The Evil Genius
JF-Expert Member
- Mar 21, 2014
- 5,433
- 17,070
Serikali ya Tanzania imeahidi shirika la fedha Duniani la IMF kwamba itaanza kutoa takwimu za vifo na maambukizi mapya ya ugonjwa wa covid 19 kila wiki kuanzia mwishoni mwa mwezi Septemba 2021 kama masharti mojawapo ya kupewa mkopo.
Serikali iliomba mkopo wa zaidi ya Dollar Milioni 500 za Marekani ama zaidi ya Trilioni 1.3 za Kitanzania ili kukabiliana na athari za ujonjwa wa Covid 19.
Mojawapo ya sababu kubwa ya kuomba mkopo huo pia ni kwa ajili ya kununulia vifaa tiba, chanjo, vipimo na vitu vinavyofanana na hivyo.