Serikali imeanzisha kampuni zinazoongeza ugumu wa maisha

Njowepo

JF-Expert Member
Feb 26, 2008
9,618
2,120
Wednesday, 12 October 2011 21:03
Fredy Azzah
UMOJA wa Maofisa Watendaji Wakuu wa Kampuni za Biashara nchini umesema serikali imeanza kujiingiza kwenye biashara kwa kasi kwa kuanzisha kampuni zinazoongeza ugumu wa maisha kwa wananchi.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Saalam jana, Mwenyekiti wa umoja huo, Ali Mufuruki alisema serikali imekuwa ikianzisha kwa kasi makampuni hayo ambayo imekuwa ikiyaita mamlaka za udhibiti.

“Haya mashirika yanaongeza ugumu wa maisha kwa wananchi, kwa mfano mafuta yakifika bandarini lita moja inawezwa kuuzwa kwa Sh400 mpaka 500, ikiwekwa kodi ya forodha na nyingine kama hizo inafikia Sh1000,” anasema na kuongeza:

“Yakija haya mashirika mengine yanayoitwa mamlaka mafuta yanafika mpaka Sh2,000 na zaidi, badala ya kuwa wasimamizi yanakuwa chombo kingine cha kukusanya kodi ambayo inakuja kuwa mzigo mzito kwa mlaji,” alisema Mufuruki.

Alisema kuwa, kitendo cha mamlaka hizo za udhibiti kugeuka vyombo vya kukusanya kodi, kimekuwa kikiongeza gharama za uzalishaji na hivyo mzigo wote kwenda kumwangukia mlaji.

Aliongeza kuwa, hali hiyo imekuwa ikifanya mamlaka hizo kuwa na fedha nyingi ambazo zimekuwa haziwanufaishi wananchi kinyume chake zinafanya mamlaka hizo kuwa washindani na wale wanaotakiwa kuwasimamia.

Kwa upande wake, mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Mashirika ya umma, Zitto Kabwe, alisema kwa kiasi kikubwa hali hiyo inatokea kutokana na serikali kuanzisha mashirika hayo bila kuyapa mtaji.
Zitto ambaye alikuwa mzungumza katika mkutano huo, alisema mashirika hayo siyo tu kuwa yanakuwa yanakusanya kodi nyingi, bali fedha hizo ambazo ni za walipa kodi, hazina usimamizi mzuri.

Alisema kuwa, kwa sasa kuna mashirika 238 ya serikali ambayo kwa ujumla wake serikali imewekeza zaidi ya Sh10.3 trilioni. “Mashirika haya yamekuwa yakitoa gawio kubwa sana kwa serikali, lakini mengi ya haya mashirika ambayo yamekuwa yakianzishwa yamekuwa hayana usimamizi mzuri wa hizi hela za walipa kodi,” alisema Zitto.

Kwa mujibu wa Zitto, shughuli zinazofanywa na mashirika hayo, zinatakiwa ziwekwe bayana na kuwa matumizi ya fedha zake yasimamiwe kikamilifu.

Alitolea mfano moja ya mamlaka ambayo kutokana na kuwa na fedha nyingi zisizokuwa na usimamizi, waliamua kubadilisha fedha wanazowalipa maofisa wake wanaosafiri nje ya nchi kutoka Dola420 za Marekani kwa siku na kufanya iwe Euro420 kwa siku.
 

Papa D

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
753
182
I concur with Mufuruki!
Hizo taasisi zisitoze ada ya aina yeyote. Ada zote zipelekwe TRA. Na endapo wanatokea kutoa adhabu ya malipo ya fedha then wasipokee fedha badala yake hizo fedha ziende kusajiliwa mahakami. Fedha ya uendeshaji kwa hayo mashirika itoke hazina. Kwa kufanya hivyo kutapunguza gharama za uzalishaji pia kuimarisha mfumo wa kumbukumbu za serikali!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom