Serikali imefeli 'coursework',itafanyaje 'UE'?

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
6,136
17,871
Wakati wa kusoma kwangu chuo kikuu,majaribio iliitwa Coursework. Mitihani ya Muhula wa kwanza au wa mwisho yaliitwa University Examinations-UE. Kufaulu coursework kulimuwezesha mwanachuo kufanya UE.

Serikali ya awamu ya tano,chini ya Rais Magufuli, inajinadi kama Serikali ya viwanda. Viwanda vinapaswa kupangwa,kujengwa na kusimamia/kuratibiwa. Kwenye sekta ya sukari,Tanzania ina viwanda vinne:TPC Moshi,Kagera Sugar,Mtibwa na Kilombero. Viwanda hivi,katika kuvisimamia,ndiyo ingekuwa Coursework ya Serikali ya viwanda.

Serikali inashindwa kuratibu ipasavyo viwanda hivi vinne. Inafeli Coursework. Itakuwaje UE ya kuwa na nchi ya viwanda?

Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Ruvuma)
 
Na mimi nimebishana na mtu mmoja humu kuhusu hii ishu ya "Tanzania ya viwanda ya Magufuli". Na nimemwambia waziwazi kuwa, unalishwa upepo tena wa vumbi!!

Watu wako madarakani kwa zaidi ya 50yrs plus, wameshindwa kusimamia uzalishaji wa sukari tu yenye kutosheleza soko ingalau la ndani, leo wamelala na wameamka wanawaza na kutuaminisha kwamba in 5yrs to come Tanzania hii itakuwa ya uchumi wa viwanda!!

Lol..... this is total insane!!

Utakuwaje na ndoto za mchana za namna hii bila kwanza kufanya mageuzi makubwa ya kisera na mifumo ya kisiasa na kiuchumi inayoonekana na kueleweka kwa watu!!??

Viwanda gani hivyo vinavyoweza kuja tu kwa kauli za kisiasa za majukwaani?....

I absolutely don't get it na ofcourse nakubaliana na wewe JPM na CCM wameshadunguliwa na CW na obviousily hawana sifa ya kuruhusiwa kuingia kwenye UE!!
 
Wakati wa kusoma kwangu chuo kikuu,majaribio iliitwa Coursework. Mitihani ya Muhula wa kwanza au wa mwisho yaliitwa University Examinations-UE. Kufaulu coursework kulimuwezesha mwanachuo kufanya UE.

Serikali ya awamu ya tano,chini ya Rais Magufuli, inajinadi kama Serikali ya viwanda. Viwanda vinapaswa kupangwa,kujengwa na kusimamia/kuratibiwa. Kwenye sekta ya sukari,Tanzania ina viwanda vinne:TPC Moshi,Kagera Sugar,Mtibwa na Kilombero. Viwanda hivi,katika kuvisimamia,ndiyo ingekuwa Coursework ya Serikali ya viwanda.

Serikali inashindwa kuratibu ipasavyo viwanda hivi vinne. Inafeli Coursework. Itakuwaje UE ya kuwa na nchi ya viwanda?

Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Ruvuma)
mzee tupa, kwanza watuambie wamiliki wa hivi viwanda ni akina nani na walimikikiswa vipi? kuanzia hapo ndo tujipange , vinginevyo hao wanaomzungusha JPM ni wenzake
 
Wee mzee akili yako kwa kweli iko ktk reverse mode, JPM ana mida gani?? Unaongea as if yupo madarakani miaka minne.

Alafu tendea haki UMRI WAKO, elimu yako NA MAONI YAKO, uwe umatoa na ushauri au kitu mbadala cha kufanya unapokosoa kitu kuwa hakiko sawa au haukiungi mkono.
 
Miezi 6 sasa ya utawala wa JPM hakuna hata kiwanda cha ngozi kimoja kilichoongezeka, hii maana yake kwa miaka mitano ijayo kama watajenga viwanda havitazidi 12
 
Wanakubali kushauriwa jibu hili kwanza. The Mabala the farmer .
 
Kama hawakubali kushauriwa, je wanakubali kukosolewa?? Au ni vichwa vibovu kufikiri nje ya boksi, hamna mbadala bali kuponda tu??
 
Miezi 6 sasa ya utawala wa JPM hakuna hata kiwanda cha ngozi kimoja kilichoongezeka, hii maana yake kwa miaka mitano ijayo kama watajenga viwanda havitazidi 12
Kijana kiwanda si kama getto unajenga kwa siku moja, ingekuwa rahisi hivyo chadema wangekuwa wamejenga hata ofisi ya makao makuu yao, ujenzi hasa mkubwa kama wa kiwanda au ofisi za chama huhitaji maandalizi.
 
Wewe mzee usilinganishe chama ambacho hakijawahi kushika madaraka na serikali
 
Kama course work kashindwa kufikisha basi ana technical supplementary ambayo akijipanga vyema anatoboa vizuri tu.
 
Wewe mzee usilinganishe chama ambacho hakijawahi kushika madaraka na serikali
Kumbe nilikua sijui, kumbe CUF walishawahi kushika madaraka ndo maana wamejenga ofisi zao, na nyie jitahidini mshike madaraka mjenge ofisi zenu.
 
Hapa tunazungumzia kujengwa viwanda na Serikali wewe mzee naona unaanza kuzeeka
 
Wee mzee akili yako kwa kweli iko ktk reverse mode, JPM ana mida gani?? Unaongea as if yupo madarakani miaka minne.

Alafu tendea haki UMRI WAKO, elimu yako NA MAONI YAKO, uwe umatoa na ushauri au kitu mbadala cha kufanya unapokosoa kitu kuwa hakiko sawa au haukiungi mkono.
Magufuli ameweza kuliziba pengo la kanumba ipasavyo kwa hilo namsifu
 
Wee mzee akili yako kwa kweli iko ktk reverse mode, JPM ana mida gani?? Unaongea as if yupo madarakani miaka minne.

Alafu tendea haki UMRI WAKO, elimu yako NA MAONI YAKO, uwe umatoa na ushauri au kitu mbadala cha kufanya unapokosoa kitu kuwa hakiko sawa au haukiungi mkono.
Ushauri wa bure....
Leadership is talent, and the man hasn't that talent.
Awaachie wenye vipaji waonyeshe maujuzi.
 
Kuanzisha kiwanda sio kama unataka kununua tecno kariakoo,inahitaji maandalizi na mtaji

Kwenye bajeti yake ya 2016/17, haionyeshi kuwa Yuko serious na suala la viwanda, dangote kiwanda chake kimetumia 1 plus trillion kujenga sasa ngosha kwenye bajeti yake kaweka 96 billions, hii si hela ya kupaka oil mitambo ya kiwanda kimoja
 
Back
Top Bottom