biashara milango iko wazi kwa ajili ya kuwasilisha maombi mapya ya usajili kwa kufuata taratibu zilizopo.

Kwa mujibu wa takwimu za ofisi ya msajili wa magazeti Tanzania inayo magazeti na majarida 881 yaliyosajiliwa kisheria.

 
Serikali imefuta usajili wa magazeti 473 kupitia tangazo lililochapishwa katika gazeti la serikali lenye namba 195, baadab ya kutochapishwa kwa miaka mitatu mfululizo.
Mbona umeandika kama unafukuzwa?kwanini usitujuze kiundani?
 
Mkuu..
siunajua kwasasa ni style/mwendo kasiiii..

mleta habari nae kaipata habarii kimwendo kasiii..lakini bila shaka atajazia nyama muda ukisogea
 
Back
Top Bottom