RUCCI
JF-Expert Member
- Oct 6, 2011
- 1,701
- 1,714
Matangazo ya bunge kwa sasa siyo "Free to air program", ni "pay program", ili uweze kuona mjadala wa bunge lazima mfukoni mwako uwe sawasawa, nikimaanisha ili uone mjadala wa bunge utalazimika kununua king'amuzi cha continental ama Azam, huko kupitia channel zao za "Star Bunge" ama "Azam Extra" ndiyo utaweza kuona vikao vya bunge, baada ya TBC ambayo ni "free to air TV" kuacha kurusha matangazo ya bunge kwa sehemu ya mjadala na kurusha maswali na majibu pekee.
Siku zote mfumo wa kibeberu hauna undungu na masikini,masikini wa Tanzania sasa itabidi wasubiri mpaka saa nne usiku ili wajue mjadala wa bunge ulikuwaje? TBC inaendeshwa kwa senti za watanzania wote ndito maana ni "free to air station".
Kuwa masikini ni hatari sana,utakosa hata haki ya kujua nini kinaendelea!hakuna atakayekuheshimu wala kukutahmini,.serikali inataka kwa makusudi kuwanyima watu masikini haki ya kujua wabunge wao wamechangia nini? Tangazo la serikali kupitia Nape,linasema mambo muhimu tu yaliyojadiliwa bunge yataoneshwa kuanzia saa nne mpaka tano usiku! Kuipata channel ya "Azam Extra" ni lazima ununue king'amuzi cha Azam na uwe na shilingi elfu 12 kila mwezi, kupata channel ya Star Bunge lazima ununue king'amuzi cha Continental.
Kwa wale wenzangu na mimi mnaotumia cable, hamtakuwa na fursa tena ya kuona mjadala bungeni, ili uone bunge sharti ni kuwa na ving'amuzi viwili, cha Azam ama continental, Na huko lazima ulipie kwa upande wa Azam Extra!.
Serikali ijifikiri upya na uamuzi wake huu, watanzania wa sasa wanapenda sana kufuatilia masuala muhimu ya nchi, kuwanyima haki ya kuona bunge kupitia "free to air TV"sidhani kama itakuwa na afya kwa sasa na kwa watanzania wa sasa..