Serikali imeanza kuhakiki mkataba wa bandari ya Bagamoyo

Yaani nyie watu mna matatizo sana!!! Yaani mnataka alichosema JPM kisikosolewe na ukimkosoa basi una chuki nae!!!

Anyway, mimi ni miongoni mwa hao watu tunaoambiwa TUNA CHUKI na Marehemu kwa sababu tu huwa napenda kuweka kumbukumbu sawa!!

The Hater Pro narudia tena hapa...

Popote pale duniani kodi ni Mali ya Serikali kwahiyo mambo ya kutokusanya kodi SIO YA KWELI...

Hata hivyo, ni kweli zipo BAADHI ya kodi zinazoweza KUSAMEHEWA kwa mujibu wa sheria zetu wenyewe!!! On top of that, binafsi nilihusika kwenye research kuhusu Belt and Road Initiative (BRI) iliyoasisiwa na China!! BRI ndiyo imezaa miradi kadhaa ya Uchina sehemu mbalimbali duniani!

Wapinzani wakubwa wa BRI ilikuwa Serikali ya Trump ambayo iliwaaminisha hadi Wamarekani wenyewe kuhusu ni namna gani BRI inavyoandaa MSIBA kwa nchi maskini! Propaganda walizokuwa wanasambaza ni pamoja na:-

1. Hizo Bandari zinazojengwa na China ni Mtego wa Madeni, na hivi sasa China wameipokonya Sri Lanka bandari yake baada ya Sri Lanka kushindwa kulipa madeni

2. Uchina inataka kuweka vituo vya kijeshi na hivyo usalama wa mataifa ya Afrika yapo hatarini kiusalama!

Media kadhaa za USA zikawa ndo wasambazaji wakubwa wa hizo propaganda!!

Baadae Wasomi wa huko huko Marekani wakashtuka na kujiuliza kama hii BRI ni mbaya kiasi hicho mbona mataifa kadhaa yanajiunga! Ili kupata majibu, ndipo baadhi ya taasisi ikiwamo Harvard University ikatuma wasomi wao kufanya research!! Kwenye hizo researches, ndipo nami nikabahatika kuwa "mbeba mikoba" wa Researcher Mmoja wapo kwa sababu yeye Case Study yake ilikuwa Bagamoyo Port Project, Hambantota Port (Maarufu kama Bandari ya Sri Lanka), pamoja na Piraeus Port ya Ugiriki!

Researcher wangu huyu, pamoja na wale wa Harvard University wakagundua yafuatayo kama yalivyokuwa summarized kwenye Abstract ambayo inapatika kwenye website ya Harvard University!

View attachment 2086214
Binafsi nina full report sema sijapata muda wa kui-summarize na kuileta JF. Na utaona hapo juu Researchers ni pamoja na Deborah Brautigam and Meg Rithmire. Google mwenyewe hayo majina upate CV zao!!

Baada ya miezi kadhaa kupita tangu kukamilika kwa Research ya Bagamoyo, nikaona stori za kwamba hatukusanyi kodi zimekuwa nyingi mno! Ikabidi nimtumie email yule researcher niliyekuwa nae ili anifafanulie hili suala kwa sababu kwa sababu kwavile mwenzangu ni Mzungu, yeye aliweza kuongea na watu wa ndani zaidi.

Jibu ambalo alinirudishia, pamoja na mambo mengine ni hili hapa chini...

View attachment 2086237
Kwenye posts zangu za nyuma nishaandika sana kuhusu kama kodi itachukuliwa na serikali, sasa hao China watarudisha vipi pesa zao! Pamoja na njia nyingine za kurudisha, kama alivyosema Mwamba hapo juu, China, like many other businesses huwa WANAOMBA WASAMEHEWE INCOME TAX.

Narudia... WANAOMBA>>>> INCOME TAX! Income Tax ni sehemu tu ya Kodi zinazokusanywa bandarini! Ukisikia watu wanalalamika kwamba Kodi Bandarini inaumiza sana basi kodi hiyo wala sio Income Tax bali Excise Duty, Import Tax na VAT ambazo ZINAENDA serikalini!!

Hii Income Tax ambayo huwa wanaomba wasamehewe ni ipi?!

Kwa mfano, pale bandarini meli zitakuwa zinatia nanga, na watalipia USHURU (sio Kodi) wa wao kutia nanga bandarini! Kuna wengine watachelewa kuchukua au kusafirisha mizigo yao na kwahiyo itabidi ihifadhiwe hapo bandarini! Ni Wachina ndio watakaofanya kazi za KUPAKI NA KUPAKUA mizigo kwenye meli!!!

Sasa shughulizi zote nilizotaja hapo juu, na zingine kama hizo, zitakuwa zinawapatia Wachina Mapato a.k.a INCOME!! Kwa sheria zetu, Mchina atatakiwa kulipa Income Tax kutoka kwenye mapato anayoingiza kupitia hizo shughuli hapo juu!! Sasa basi, Wachina ndo huwa wana kawaida ya KUOMBA kusamehewa hiyo Income Tax! Kwamba, wakishusha na kupakia kontena kwenye meli, basi ile pesa watakayolipwa kwa hiyo huduma wanataka wachukue yote badala ya kulipia kodi!!

Kinyume chake, wewe ukiingiza let's kontena 100 kwenye bandari, KODI ZOTE utazilipa TRA kwa sababu ni MALI YA SERIKALI!!

JF Ina watu wengi sana tunafanya kazi sehemu mbalimbali na usiongee kitu kama hujui tafadhali. Wengine wapo kwa AG wengine ni wanasheria wa makampuni binafsi hivyo huwa tunapata access ya hizi documents Ila hatuwezi kuongelea kila kipengele. Wanaojua wamekaa kimya maana mlishaamua kuongea Ila mradi itajengwa tu.

Kimsingi, mkataba upo stage ya negotiation na hizo ni proposed clauses za wachina na kiufupi Ila draft contract Ina page zaidi ya 1000 kijana usiandike kitu hujui.

Pia fahamu kwamba hizo propositions ni kawaida kwa mfanyabiashara maana hajaja kutangaza dini hapa kwetu yeye anatumia hela apate faida so mianya kama hii akipenya anajua ana uhakika wa kumaximize profit.

Wao walitaka mambo mengi mno nashindwa hata kuelezea ikiwemo suala la tax holiday sio wasilipe Kodi acha kudanganya. Hata hiyo ilishakataliwa wakati wa majadiliano sababu hata kisheria tax holiday ilishafutwa.

Walitaka pia kuwa na port charges zao kitu ambacho kilikataliwa kwakuwa Bandari zote nchini wanatumia tarrif rate moja tu za kwenye bahari kuna tarrif zake na maziwa Wana tarrif zao.

Pia walitaka Bandari nyingine isijengwe kuanzia pangani hadi Mtwara ili waweze kurudisha pesa yao kwa wakati uliopangwa kwa kuwa Ile Bandari tumeingia concession agreement kwa miaka 33 na ikiisha wanatuachia ingali bado watakuwa wanatupatia gawio kwa kuwa tunaform kampuni yetu itakayoingia ubia katika uendeshaji wa Ile Bandari hivyo tutagawana mapato kulingana na share capital tuliyoinject.

Haya mengine hayapo ni wazimu wa Magufuli tu hii nakueleza mie sipendi tudanganye sana kuhusu huu mradi maana kila mtu anakaza shingo sana tunasahau huu mradi utaajiri watu zaidi ya 12,000 direct employment na watu zaidi ya 200,0000 watapata indirect employment kwa kuajiriwa kwenye mahoteli yatakayojengwa kule ili watu wanaotoa mizigo wapate malazi, chakula transportation nk.

Mradi utaunga na kuzindua special economic zone (SEZ) ambayo Kuna eneo limetengwa la viwanda kwa sababu ya Ile Bandari itakuwa free port. Tafuta maana ya free port sio kwamba hulipi.

Kuna airstrip itajengwa, reli itajengwa kuiunganisha Bandari na reli ya Kati pamoja na Tazara hivi kwa nini mnapinga huu mradi????????? Hawa watu wana shida gani? Kisa Magufuli aliukataa??? Yule alikuwa na ishu zake ndio maana aliuchafua na wajinga wanamuona kama Mungu.

Magufuli aliukataa sababu kwenye kutengeneza kampuni inabidi serikali itoe hela kama share capital ili tuchangie sababu wao walitaka waendeshe wenyewe sisi tukasema hapana tukisubiri Kodi pekee siku tukikabidhiwa huu mradi tutashindwabsababu tutakuwa hatujajiweka tayari kuendesha so tukaamua iwe formed kampuni ili tuweke watu wetu nao waingie kwenye management.

Magufuli aliona pesa inayotakiwa ni nyingi akaamua kutoa visingizio vya kijinga sana na alikataa alisema sisi tuna ardhi kwa nini tutoe hela

Sasa ndugu zangu hata kama una ardhi ukitaka kukodisha hakuna shida Ila ukitaka na kuingia ubia upate gawio lazima utoe pesa otherwise subiri Kodi ya pango.

Mambo ni mengi sana Ila kuna watu tunaufahamu vizuri huo mchezo wa hapo sehemu.
 
Hela uliyowapiga wachina uje kutetea bandari yao hapa ni bora uwarudishie tu maana hakuna unachofanya.

Ujinga mtupu
 
Kimsingi, mkataba upo stage ya negotiation na hizo ni proposed clauses za wachina na kiufupi Ila draft contract Ina page zaidi ya 1000 kijana usiandike kitu hujui.
Unaposema "proposed clauses" ndiyo hiyo niliyoita/ inayoitwa Framework Agreement... huu sio mkataba!

Kwamba "Hizo ndo proposed clauses" unatakiwa kutaja ni zipi!!

Mimi nimezungumzia KODI, na nime-specify aina ya kodi ambazo Wachina and any other businesses huwa wanaomba kusamehewa lakini SIO KODI ZOTE... HAKUNA KITU KAMA HICHO!
Pia fahamu kwamba hizo propositions ni kawaida kwa mfanyabiashara maana hajaja kutangaza dini hapa kwetu yeye anatumia hela apate faida so mianya kama hii akipenya anajua ana uhakika wa kumaximize profit.
Sasa si ndicho nilichosema, au?
Wao walitaka mambo mengi mno nashindwa hata kuelezea ikiwemo suala la tax holiday sio wasilipe Kodi acha kudanganya. Hata hiyo ilishakataliwa wakati wa majadiliano sababu hata kisheria tax holiday ilishafutwa.
Hivi ulikuwa unanijibu mimi, au?!

Nimesema wasilipe kodi au nimesema Wachina kama ilivyo kwa other businesses, WANA KAWAIDA ya kuomba Msamaha wa Income Tax? Na suala lingine la kodi, nikasema kuna kodi zingine hadi kesho huwa tunasamehe kwa sheria zetu wenyewe!
Walitaka pia kuwa na port charges zao kitu ambacho kilikataliwa kwakuwa Bandari zote nchini wanatumia tarrif rate moja tu za kwenye bahari kuna tarrif zake na maziwa Wana tarrif zao.
Nimezungumzia masuala ya kodi na sio charges!!

Hata hivyo, hivi sasa kuwa na rate moja haiwezi kuwa hoja ya msingi kwa sababu as of now, operator ni mmoja! A moment tukishataka kuwa na multiple operator, hatuwezi tena kuwabana kuhusu same charges kwa sababu hapo inakuwa ni biashara huru!
Pia walitaka Bandari nyingine isijengwe kuanzia pangani hadi Mtwara ili waweze kurudisha pesa yao kwa wakati uliopangwa kwa kuwa Ile Bandari tumeingia concession agreement kwa miaka 33 na ikiisha wanatuachia ingali bado watakuwa wanatupatia gawio kwa kuwa tunaform kampuni yetu itakayoingia ubia katika uendeshaji wa Ile Bandari hivyo tutagawana mapato kulingana na share capital tuliyoinject.
Halafu hivi tangu taifa lipate uhuru miaka zaidi ya miaka 60 iliyopita, TZ tumewahi kujenga bandari ipi?! As far as I know, hata bandari tulizokuta zingine zimeshakufa na zingine zinapumulia mashine lakini leo hii suala hili linaongewa sana... all in all, it's just a proposal, na hakuna mjinga anayeweza kusema we'd accept all proposals!

Only the dead can do that!
Haya mengine hayapo ni wazimu wa Magufuli tu hii nakueleza mie sipendi tudanganye sana kuhusu huu mradi maana kila mtu anakaza shingo sana tunasahau huu mradi utaajiri watu zaidi ya 12,000 direct employment na watu zaidi ya 200,0000 watapata indirect employment kwa kuajiriwa kwenye mahoteli yatakayojengwa kule ili watu wanaotoa mizigo wapate malazi, chakula transportation nk.
Na kwa mchumi hayo ndo ya msingi zaidi kuliko hoja nyingi ambazo zimekuwa zikitolewa kama vile ardhi wakati tayari kuna watu wamemilikishwa ardhi kwa miaka 99 wakati tija kwa taifa toka kwenye ardhi husika hakuna!
Mradi utaunga na kuzindua special economic zone (SEZ) ambayo Kuna eneo limetengwa la viwanda kwa sababu ya Ile Bandari itakuwa free port. Tafuta maana ya free port sio kwamba hulipi.

Kuna airstrip itajengwa, reli itajengwa kuiunganisha Bandari na reli ya Kati pamoja na Tazara hivi kwa nini mnapinga huu mradi????????? Hawa watu wana shida gani? Kisa Magufuli aliukataa??? Yule alikuwa na ishu zake ndio maana aliuchafua na wajinga wanamuona kama Mungu.
Yote hayo nishaeleza sana huko nyuma ndo maana nikahoji hivi unaniuliza mimi, au?!
Magufuli aliukataa sababu kwenye kutengeneza kampuni inabidi serikali itoe hela kama share capital ili tuchangie sababu wao walitaka waendeshe wenyewe sisi tukasema hapana tukisubiri Kodi pekee siku tukikabidhiwa huu mradi tutashindwabsababu tutakuwa hatujajiweka tayari kuendesha so tukaamua iwe formed kampuni ili tuweke watu wetu nao waingie kwenye management.
Magufuli aliona pesa inayotakiwa ni nyingi akaamua kutoa visingizio vya kijinga sana na alikataa alisema sisi tuna ardhi kwa nini tutoe hela
Hivyo ni visingizio vyake tu.. hivi unadhani Bagamoyo ingekuwa ndo Chato hayo ya share capital yangetokea?! Tatizo lingine la Magu ndo ile ya kutaka kujifanya yeye tu ndio msafi lakini wenzake wote ni wezi!

Matokeo yake, ndo kama ilivyokuwa SGR! Mwanzoni kawapiga chini Wachina, watu wakashangilia kwelikweli! Sie wengine tukasema wazi hapa Mturuki HANA pesa iliyo available kwa mradi mkubwa kama huu, na hasara yake ni kwamba mradi unaweza ku-delay!

What happened... baadae tukarudi kwa Mchina yule yule ambae plan ya mwanza ilikuwa ni more strategic kwa sababu a huge SGR Investment ingekuwa utilized na bandari! Leo hii sijui tunaratajia kui-utilize na nini!
 
Gazeti la Mwananchi toleo la leo limekuja na habari kuwa serikali ya Rais Samia imeanza kupitia upya na kuhakiki mkataba wa ujenzi wa bandari ya Bagamoyo uliotiliwa shaka na hayati Magufuli kuwa una mashariti magumu yanayolenga kuuwa taifa kiuchumi na ni kichaa tu anayeweza kusaini na kukubaliana na mashariti hayo.

Ikumbukwe waziri aliyetumbuliwa bwana Geofrey Mwambe alikanusha kuwa hakuna mkataba wowote wa bandari ya Bagamoyo na kwamba Magufuli alipotoshwa.

My take: Serikali inahakiki mkataba upi tena wakati haujawahi kuwepo?

View attachment 2084598
Mkataba upi tena jamani? si kuna mheshimiwa alisema hapakuwa hata na mkataba?!!!
 
Nyinyi wasomi mnazinguka mwisho wa siku ndo mnasaini vitu vya ajabu! Hivi tangia lini sehemu inawekwa jiwe la msingi alafu kusiwe na mkataba uliosainiwa? Polepole alimuomya Waziri Mwambe kipindi kile cha Shule ya Uongozi, alimweleza kuwa usipotoshe watu, haiwezekani mkurugenzi wa ile kampuni ya China atoke China aje mpaka Bagamoyo, atoke yule mwarabu Dubai aje mmpaka Bagamoyo alafu atoke Kikwete Magogoni aende mpaka Bagamoyo ajashike lile chepe wachanganye ule udongo pale alafu kusiwe ata na Mkataba? Ni uongo mtupu
Kuna jambo unataka kupotosha kwa makusudi au kutofahamu kulingana na huyo mwandishi alivyoandika hiyo heading ilimradi hatujasoma maudhui yanasemaje.

Waziri aliposema haijawahi kuwepo mkataba ni kweli kwa kuwa ili isemekane Kuna mkataba basi lazima uwe na zile sifa za kuwa mkataba ikiwemo kusainiwa na pande zote .

Ukiangalia hayo ndipo unajiuliza kwani kilikuwa na mkataba kwenye Bagamoyo port project? Jibu ni HAPANA sababu hakukuwepo utiaji wa saini yale makubaliano na hayakufikia tamati ndipo yalikatishwa kuendelea kutokana na sababu ambazo hata Waziri alishindwa kuelewa maana mambo yaliyokuja kusemwa hayakuwepo hata kwenye rasimu (draft) .

Sasa kwa sababu ilitokea sintofahamu na tayari muda umepita ni utaratibu wa kawaida kabisa kuupitia upya huo mkataba kabla ya kusaini au kuendelea na majadiliano ili kubaini kama kuna lolote lipo kinyume na yaliyotarajiwa .

Hata ingekuwa wewe ukiipewa huo mkataba utasaini bila hata kufanya mapitio?
(Vetting).

Mikataba yote ya serikali inayozidi cost ya 600 million hufanyiwa vetting kwa Attorney General na wakisharidhika ndipo hurudisha either mrekebishe au wakiona upo sawa basi wanashauri muendelee na taratibu nyingine.

So to me naona ni Jambo la kawaida na hakuna haja ya kuwa na wasiwasi au speculation zenye kuleta taharuki zisizo na msingi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unaposema "proposed clauses" ndiyo hiyo niliyoita/ inayoitwa Framework Agreement... huu sio mkataba!

Kwamba "Hizo ndo proposed clauses" unatakiwa kutaja ni zipi!!

Mimi nimezungumzia KODI, na nime-specify aina ya kodi ambazo Wachina and any other businesses huwa wanaomba kusamehewa lakini SIO KODI ZOTE... HAKUNA KITU KAMA HICHO!

Sasa si ndicho nilichosema, au?

Hivi ulikuwa unanijibu mimi, au?!

Nimesema wasilipe kodi au nimesema Wachina kama ilivyo kwa other businesses, WANA KAWAIDA ya kuomba Msamaha wa Income Tax? Na suala lingine la kodi, nikasema kuna kodi zingine hadi kesho huwa tunasamehe kwa sheria zetu wenyewe!

Nimezungumzia masuala ya kodi na sio charges!!

Hata hivyo, hivi sasa kuwa na rate moja haiwezi kuwa hoja ya msingi kwa sababu as of now, operator ni mmoja! A moment tukishataka kuwa na multiple operator, hatuwezi tena kuwabana kuhusu same charges kwa sababu hapo inakuwa ni biashara huru!

Halafu hivi tangu taifa lipate uhuru miaka zaidi ya miaka 60 iliyopita, TZ tumewahi kujenga bandari ipi?! As far as I know, hata bandari tulizokuta zingine zimeshakufa na zingine zinapumulia mashine lakini leo hii suala hili linaongewa sana... all in all, it's just a proposal, na hakuna mjinga anayeweza kusema we'd accept all proposals!

Only the dead can do that!

Na kwa mchumi hayo ndo ya msingi zaidi kuliko hoja nyingi ambazo zimekuwa zikitolewa kama vile ardhi wakati tayari kuna watu wamemilikishwa ardhi kwa miaka 99 wakati tija kwa taifa toka kwenye ardhi husika hakuna!

Yote hayo nishaeleza sana huko nyuma ndo maana nikahoji hivi unaniuliza mimi, au?!

Hivyo ni visingizio vyake tu.. hivi unadhani Bagamoyo ingekuwa ndo Chato hayo ya share capital yangetokea?! Tatizo lingine la Magu ndo ile ya kutaka kujifanya yeye tu ndio msafi lakini wenzake wote ni wezi!

Matokeo yake, ndo kama ilivyokuwa SGR! Mwanzoni kawapiga chini Wachina, watu wakashangilia kwelikweli! Sie wengine tukasema wazi hapa Mturuki HANA pesa iliyo available kwa mradi mkubwa kama huu, na hasara yake ni kwamba mradi unaweza ku-delay!

What happened... baadae tukarudi kwa Mchina yule yule ambae plan ya mwanza ilikuwa ni more strategic kwa sababu a huge SGR Investment ingekuwa utilized na bandari! Leo hii sijui tunaratajia kui-utilize na nini!
Mchina anajenga Isaka - Mwanza na Mturuki anajenga Dar - Tabora
 
Huyu mama tangu aseme wale kwa urefu wa kamba zao simwamini tena, labda kama alikuwa anamaanisha kitu kingine na sio ninachofikiria
Kama umefungiwa kamba ya mita mbili kuzungukia chumbani mwako tu, acha wenzio waliofungwa na kamba za kilomita elfu na mia tano watakula shamba lota toka dar mpaka Bukoba na kuzungukia nchi nzima. Il kamba ya mama mwenyewe ndiyo hatujui ina urefu gani.
 
Ile djibout sio cormercial base Ni navy base from get go,. Tena sasa base ya mchina iko umbali wa mita chache kutoka base ya marekani,,, serikali ya Djibouti iliamua kuwakubalia wote, na US hakua na la kufanya zaidi ya kuanza propaganda chafu
Djibouti ni military strategic area, kikosi cha marekani Africom ndo kina makao yake djibout,
Kwa maana kuwa ndo centre ya US ya military command in Africa
Commercial base ndiyo nini?
 
Back
Top Bottom