Serikali iliwapiga changa la macho wastaafu nchini kwa kuongeza pension kwa 100%

Retina

JF-Expert Member
Mar 6, 2015
1,039
1,163
Unaweza usiamini,kumbe ni kweli huku waziri Saada,Mwigulu na Malima walipouhakikishia umma kwa madaha kuwa kwenye budget ya mwaka 2015/16 wangewaongezea pension ya mwez wastaafu wote waliotumikia taifa hili kwa moyo wao wote kwa 100%·Lakini mpaka leo hakuna badiliko serikali ya ccm ilifanya hivyo ili kuomba kura toka kwa wastaafu hao ambao wanaishi kwa shida kutokana na ukali wa maisha.Tofauti hayo malipo hayo hususan yanayopitia mfuko wa pspf yamekuwa yakichelewa kuwafikia walengwa bila sababu kutolewa na serikali au mfuko husika.Pia badiliko la pension kwa wastafu kutoonekana kuamzia mwez wa fedha ulipoanza yaani mwezi julai 2015 halijawahi kutolewa maelezo yeyote na serikali kupitia hazina au mifuko yenyewe au wazir wa wizara husika.Haya ni mateso vs maumivu,uongo wa serikali ya ccm inayojiita ni serikali sikivu kumbe ni katili kwa wananchi wake.Hakuna haja ya kuweka akiba kwenye mifuko ni bora mtumishi ale chake ajue moja,inakera sana.Hii movement kwa wastaafu ni endelevu mpaka pale wastaafu watakaposikilizwa kilio chao.
 
Kustaafu kwenye nchi yetu ni shida..Nawaonea sana huruma wazee waliotoa jasho lao Katika utumishi kisha kunyanyaswa kwenye kupata mafao yao stahiki..Hivi hakuna wa kuyabana haya mashirika ya pensheni??? Mbona kama yote yana matatizo ???
 
Kustaafu kwenye nchi yetu ni shida..Nawaonea sana huruma wazee waliotoa jasho lao Katika utumishi kisha kunyanyaswa kwenye kupata mafao yao stahiki..Hivi hakuna wa kuyabana haya mashirika ya pensheni??? Mbona kama yote yana matatizo ???
Sasa kama hela za haya Mashirika zilitumika kuhakikisha chama tawala kinashinda uchaguzi unategemea nini hapo?
 
Hakuna ninalotegemea..nataka mwongozo uwepo.Haya mashirika yamekuwa yakijiendesha kwa ukiritimba wa hali ya juu.Sera zao za Uwekezaji ziwe wazi na sheria ya kuwalinda wanachama iwe na meno.Afu si alisema JPM hana ubia na mfanyabiashara ,taasisi au shirika lolote ???? Sasa pesa za mafao ukafanyie kampeni si jipu hilo.Tumpe muda tuone...
 
Kustaafu kwenye nchi yetu ni shida..Nawaonea sana huruma wazee waliotoa jasho lao Katika utumishi kisha kunyanyaswa kwenye kupata mafao yao stahiki..Hivi hakuna wa kuyabana haya mashirika ya pensheni??? Mbona kama yote yana matatizo ???
Usiseme unawaonea huruma kwani wafanyakazi wote ni wazee wastaafu watarajiwa. Wote itatukumba siku moja. Yaani hatari sana!!!!!
 
Kwa sasa lzma niwaonee huruma..yaani unakuta mzee wa watu kutwa na makabrasha yake anazungushwa tu kwenye maofisi.I feel for them.Kuhusu mimi imenibidi niliangalie hili swala upya na kujipanga ili niandae mazingira ya kuepukana na adha hii,kikubwa ni kuweka akiba binafsi na kuwekeza katika miradi ya muda mrefu mf.Hisa DSE,kilimo cha miti n.k
Cc Nguto
 
lipumba alishasema bajeti ya 2015/16 ni jipu lililokaa sehemu za.siri
 
Ni jukumu lako kujiandalia maisha baada ya kustaafu. Usitegemee serikali ije ikulee ukiwa umezeeka na hujiwezi. Na tunakokwenda hali itakuwa ngumu zaidi kwale wanaotegemea malezi kutoka serikalini baada ya kustaafu. Sheria nyingi zitabadilishwa na mzigo huo ataubeba mwajiriwa mwenyewe.
 
Back
Top Bottom