Serikali imeanza kuhakiki mkataba wa bandari ya Bagamoyo

Kijogoodi

JF-Expert Member
Mar 29, 2021
985
1,000
Gazeti la Mwananchi toleo la leo limekuja na habari kuwa serikali ya Rais Samia imeanza kupitia upya na kuhakiki mkataba wa ujenzi wa bandari ya Bagamoyo uliotiliwa shaka na hayati Magufuli kuwa una mashariti magumu yanayolenga kuuwa taifa kiuchumi na ni kichaa tu anayeweza kusaini na kukubaliana na mashariti hayo.

Ikumbukwe waziri aliyetumbuliwa bwana Geofrey Mwambe alikanusha kuwa hakuna mkataba wowote wa bandari ya Bagamoyo na kwamba Magufuli alipotoshwa.

My take:
Serikali inahakiki mkataba upi tena wakati haujawahi kuwepo?

20220117_095427.jpg
 

ngalanga

JF-Expert Member
Jul 29, 2015
1,727
2,000
Nilimwona wakati akihojiwa na kipindi kinachorushwa na ITV maarufu kama "HOJA MEZANI" jamaa anajikanyagakanyaga utadhani tapeli vile
Waziri Mwambe asiishie kutumbuliwa uwaziri tu avuliwe mpaka ubunge. Nchi haiwezi kuongozwa na mtu muongo na tapeli
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom