Serikali imefuta matokeo ya nadharia kwa masomo ya Utabibu Ngazi ya Tano baada ya kubainika kuwa ilivuja

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,802
11,961
Serikali imefuta matokeo ya nadharia (theory) kwa masomo ya program ya Utabibu Ngazi ya Tano (NTA Level 5) baada ya kubainika kuvuja kwa mitihani ya muhula wa pili wa programu hiyo.

======

1.jpg

2.jpg

3.jpg
 

Serikali imefuta matokeo ya nadharia (theory) kwa masomo ya program ya Utabibu Ngazi ya Tano (NTA Level 5) baada ya kubainika kuvuja kwa mitihani ya muhula wa pili wa programu hiyo.

Akitangaza maamuzi hayo jijini Dodoma, leo Novemba 4, Mganga Mkuu wa Serikali, Dk Aifello Sichalwe amesema maamuzi hayo yamefikiwa baada ya uchunguzi wa kamati iliyoundwa kuchunguza viashiria vya uvujifu wa mitihani hiyo iliyofanyika ilifanyika 16 Agosti, 2021 hadi 30 Septemba, 2021.

“Wakati wa uchunguzi wa mitihani iliyovuja, kamati ilibaini kuwa mitihani hiyo ilisambazwa kupitia mitandao ya kijamii (telegram na WhatsApp) na kuonekena kwenye baadhi ya namba za simu za wanafunzi zilizofanyiwa uchunguzi na kamati.

Kupitia sheria ya Baraza Sura 129 na Kanuni za Mitihani, Kifungu 33 (1) (iii), 2004 limefuta matokeo ya mitihani ya nadharia (theory) kwa masomo yote ya Programu ya Utabibu Ngazi ya Tano na baraza limeagiza kurudiwa kwa mitihani hiyo upya ndani ya wiki Sita kuanzia tarehe Novemba 1, 2021.” Amesema Dk Sichalwe.

Mganga Mkuu huyo pia amesema mitihani hiyo itafanyika sambamba na mitihani ya marudio (supplementary Exams) kwa program zingine za afya nchi nzima.

Pia, soma=> Matokeo ya CO mwaka wa pili yashikiliwa NACTE Tanzania nzima
 
Back
Top Bottom