Serikali imefuta pia adhabu ya 10% inayotozwa na Bodi ya Mikopo kwa wanaochelewa kulipa deni

Abdul Nondo

JF-Expert Member
Oct 28, 2016
515
2,874
Waziri wa Elimu Prof.Joyce Ndalichako leo Bungeni tarehe 4 Mei 2021. Ameiagiza Bodi ya mikopo elimu ya juu kuondoa adhabu ya asilimia 10 ya mkopo inayotozwa na kwa wanafaika wa mikopo elimu ya juu wanaochelewa kulipa mikopo hiyo baada ya miaka miwili kupita tangu kuhitimu kwao chuo.

Kwaniaba ya Ngome ya vijana Act Wazalendo, napenda kuishukuru na kuipongeza serikali kwa maamuzi haya makubwa na ya kupongezwa.

Ngome ya vijana Act Wazalendo tumekuwa mstari wa mbele haswa kusemea changamoto zote kuhusu urejeshaji wa mikopo elimu ya juu.

Mbali na kusemea tozo ya ongezeko wa thamani ya fedha (Value Retention fee 6%) mbayo tayari imefutwa na Mh.Rais Samia.Pia tumekuwa tukishauri na kutaka kufutwa kwa penalti ya 10% inayotozwa mara moja na Bodi ya mikopo kwa wanufaika ambao wamechelewa kulipa mikopo yao miaka 2 tangu kuhitimu kwao.

Tarehe 20/Januari /2021 tuliandikia barua wizara ya elimu yenye kumb Na:ACT/HQ/Vijana/001, nakala tukapeleka Ofisi ya Rais Ikulu,Ofisi ya waziri mkuu na Bodi ya mikopo. Iliyoandikwa na katibu wa Ngome wetu Mwanaisha Mndeme yenye kichwa cha habari SERIKALI KUFANYA MAREJEO NA TATHIMINI MPYA JUU YA VIWANGO NA MASHARTI YA MAREJESHO YA MIKOPO ELIMU YA JUU.

1. Tukishauri na kupendekeza kufutwa kwa Value Retention fee 6% ambayo tayari imefutwa na Mh.Rais.

2. Tukishauri kufutwa kwa Penalti /Adhabu ya 10% ,na hili pia tulilisisitiza juzi tarehe 2 /Mei /2021 katika mkutano wetu wa vyombo vya habari ,Leo hii tar 4 Mei Waziri wa Elimu ametoa maagizo nayo hii Penalti/Adhabu ya 10% ifutwe .

3. Tukishauri Makato ya 15% yarudi 8% au chini ya 8% . Bado halijafanyiwa kazi tunaendelea kuishauri serikali nayo hii ishushwe.

4. Tukishauri kufutwa kwa tozo ya 1% ya kugharamikia shughuli za Bodi (Loan Administration fee).Bado halijafanyiwa kazi tunaendelea kuishauri serikali nayo iondolewe.

Ngome ya vijana Act wazalendo tunaendelea kuishukuru na kuipongeza serikali kwa maamuzi haya,lakini pia tunapongeza jitihada za wabunge wote waliolisemea hili pia Mh.Khatibu Said Khaji wa act wazalendo ,Mh.Ester Matiko na wengine wote,bila kusahau wanaharakati pia ,Azaki , waandishi wa habari na wengine wote.

Ngome ya vijana Act wazalendo tutaendelea kusemea na kupigania maslahi ya vijana na makundi yote nchini bila kuchoka.

Imetolewa na,

Abdul Nondo.

Mwenyekiti wa Ngome ya vijana Act wazalendo Taifa

Tarehe 4,Mei,2021.

IMG_20210504_130112_243.jpg
 
Je, naomba kujua tulio maliza chuo miaka ya 2011 hizi tozo zilizo tolewa zina tuhusu au ina anza na wahitimu wapya?

Naambiwa nadaiwa 16.7Milion wakati mkopo wangu mpaka nilipo maliza mahesabu yanaonyesha ni only 9.3M.. nikauliza hizo addition charges nikaambiwa ni penalty 10% na ile.6% retention fee ya kila.mwaka.

Je, kwa kufutwa huku deni langu litarudi mpaka ile hela halali ya 9.3milion ambayo ndio halisi niliyo ipokea???

Naombeni mnisaidie mlio.elewa maana nilichukia nikaanza kukwepa kwa kuona nimeonewa.
 
Kama hizo tozo ziliwekwa kisheria maana yake zinapaswa kufutwa kisheria.
Je, sheria za huo ufisadi zimefutwa?
Kama bado, safari bado ni ndefu, pambaneni muswada wa kufutwa hizo sheria uletwe bungeni haraka na sio kuja mbio mbio hapa JF kupongeza.
Tamko huanza, mchakato hufuata .Ila ninavyojua Mimi mfano tozo ya kulinda thamani ya fedha Value Retention fee iliyofutwa na Rais haipo kisheria na haina msingi wowote kisheria ilikuwa inatozwa kienyeji
 
Tulio maliza mikopo waturudishie fedha zetu
Waziri wa Elimu Prof.Joyce Ndalichako leo Bungeni tarehe 4 Mei 2021. Ameiagiza Bodi ya mikopo elimu ya juu kuondoa adhabu ya asilimia 10 ya mkopo inayotozwa na kwa wanafaika wa mikopo elimu ya juu wanaochelewa kulipa mikopo hiyo baada ya miaka miwili kupita tangu kuhitimu kwao chuo.

Kwaniaba ya Ngome ya vijana Act Wazalendo, napenda kuishukuru na kuipongeza serikali kwa maamuzi haya makubwa na ya kupongezwa.

Ngome ya vijana Act Wazalendo tumekuwa mstari wa mbele haswa kusemea changamoto zote kuhusu urejeshaji wa mikopo elimu ya juu.

Mbali na kusemea tozo ya ongezeko wa thamani ya fedha (Value Retention fee 6%) mbayo tayari imefutwa na Mh.Rais Samia.Pia tumekuwa tukishauri na kutaka kufutwa kwa penalti ya 10% inayotozwa mara moja na Bodi ya mikopo kwa wanufaika ambao wamechelewa kulipa mikopo yao miaka 2 tangu kuhitimu kwao.

Tarehe 20/Januari /2021 tuliandikia barua wizara ya elimu yenye kumb Na:ACT/HQ/Vijana/001, nakala tukapeleka Ofisi ya Rais Ikulu,Ofisi ya waziri mkuu na Bodi ya mikopo. Iliyoandikwa na katibu wa Ngome wetu Mwanaisha Mndeme yenye kichwa cha habari SERIKALI KUFANYA MAREJEO NA TATHIMINI MPYA JUU YA VIWANGO NA MASHARTI YA MAREJESHO YA MIKOPO ELIMU YA JUU.

1. Tukishauri na kupendekeza kufutwa kwa Value Retention fee 6% ambayo tayari imefutwa na Mh.Rais.

2. Tukishauri kufutwa kwa Penalti /Adhabu ya 10% ,na hili pia tulilisisitiza juzi tarehe 2 /Mei /2021 katika mkutano wetu wa vyombo vya habari ,Leo hii tar 4 Mei Waziri wa Elimu ametoa maagizo nayo hii Penalti/Adhabu ya 10% ifutwe .

3. Tukishauri Makato ya 15% yarudi 8% au chini ya 8% . Bado halijafanyiwa kazi tunaendelea kuishauri serikali nayo hii ishushwe.

4. Tukishauri kufutwa kwa tozo ya 1% ya kugharamikia shughuli za Bodi (Loan Administration fee).Bado halijafanyiwa kazi tunaendelea kuishauri serikali nayo iondolewe.

Ngome ya vijana Act wazalendo tunaendelea kuishukuru na kuipongeza serikali kwa maamuzi haya,lakini pia tunapongeza jitihada za wabunge wote waliolisemea hili pia Mh.Khatibu Said Khaji wa act wazalendo ,Mh.Ester Matiko na wengine wote,bila kusahau wanaharakati pia ,Azaki , waandishi wa habari na wengine wote.

Ngome ya vijana Act wazalendo tutaendelea kusemea na kupigania maslahi ya vijana na makundi yote nchini bila kuchoka.

Imetolewa na,

Abdul Nondo.

Mwenyekiti wa Ngome ya vijana Act wazalendo Taifa

Tarehe 4,Mei,2021.

View attachment 1772955
 
Ni hatua nzuri ila bado kuna ishu kama bodi kukata wanufaika zaidi ya theluthi mbili ya basic salary, na kuwaacha wakiwa na take home ndogo sana. Ninao marafiki zangu wawili hii ishu inawaumiza sana. Abdul Nondo endeleeni kuyasemea haya kwani ilikuwa ni kuwakomoa wakopaji ambao hawana tatizo na ulipaji na pia walisomea kodi za ndugu zao...
 
Je, naomba kujua tulio maliza chuo miaka ya 2011 hizi tozo zilizo tolewa zina tuhusu au ina anza na wahitimu wapya?

Naambiwa nadaiwa 16.7Milion wakati mkopo wangu mpaka nilipo maliza mahesabu yanaonyesha ni only 9.3M.. nikauliza hizo addition charges nikaambiwa ni penalty 10% na ile.6% retention fee ya kila.mwaka.

Je, kwa kufutwa huku deni langu litarudi mpaka ile hela halali ya 9.3milion ambayo ndio halisi niliyo ipokea???

Naombeni mnisaidie mlio.elewa maana nilichukia nikaanza kukwepa kwa kuona nimeonewa.
Hata mi ndilo swali ninalojiuliza, na je wale ambao wameshaanza kulipa tayari,deni lao litapunguzwa katika mfumo upi?
 
Safi sana ngome ya vijana ACT. Hivi ndivyo taasisi na jumuiya za vijana zinavyotakiwa kufanya kwa maslahi ya vijana wa Tz.

UVCCM na BAVICHA igeni mfano huu.
 
Bora mama alivyoondoa ile 6%
Den lilikuwa haliishi kirahisi!, Ulikuwa unajikuta mpaka unamaliza kulipa basi kile ulichokatwa ushasomesha watu hata watatu kwa mgongo wako!
 
CCM bhana! Ni mabingwa wa kutengeneza matatizo, halafu mwisho wa siku wanakuja kuyatatua wao wenyewe!

Sasa unajiuliza, wakati wanapitisha sheria za kipuuzi na za kinyonyaji kama hizo, walikuwa wamelewa! Au!
Pongezi hizi zote ni kwa MAMA SAMI tu, hawo wengine ni kufuata mkumbo tu, kwani angekuwepo meko wala hili lisingewezekana kamwe!!
 
Utekelezaji wa jambo hili kunatoa alama ya mafanikio ya mapambano ya chama cha ACT-Wazalendo.

Hakuna ubishi chama hiki kimekuwa kikipigania suala la ulipaji wa mikopo ya elimu ya juu.

Hongera ACT kwani kuna vyama vikubwa na vikongwe kuliko hiki na bado vinafeli katika harakati zao na vinakosa alama za mafanikio ya muhimu kwa taifa.
 
Waziri wa Elimu Prof.Joyce Ndalichako leo Bungeni tarehe 4 Mei 2021. Ameiagiza Bodi ya mikopo elimu ya juu kuondoa adhabu ya asilimia 10 ya mkopo inayotozwa na kwa wanafaika wa mikopo elimu ya juu wanaochelewa kulipa mikopo hiyo baada ya miaka miwili kupita tangu kuhitimu kwao chuo.

Kwaniaba ya Ngome ya vijana Act Wazalendo, napenda kuishukuru na kuipongeza serikali kwa maamuzi haya makubwa na ya kupongezwa.

Ngome ya vijana Act Wazalendo tumekuwa mstari wa mbele haswa kusemea changamoto zote kuhusu urejeshaji wa mikopo elimu ya juu.

Mbali na kusemea tozo ya ongezeko wa thamani ya fedha (Value Retention fee 6%) mbayo tayari imefutwa na Mh.Rais Samia.Pia tumekuwa tukishauri na kutaka kufutwa kwa penalti ya 10% inayotozwa mara moja na Bodi ya mikopo kwa wanufaika ambao wamechelewa kulipa mikopo yao miaka 2 tangu kuhitimu kwao.

Tarehe 20/Januari /2021 tuliandikia barua wizara ya elimu yenye kumb Na:ACT/HQ/Vijana/001, nakala tukapeleka Ofisi ya Rais Ikulu,Ofisi ya waziri mkuu na Bodi ya mikopo. Iliyoandikwa na katibu wa Ngome wetu Mwanaisha Mndeme yenye kichwa cha habari SERIKALI KUFANYA MAREJEO NA TATHIMINI MPYA JUU YA VIWANGO NA MASHARTI YA MAREJESHO YA MIKOPO ELIMU YA JUU.

1. Tukishauri na kupendekeza kufutwa kwa Value Retention fee 6% ambayo tayari imefutwa na Mh.Rais.

2. Tukishauri kufutwa kwa Penalti /Adhabu ya 10% ,na hili pia tulilisisitiza juzi tarehe 2 /Mei /2021 katika mkutano wetu wa vyombo vya habari ,Leo hii tar 4 Mei Waziri wa Elimu ametoa maagizo nayo hii Penalti/Adhabu ya 10% ifutwe .

3. Tukishauri Makato ya 15% yarudi 8% au chini ya 8% . Bado halijafanyiwa kazi tunaendelea kuishauri serikali nayo hii ishushwe.

4. Tukishauri kufutwa kwa tozo ya 1% ya kugharamikia shughuli za Bodi (Loan Administration fee).Bado halijafanyiwa kazi tunaendelea kuishauri serikali nayo iondolewe.

Ngome ya vijana Act wazalendo tunaendelea kuishukuru na kuipongeza serikali kwa maamuzi haya,lakini pia tunapongeza jitihada za wabunge wote waliolisemea hili pia Mh.Khatibu Said Khaji wa act wazalendo ,Mh.Ester Matiko na wengine wote,bila kusahau wanaharakati pia ,Azaki , waandishi wa habari na wengine wote.

Ngome ya vijana Act wazalendo tutaendelea kusemea na kupigania maslahi ya vijana na makundi yote nchini bila kuchoka.

Imetolewa na,

Abdul Nondo.

Mwenyekiti wa Ngome ya vijana Act wazalendo Taifa

Tarehe 4,Mei,2021.

View attachment 1772955
Hivi wanufaika tuliokuwa tayari tunakatwa tutegemee figure ya deni letu kushushwa kutokana na kuondolewa kwa hizo asilimia 6% na 10%?

Msingi wa swali langu ni kwamba, wakati bodi inapeleka deni la mnfuika kwa mwajiri mwazoni kabisa walijumlisha vyote hivyo.

Yaani walijumlisha retention fee 6% ya mwaka ule na penalty ya 10% kwa mwaka ule wakati deni linapelekwa kwa mwajiri.

Je, na hizo zinaondolewa au zitaondolewa hizi 6% zilizokuwa zinaongezeka kila mwaka bila kuonekana kwenye salary slip?

Wasiposhusha madeni kwa kuondoa kile kiasi kilichoongezwa mwanzoni kilichotokana na hizo 6% za retention na 10% ya penalty bado watakuwa wamewaibia wanufaika
 
Tengeneza tatizo, halafu tatua tatizo ili upate ujiko...

Serikali mwanzo ilifanya kusudi kuweka hayo ma asilimia kwa sababu iliifanya bodi ijiendeshe yenyewe kwa kupitia mgongo wa waliokopeshwa...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom