Serikali imefilisika hakuna pesa! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Serikali imefilisika hakuna pesa!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mr.kibulala, Apr 17, 2012.

 1. M

  Mr.kibulala Member

  #1
  Apr 17, 2012
  Joined: Nov 8, 2011
  Messages: 59
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hakika serikali ya CCM inaelekea kuanguka,hali ni mbya sna katika taasisi zake hususani Halmashauri kwani mpaka sasa mwaka wa fedha unakwisha(2011/12) fedha za miradi ya maendeleo kwa wananchi hazijafika ktk halmashauri cha kushangaza halmashauri hzo wameshaanda bajeti ya FY 2012/13 sasa sijui wanatwanga maji kwenye kinu,na cha kuckitisha kuna ofisi nyingi za serikali hakuna karatasi,wino,mafuta,karatasi n.k yaani ni ovyo mazingira magumu.

  ILA JK YUKO BRAZIL
   
 2. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #2
  Apr 17, 2012
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Let us think, I will come back.
   
 3. Watu

  Watu JF-Expert Member

  #3
  Apr 17, 2012
  Joined: May 12, 2008
  Messages: 3,054
  Likes Received: 427
  Trophy Points: 180
  Mliozoea kujichotea hela zetu mtafkufa mwaka huu, ni taratibu tu zimebadilika fedha tele huoni mkuu anazunguka dunia?
   
 4. M

  Magwero JF-Expert Member

  #4
  Apr 17, 2012
  Joined: Oct 28, 2011
  Messages: 243
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 45
  Ni ukweli kabisa ya kuwa SERIKALI YETU ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania yawezakuwa haina fedha za kutosha kuwezesha(finance) hyo miradi ya maendeleo....!
  Tena hilo halina wa kuweza kubisha sana..

  Lakini Siyo SERIKALI YA CCM...
   
 5. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #5
  Apr 17, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,296
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Fedha hamna na deni la serikali linaongezeka from 10 to 14 trillion ie kila mtz anadaiwa 360,000tshs
   
 6. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #6
  Apr 17, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,326
  Likes Received: 1,792
  Trophy Points: 280
  Hawawezi kuacha kutengeneza bajeti...ila tulikua tunaona wapi tunakwenda taratibu na wanasiasa wakawa wanatudharau. Na bado...waendelee kwenda kuvumbua nchi nyingine mpya baada ya ulaya na marekani. Siku wamekuja kutulia hapa kila kitu kwishney.
   
 7. Losambo

  Losambo JF-Expert Member

  #7
  Apr 17, 2012
  Joined: Nov 8, 2011
  Messages: 2,623
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Ni kweli hali ni mbaya hasa ofisi za serikali.
   
 8. Power G

  Power G JF-Expert Member

  #8
  Apr 17, 2012
  Joined: Apr 20, 2011
  Messages: 3,911
  Likes Received: 88
  Trophy Points: 145
  Hapo ndipo naposhindwa kabisa kuelewa dhana za "TRA KUVUNJA REKODI YA MAKUSANYO" na "UCHUMI WETU UNAONGEZEKA KWA KASI" kama tunavyoambiwa na wanasiasa wetu wa ccm kila siku.
   
 9. Ileje

  Ileje JF-Expert Member

  #9
  Apr 17, 2012
  Joined: Dec 20, 2011
  Messages: 3,872
  Likes Received: 1,658
  Trophy Points: 280
  Naishauri serikali ibuni mbinu mpya za kuiwezesha kupata fedha na kuzipangia mipango ya maendeleo! Kimsingi napendekeza serikali ijaribu kufanya yafuatayo:
  1. Serikali iache kabisa kutegemea fedha za wahisani wa nje katika bajeti yake;
  2. Serikali iainishe upya vyanzo vyake vya mapato na kujua kiasi ambacho inaweza kukusanya kwa mwaka;
  3. Mipango yote ya maendeleo ipangwe kutokana na fedha za ndani;
  4. Ziara za viongozi ndani na nje ya nchi zidhibitiwe. Kwa hili serikali itumie zaidi technolojia ya habari kupata taarifa za miradi inayojengwa na pia kuwatumia wawakilishi mbalimbali walio katika maeneo husika.
  5. Serikali ipange miradi michache ya kutekeleza ambayo ina hakika ya kuikamilisha badala ya kuwa na miradi mingi ambayo haitekelezeki kwa wakati;
  6. Kwa sasa serikali iache mara moja kupanga miradi mipya na badala yake ijikite katika kutekeleza miradi ambayo haijakamilika; na
  7. Serikali iangalie uwezekanao wa kupunguza ukubwa wa baraza la mawaziri na badala yake iimarishe idara za utekelezaji.
   
 10. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #10
  Apr 17, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,326
  Likes Received: 1,792
  Trophy Points: 280
  Inawezekana nazo pia ni siasa...maaana biashara matangazo. Tutajuwaje wapo na wanafanya kazi hata kama kazi yenyewe ni sifuri.
   
 11. o

  oyaoya JF-Expert Member

  #11
  Apr 17, 2012
  Joined: Mar 4, 2012
  Messages: 277
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Wakuu,kuna taarifa kuwa walimu wa shule za sekondari walioajiriwa hivi karibuni wameamua kurudi makwao kutokana na halmashauri husika kutokuwa na fungu la kuwalipa mishahara na marupurupu yao mengine. Mfano ni walimu waliopangiwa shule za Chunya mkoani Mbeya.
   
 12. Kombo

  Kombo JF-Expert Member

  #12
  Apr 17, 2012
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 1,819
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Hii ni Ugiriki sasa! Ingawa si vizuri kufanya ulinganisho, hivi iwapo JK angefuta ziara yake ya Brazil na kuamua gharama za ziara ile zikaokoe sekta ya Elimu hasa ajira mpya, angebanduka ngozi?
   
 13. Jethro

  Jethro JF-Expert Member

  #13
  Apr 17, 2012
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 2,223
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 145
  TANZANIA ZAIDI YA UIJUAVYO.

  Shangaaa wafanyakazi wa Halmashauri hizo wanaishi na kusomesha watoto wao na hakuna hata mmoja alisha goma au kuandamana kudai malipo yao ndio TANZANIA hiiiii jamani,

  Wachahche wetu wakidai haki twaaambiwa wanafanya vurugu hizi sera za woga zinatoka wapi tutakuja chanana mapanga humu ndani kila mmoja atakula na adui wake kwa jinsi alivyo muona kama alikuwa upande wa wanyonge au MAFISADISTANI


   
 14. doup

  doup JF-Expert Member

  #14
  Apr 17, 2012
  Joined: Feb 26, 2009
  Messages: 1,172
  Likes Received: 335
  Trophy Points: 180

  anawezekana kuna chembechembe za ukweli ndani yake, kama hakuna inakuwaje jamaa kama mwewe, na terehe ishirini na ngapi sijui anaenda kumzika BINGWA.
   
 15. k

  kilolambwani JF-Expert Member

  #15
  Apr 17, 2012
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 395
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Siyo WALIMU tu hata wataalam wa KILIMO waliopangiwa kuripoti baadhi ya Halmashauri wamerudi majumbani kwao sababu serikali haina pesa za kuwalipa mishahara.
   
 16. TWIZAMALLYA

  TWIZAMALLYA JF-Expert Member

  #16
  Apr 17, 2012
  Joined: Oct 1, 2011
  Messages: 398
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  TERRIBLE,sasa hili ongezeko la deni liko wapi sasa?
   
 17. kookolikoo

  kookolikoo JF-Expert Member

  #17
  Apr 17, 2012
  Joined: Mar 9, 2012
  Messages: 2,537
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  serikali haiwezi kukosa pesa za mishahara kwa wafanyakazi wake ambao majina yao yako hazina kwa vile hulipa mishahara kwanza kabla ya kufanya malipo mengine. hao wapya huenda majina yao hayajapelekwa hazina kwa sababu mbalimbali.
   
 18. mopaozi

  mopaozi JF-Expert Member

  #18
  Apr 17, 2012
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 3,290
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Kelele zenu ni sawa na inzi chooni ambazo hazimpi shida mnyaji!
   
 19. luhala

  luhala JF-Expert Member

  #19
  Apr 17, 2012
  Joined: Feb 25, 2012
  Messages: 412
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hakuna ubishi kabisa kwamba serikali hii ya kisanii na badhirifu haina kabisa hela kwani imeshindwa kuheshimu commitments zake nyingi tu ikiwa ni pamoja na malipo ya pensheni ya wazee wastaafu ambao mara ya mwisho walilipwa January mwaka huu na kwa kadiri ya tangazo lao la awali walipaswa kulipwa baada ya miezi mitatu yaani mwanzoni mwa Aprili hii. Sasa ni zaidi ya nusu mwezi na malipo yameshindikana, serikali imeshindwa hata kuwasiliana nao na haijaeleweka kama mwezi ujao watalipwa au la! La ajabu wanaendelea na ubadhirifu hata wa kidogo kilichobaki. Tanzania ni nchi ya ajabu, serikali inakusanya kodi kwa machinga tu, mapapa yanaachwa na kupewa misamaha isiyo na mantiki yoyote, serikali inawahadaa wananchi wake kwamba eti imevunja rekodi kwa kukusanya kodi! Wakati huo huo Rais anabembea kwenye ndege akifanya safari zisizo na tija yoyote kama mbayuwayu.
   
 20. kukomya

  kukomya JF-Expert Member

  #20
  Apr 17, 2012
  Joined: Sep 20, 2011
  Messages: 344
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 35
  Kama hiyo ni kweli basi ni aibu kubwa kabisa kwa serikali hii ya msanii huyu. Izingatiwe wazee hawa walilitumikia taifa kwa uadilifu na uaminifu mkubwa na si haki hata kidogo kuwanyanyasa kama serikali inavyofanya. Ingefaa sasa wazee hawa waunge mkono harakati za mageuzi zinazoendelea sasa. Binaafsi nitakipigia kura chama chochote (Isipokuwa CCM kwani ahadi zao nyingi huwa ahadi hewa) kitakachoahidi kwa dhati kuli address suala hili la wazee wastaafu kuchakachuliwa haki zao. Naona sasa serikali hii ya CCM inaugua laana iliyotolewa na vikongwe wa iliyokuwa East African Community waliodhulumiwa na serikali hii hii ya wezi, vibaka na mafisadi.
   
Loading...