Serikali imefikia kilele cha uzembe; hata TBC haina bodi ya wakurugenzi!!

Dark City

JF-Expert Member
Oct 18, 2008
16,253
11,598
Bunge latupa taarifa za mashirika ya umma


na Deogratius Temba


KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali Mashirika ya Umma, imekataa kupokea taarifa za mashirika matano ya umma kutokana na kutokuwa na bodi za kuyasimamia.
Imewataka mawaziri wanaohusika na taasisi hizo kujieleza mbele ya kamati sababu za kuchelewa kuteua bodi hadi sasa.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana baada ya kukataa kupokea taarifa ya Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Estarina Kilasi, alisema hawawezi kupokea taarifa na mashirika ambayo hayana bodi ambazo kisheria ndizo zinazowajibika katika utendaji na usimamizi.
“Tumewarudisha hawa wa Mwalimu Nyerere, juzi tuliwarudisha wengine, tutawaandikia mawaziri husika barua waje hapa watueleze ni kwanini hawajateua bodi siku zote hizo,” alisema.
Aliyataja mashirika mengine ambayo hayana bodi kuwa ni Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU), Taasisi ya Ustawi wa Jamii, Veta na Shirika la Tija la Taifa.
Mashirika mengine matatu ambayo taarifa zake zimekataliwa na wahusika wataitwa bungeni ili kutafutiwa muda wa kuzijadili ni Kampuni ya kusimamia mali za lililokuwa Shirika la Reli Tanzania – TRC (RAHCO), Shirika la Utangazaji (TBC) na Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HESLB).
 
Back
Top Bottom