Serikali ilivyotekeleza Maazimio ya Bunge Richmond-Pinda.

Tunasubili JK awastaafishe kwa manufaa ya umma utasikia tu na si kuwafukuza kazi mimi nipo.
 
"WAKIENDELEA KUTUZUGA TUTAANIKA HATA USHAHIDI WA YULE MWANASHERIA ALIYEKWENDA KUBEBA MZIGO WA MZEE NJE YA NCHI NA KUUKABIDHI KWA WAHUSIKA NA JINSI WALIVYOKABIDHIWA".

Jamani hilo zigo si tuambiane ni zigo gani kwani?
Na mchongo uliendaje kwani?Hapa ni JF hakifichwi kitu ni open and truth only.
 
Jana nilipokuwa nikimwangalia WM wetu ni kama vile alikuwa anasoma RISALA tu. Nadhani Bunge lilimkabidhi Azimio lile huku likijua fika kwamba HANA MAMLAKA yoyote kama WM kwa yeyote yule katika lile sakata zima.
Na yeye WM kama alivyo siku zote ni mtu wa tahadhari muda wote, akaishia kulieleza Bunge watu wote amewakabidhi kwenye MAMLAKA husika kwa hatua zaidi!
 
Pinda alijibu zile hoja vizuri na kwa ufasaha na kuzingatia sheri za Nchi,Siyo rahisi kuamua jambao ambalo linawedha kumfedhehesha Rais.Rejea Hotuba ya rais ya mwezi April Mwaka jana..aliwahid kumwadhibu mtu kwa kumuonea na sasa amekuwa makini sana..
 
Hosea, Mwanyika kiama chao Ikulu

2008-08-29 09:37:41
Na Waandishi Wetu

Hatma ya vigogo wanaotuhumiwa kuhujumu nchi kupitia mradi tata wa kampuni ya kufua umeme ya Richmond imewekwa kiporo, baada ya Bunge kuambiwa kuwa mstakabali wao uko mikononi mwa Rais Jakaya Kikwete.

Vigogo wote wanaodaiwa kuhusika kwa namna moja au nyingine katika kashta hiyo wameandikiwa barua za kutakiwa kujieleza ndani ya siku 14 na wote wamefanya hivyo.

Waziri Mkuu, Bw. Mizengo Pinda, alisema hayo mjini Dodoma jana wakati akiwasilisha ripoti ya serikali kuhusu namna ilivyotekeleza mapendekezo 23 ya Kamati Teule ya Bunge iliyochunguza utata huo.

Alisema barua zao za kujieleza zinafanyiwa kazi na iwapo watabainika kuhusika watafikishwa mahakamani. Hata hivyo, uamuzi wa kuwachukulia hatua vigogo hao umechukua zaidi ya miezi sita tokea Bunge kupitisha pendekezo hilo, Februari mwaka huu.

Vigogo ambao hatma yao iko Ikulu ni Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Dk. Edward Hosea, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Bw.Johnson Mwanyika, Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Bw. Athur Mwakapugi na Kamishna wa Nishati wa wizara hiyo, Bw. Bashir Mrindoko.

Alisema vigogo hao wameandikiwa barua na kutakiwa kujieleza kwa misingi ya sheria ya haki za binadamu ya kujitetea kabla ya kuhukumiwa na kwamba maelezo yao yamewasilishwa na sasa yanashughulikiwa na Ikulu.

Watendaji hao wameteuliwa na Rais Jakaya Kikwete, hivyo mamlaka yenye wajibu wa kuwawajibisha ni Ikulu.

Waziri Mkuu aliliambia Bunge kuwa, katika barua za kuchukuliwa hatua za kinidhamu wamepewa maeneo ya kutoa maelezo ya jinsi walivyohusika kwenye mkataba huo.

Pia walivyoshindwa kuikagua, kuona udanganyifu wa kisheria na kuishauri serikali kuwa Richmond LLC haikuwa na uwezo kifedha, utaalamu na kisheria kupewa zabuni ya kufua umeme wa dharura wa megawati 100.

Kadhalika wametakiwa kujieleze jinsi zabuni hiyo ilivyotolewa kwa kukiuka taratibu za Sheria za Manunuzi ya Umma (PPRA), kutokuwa makini na kutambua udanganyifu wa kampuni hiyo na jinsi ilivyojitangaza kuwa ina ubia na kampuni kubwa zenye uwezo na kujinadi kuwa inaendesha miradi mikubwa nchini, madai ambayo si ya kweli.

Kwa upande wa Dk. Hosea, ametakiwa kujibu taarifa yake kuwa mchakato wa kumpata mzabuni Richmond ulikuwa wa wazi na hakuna jinai inayowahusisha viongozi.

Taarifa hiyo ya TAKUKURU ilisema hakukuwa na hasara kwa serikali licha ya kuwepo kwa mapungufu madogo ya kiutendaji na kusisitiza kuwa hakuna ushahidi wa kuwepo uzembe wala rushwa.

Kwa upande wa Mrindoko, ametakiwa kujieleza kwenye eneo la kushindwa kumshauri Mwakapugi kuhusu udhaifu wa Richmond LLC ambao aliujua tangu mwaka 2004 kwenye mkataba wa kujenga bomba la mafuta kutoka Dar es Salaam hadi Mwanza.

``Mrindoko ndiye aliyeiandikia barua kampuni hiyo kusitisha mkataba na serikali mwezi mmoja tu kabla ya mchakato wa zabuni ya umeme wa dharura haujaanza, `` Waziri Mkuu alinukuu sehemu ya pendekezo la kamati ya Bunge.

Kuhusu Mwanyika, alisema alionekana kuwa na udhaifu mkubwa wa kitaalamu na ukosefu wa umakini katika kuiwakilisha serikali na kushindwa kutambua ukosefu wa sifa za kikampuni na kushindwa kuifanyia ukaguzi wa awali ama baada ya uteuzi.

Hata hivyo, alisema Mwanasheria Mkuu amewasilisha maelezo yake ya utetezi Ikulu na yanafanyiwa kazi na Ofisi ya Rais.

Kwa upande mwingine, alisema wajumbe wa kamati ya serikali ya majadiliano na maofisa wa TAKUKURU nao wamepewa barua za kujieleza na wameshawasilisha utetezi.

Waziri Mkuu aliwataja wajumbe hao ambao ni maofisa wa serikali kuwa ni Singi Madata kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, Theophillo Bwakea, Julius Sarota wote wa Wizara ya Nishati na Madini, Wakili wa Serikali Donald Chidowu, Stephen Mabada, Mohamed Salehe, Godson Makia, James Mtei na Wangwe Mwita wote wa Tanesco.

Alisema wajumbe kutoka Tanesco wamewasilisha utetezi kwenye kamati ya bodi ya shirika hilo ambayo itaishauri serikali hatua za kuchukua dhidi ya watumishi hao.

Kadhalika, alisema maofisa wanane wa Takukuru waliofanya uchunguzi na Dk. Hosea, akiwemo mpelelezi mkuu wa taasisi nao wamepewa barua na maelezo yao yanashughulikiwa na Ofisi ya Katibu Mkuu Kiongozi kwa kuwa Mkurugenzi wa TAKUKURU ni mtuhumiwa.

* SOURCE: Nipashe
 
Mimi nashikwa na hasira sana, yaani mijitu inakubali, na inaendelea kuimba CCM CCM mbona sisi ni wajinga kiasi hicho jamani??????????

Watu tulishakuwa na hasira sana,na dawa ambyo mie niliona ni ya msingi ni kujiunga nao tu..

CCM Nambari one!Chama Chetu cha Mapinduzi chajenga Nchi..
 
Watu tulishakuwa na hasira sana,na dawa ambyo mie niliona ni ya msingi ni kujiunga nao tu..

CCM Nambari one!Chama Chetu cha Mapinduzi chajenga Nchi..
cha bomoa nchi. hakuna wanachokijenga labda vitambi vyao
 
TAARIFA YA WAZIRI MKUU, MHE. MIZENGO P. PINDA, (MB.), KUHUSU UTEKELEZAJI WA MAAZIMIO YA BUNGE YA MKATABA BAINA YA TANESCO NA RICHMOND DEVELOPMENT COMPANY LLC – 28 AGOSTI 2008


UTANGULIZI:

1. Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa kifungu cha 37(1) cha Kanuni za Kudumu za Bunge (Toleo la 2007), naomba kuwasilisha Taarifa ya Serikali kuhusu Utekelezaji wa Maazimio ya Bunge ya Mkataba baina ya TANESCO na Kampuni ya Richmond Development Company LLC.

2. Mheshimiwa Spika, Katika Mkutano wa Kumi wa Bunge tarehe 15 Februari 2008, Bunge lako Tukufu lilipitisha Maazimio 23 baada ya mjadala wa Taarifa ya Kamati Teule ya Bunge iliyoundwa mwezi Novemba 2007 ili kuchunguza mchakato wa Zabuni ulioipa ushindi Kampuni ya Richmond Development Company LLC wa kuzalisha umeme wa dharura Nchini mwaka 2006. Kwa kuzingatia uzito wa suala hili, wakati nilipotoa Hotuba yangu ya kuahirisha Mkutano wa Kumi wa Bunge nilieleza kuwa Serikali itaunda Timu ndogo ya Wataalam ili kuchambua kwa makini na kupendekeza namna ya kutekeleza Maazimio hayo 23 yaliyopitishwa na Bunge. Vilevile, niliahidi kuwa Kamati hiyo itazingatia mambo yote muhimu yaliyomo kwenye Taarifa ya Kamati Teule ya Bunge na Taarifa za majadiliano zilizoingizwa kwenye kumbukumbu za Bunge (HANSARD).

3. Mheshimiwa Spika, tarehe 25 Aprili 2008 wakati nikitoa Hotuba yangu ya kuahirisha Mkutano wa Kumi na moja wa Bunge lako Tukufu, niliwasilisha Taarifa ya Awali ya hatua zilizochukuliwa na Serikali katika utekelezaji wa Maazimio hayo.

Aidha, niliahidi pia kuwa Serikali itajitahidi kuharakisha utekelezaji wa Maazimio hayo kwa kadri itakavyowezekana na Taarifa rasmi itawasilishwa katika Mkutano huu wa Kumi na Mbili wa Bunge, jambo ambalo linafanyika leo.

4. Mheshimiwa Spika, mwezi Februari 2008 Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania , alikubali kujiuzulu kwa aliyekuwa Waziri Mkuu Mheshimiwa Edward Lowassa (Mb.). Aidha, Mawaziri wawili, Mheshimiwa Dkt. Ibrahim Msabaha, (Mb.), na Mheshimiwa Nazir Karamagi (Mb.), nao kwa wakati mmoja walijiuzulu kwa kuwajibika kwao kisiasa kwa Maslahi ya Taifa. Kutokana na uamuzi wa aliyekuwa Waziri Mkuu kujiuzulu, Kikatiba kulisababisha Baraza zima la Mawaziri kuvunjwa, jambo ambalo lilikuwa ni uamuzi mkubwa kwa Serikali. Hatua hii inaonyesha kiwango kikubwa cha usikivu wa Serikali yetu. Hasa kwa kuzingatia kwamba, hatua hii ilichukuliwa mapema mara tu baada ya Taarifa ya Kamati Teule kuwasilishwa katika Bunge lako Tukufu.

5. Mheshimiwa Spika, pamoja na hatua hiyo, napenda kueleza hatua nyingine muhimu zilizochukuliwa na Serikali hadi hivi sasa:-

Kwanza , Serikali imekwishapeleka maelekezo kwa kila Wizara na Taasisi zinazohusika na utekelezaji wa Maazimio haya na hatua za utekelezaji zinaendelea kuchukuliwa na Vyombo hivyo;

Pili, Kufuatia utata uliojitokeza kuhusu uhalali wa Mkataba baina ya TANESCO na Richmond Development Company LLC uliorithiwa na Dowans S.A, Serikali imechukua hatua ya kusitisha Mkataba huo kuanzia tarehe 1 Agosti 2008.

Tatu, Serikali imesitisha malipo yote ya fedha zinazohusiana na Mkataba baina ya TANESCO na Richmond Development Company LLC uliorithiwa na Kampuni ya Dowans S.A. ;

Nne, Watumishi wote wa Umma waliohusika katika mchakato wa kuandaa na kutoa Zabuni ya Mkataba baina ya TANESCO na RICHMOND wameandikiwa barua za kujieleza kama hatua za awali za Kinidhamu kwa kuzingatia Sheria, Taratibu na Kanuni za Utumishi wa Umma. Aidha, kwa wale watakaoonekana kuwa wamefanya makosa ya jinai, hatua stahiki za Kisheria zitachukuliwa dhidi yao .

6. Mheshimiwa Spika, baada ya utangulizi huo sasa ningependa kueleza kipengele kwa kipengele kuhusu hatua za utekelezaji wa Maazimio yote kama yalivyorekebishwa tarehe 15 Februari 2008 na Mtoa Hoja wakati akihitimisha hoja yake.


AZIMIO NAMBA 1:
" Sheria ya Manunuzi ya Umma ya Mwaka 2004 (Public Procurement Act, 2004) haina nguvu ya kutosha. Sheria ipitiwe upya ili kuiboresha kwa kuipa Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA) nguvu zaidi za udhibiti na uwezo wa kuchukua hatua pale Sheria na Kanuni zinapokiukwa, badala ya kutoa ushauri tu kama ilivyo sasa."

HATUA ZILIZOCHUKULIWA:
Wizara ya Fedha na Uchumi ikishirikiana na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali pamoja na Mamlaka ya Udhibiti wa Manunuzi ya Umma (PPRA), wamekwishaainisha maeneo yote yenye mapungufu na yanayohitaji marekebisho kwenye Sheria ya Manunuzi ya Umma ya mwaka 2004.

Baada ya zoezi hilo kufanyika, Serikali itawasilisha katika Mkutano wa Kumi na Tatu wa Bunge lako Tukufu, Mapendekezo ya kufanya Marekebisho katika Sheria hiyo. Maeneo yatakayozingatiwa ni yafuatayo:

(i) Kuipa uwezo PPRA kusitisha Zabuni yoyote pale itakapobainika kuwepo kwa ukiukwaji wa Sheria na Kanuni zinazosimamia Manunuzi ya Umma.
(ii) Kuipa nguvu PPRA kutoa maelekezo kwa Mamlaka zinazohusika na ununuzi, (yaani Procuring Entities) kuchukua hatua kwa watakaokiuka Sheria ya Manunuzi ya Umma.

(iii) Kuifanya PPRA kuwa Taasisi Huru inayojitegemea ikiwa na Muundo sawa na ule wa Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Serikali (CAG).

(iv) Kufanya marekebisho yatakayowezesha Sheria kutoa adhabu kali kwa Viongozi na Watumishi wa Umma watakaobainika kujihusisha na ukiukwaji wa Sheria na Kanuni za Manunuzi ya Umma.

(v) Kufanya marekebisho ya kuzitaka Mamlaka zenye dhamana zitakazopokea hoja za ukiukwaji wa Sheria ya Manunuzi ya Umma kutoka PPRA, kutoa taarifa kuhusu hoja hizo katika kipindi maalum, na ikibidi kuchukua hatua zaidi kwa Taasisi au Mtu atakayekiuka Sheria na Kanuni za Manunuzi ya Umma.

(vi) Kuweka utaratibu mzuri wa namna ya kushughulikia masuala ya Ununuzi wa Dharura yanapotokea.

(vii) Kuweka utaratibu wa kuwezesha kufanyika uchunguzi wa kina (due deligence) kwa Wazabuni wa ndani na nje ya Nchi wanaoomba kuingia Mikataba na Serikali.

(viii) Kuweka Utaratibu wa kutumia Kamati Huru ya Wataalam itakayofanya uchunguzi wa kina pale itakapobidi.


AZIMIO NAMBA 2:
"Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA) isiwajibike Wizara ya Fedha ambayo nayo ni Taasisi ya Ununuzi (Procuring Entity) badala yake iwe chombo huru kinachowajibika Ofisi ya Rais na Taarifa zake kuwasilishwa Bungeni."

HATUA ZILIZOCHUKULIWA:
(i) Kulingana na Sheria ilivyo hivi sasa, PPRA ni Taasisi Huru inayojitegemea nje ya Muundo wa Wizara ya Fedha na Uchumi. Aidha, PPRA ina Bajeti yake inayojitegemea na pia ina Chombo chake Maalum cha Usimamizi, (yaani Bodi ya Wakurugenzi). Hata hivyo, katika Marekebisho ya Sheria yanayotarajiwa kufanyika, Serikali inakusudia kuwasilisha pendekezo la kufanya PPRA iwe na Muundo sawa na ule wa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, (CAG) ambapo utatoa uhuru kwa Chombo hicho kutoa maamuzi ya kila siku bila kuingiliwa na Chombo chochote, ingawa Kisera itaendelea kuwa chini ya usimamizi wa HAZINA kama ilivyo kwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali.

(ii) Kuhusu Taarifa za mwaka za PPRA kuwasilishwa Bungeni, suala hili limezingatiwa katika Kifungu cha 26 (2) cha Sheria ya Manunuzi ya Umma ya mwaka 2004, inayotumika hivi sasa. Chini ya Sheria hiyo, Waziri wa Fedha na Uchumi huwasilisha Bungeni Taarifa ya kila mwaka ya utendaji wa PPRA.


AZIMIO NAMBA 3:
"Mikataba kati ya TANESCO na Richmond Development Company LLC (uliyorithiwa Dowans Holdings S.A) na ile kati ya TANESCO na IPTL, SONGAS, AGGREKO na Alstom Power Rentals ipitiwe upya mapema iwezekanavyo kama ambavyo Mikataba ya Madini ilivyopitiwa upya na Serikali. Bila kufanya hivyo, mzigo mkubwa wa gharama za umeme utawaelemea Wananchi na kushindwa kufikia azma ya Serikali ya maisha bora kwa kila Mtanzania"

HATUA ZILIZOCHUKULIWA:
Pamoja na kutoa Taarifa ya utekelezaji wa Azimio hili, napenda kueleza kuhusu hali ilivyo sasa kwa Mikataba baina ya TANESCO na IPTL, SONGAS, AGGREKO na Alstom Power Rentals.

(i) Mkataba baina ya TANESCO na IPTL

Mgogoro uliopo sasa kati ya TANESCO na IPTL unatokana na§ kutokubaliana kwa pande zote mbili kuhusu kiwango cha capacity charge kinachotozwa na IPTL.

Kwa mujibu wa Mkataba wa kuuziana Umeme kati ya§ IPTL na TANESCO, capacity charge inapaswa kukokotolewa kwa kuzingatia mtaji (equity) wa asilimia 30 na faida ya asilimia 22.31 uliopaswa kuwa umewekezwa (ambao ni US$ 36.54 milioni) wakati IPTL wanaanza kuzalisha Umeme na kuiuzia TANESCO tarehe 15 Januari, 2002. Hata hivyo, kufuatia uchunguzi uliofanywa na TANESCO imegundulika kwamba mtaji halisi wakati IPTL inaanza kuzalisha Umeme ulikuwa Shilingi Hamsini Elfu tu (50,000/=). Hivyo, mtaji huu ndiyo unaostahili kutumika kukokotoa capacity charge inayolipwa IPTL na si vinginevyo.

§ Kwa mantiki hiyo, madai ya TANESCO na Serikali katika Mradi huu ni kuwa, capacity charge inayotozwa na IPTL izingatie kiwango halisi cha mtaji (equity) uliowekezwa na IPTL, na si zaidi ya hapo. Aidha, Serikali na TANESCO inadai kutoka IPTL kiasi chote cha malipo kilichofanywa kimakosa kama capacity charge ambacho hakikustahili kulipwa kwa IPTL.

Kutokana Serikali kutoridhika§ na kiwango cha malipo ya capacity charge chini ya Mradi huu wa IPTL, ilisitisha malipo kwa IPTL; jambo ambalo lilipelekea IPTL kufungua Shauri la Madai dhidi ya TANESCO kwenye Mahakama ya New York Nchini Marekani mwezi Novemba 2007. Mnamo mwezi Aprili 2008 Serikali ilishinda Shauri hilo baada ya Mahakama hiyo kutupilia mbali shauri hilo na kuelekeza kwamba mgogoro huo uwasilishwe kwenye Baraza la Usuluhishi (Arbitration) kama Mkataba baina ya pande mbili unavyoelekeza.

Tarehe 9 Julai, 2008 IPTL iliwasilisha mgogoro huu§ kwenye International Centre for Settlement of Investment Disputes (ICSID). Kwa sasa shauri hili bado halijatolewa uamuzi.

Hata hivyo, Serikali§ imejiandaa ipasavyo kutetea na kulinda haki zake chini ya Kamati Maalum ya Serikali iliyoundwa kushughulikia mgogoro huu. Mmoja wa Wajumbe wa Kamati hiyo Maalum, ni Wakili mzoefu wa Kujitegemea Mheshimiwa Nimrod Elirehema Mkono, Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini.

Hivyo, Mkataba huu tayari§ umekwishapitiwa na Kamati husika na mapungufu yake yaliyobainika ndiyo yamepelekea kuwepo kwa Shauri hili.

(ii) Mkataba baina ya TANESCO na RICHMOND (uliorithiwa na DOWANS)

Kutokana na utata uliojitokeza katika mchakato mzima kuhusu Mkataba baina ya TANESCO na RICHMOND uliotiwa saini tarehe 23 Juni 2006, Serikali kupitia TANESCO iliamua kufanyike mapitio ya Mkataba huo na kupata ushauri wa kitaalam kutoka kwa Wanasheria waliobobea katika masuala ya Mikataba ya Kimataifa wa Kampuni ya REX ATTORNEYS. Uchunguzi wa REX ATTORNEYS ulibaini pamoja na mambo mengine kwamba:-

(a) Utaratibu mzima wa manunuzi ya huduma ya umeme na kuingia Mkataba na Richmond Development Company LLC ulikiuka Sheria ya Manunuzi ya Umma ya mwaka 2004;

(b) Kutokana na ukiukwaji huo, Mkataba baina ya TANESCO na Richmond Development Company LLC haukuwa halali na hauna nguvu ya Kisheria; na,

(c) Vilevile, hata kama Mkataba husika ungekuwa halali, uhamishaji (assignment) wa Mkataba huo kutoka RDEVCO badala ya Richmond Development Company LLC kwenda DOWANS HOLDINGS S.A. na hatimaye Dowans Tanzania Limited haukuwa halali.

Kwa kuzingatia mapungufu hayo yaliyobainishwa katika Mkataba huo, Serikali iliamua kusitisha huduma za Dowans Tanzania Limited kuanzia tarehe 1 Agosti 2008.


(iii) Mkataba baina ya TANESCO na Alstom Power Rentals (APR)

Kama ilivyoelezwa na Waziri wa Nishati na Madini Mheshimiwa William Ngeleja (Mb.) wakati akiwasilisha Hotuba yake hapa Bungeni, tarehe 8 Julai 2008, katika Mkutano huu wa Bunge lako Tukufu, alifafanua kuwa, mitambo ya Alstom Power Rentals ilikodishwa na TANESCO kwa kipindi cha miezi 12 kuanzia tarehe 20 Machi, 2007 hadi tarehe 19 Machi, 2008. Baada ya muda wa Mkataba huo kumalizika, Serikali haikuhuisha Mkataba huo, licha ya jitihada za Wahusika kutaka uhuishwe.

(iv) Mkataba baina ya TANESCO na AGGREKO

Mkataba baina ya TANESCO na AGGREKO ulianza kutekelezwa mwezi Desemba 2006 na unatarajiwa kumalizika mwezi Novemba 2008. Kamati ya Serikali ya Wataalam inapitia Mkataba huu ili kujiridhisha kama upo kwa maslahi ya Taifa na kuchukua hatua kadri itakavyoonekana inafaa.

(v) Mkataba baina ya TANESCO na SONGAS

Kwa sasa Mkataba mkubwa wa Sekta ya Nishati ambao unapaswa kupitiwa upya ni baina ya TANESCO na SONGAS. Mkataba wa SONGAS unahusisha Wadau wengi na unajumuisha Mikataba midogo mbalimbali ipatayo ishirini na moja inayohusu masuala ya utafutaji, usambazaji, ununuzi na mikopo ya uendelezaji wa Gesi Asilia na hivyo kuwa na uzito wa aina yake, (complex). Ili kuwa na tija katika mapitio ya Mikataba hiyo na kupata ushauri mzuri, Serikali inaendelea kushauriana na Wataalam Washauri waliobobea katika Sekta hii ya Gesi Asilia wakiwemo Wanasheria, ambao wataweza kushauri ipasavyo iwapo kuna mapungufu yoyote yanayostahili kufanyiwa marekebisho kwa maslahi ya Taifa.


AZIMIO NAMBA 4:
"Serikali itathmini upya uhalali wa kuwepo Mkataba kati ya TANESCO na Richmond Development Company LLC (sasa Dowans Holdings S.A.) kwa lengo la kusitisha malipo kwa Dowans Holdings S.A. na kuvunja Mkataba huo haraka iwezekanavyo."

HATUA ZILIZOCHUKULIWA:
Kama nilivyoeleza awali, kufuatia utata ulijitokeza kuhusu uhalali wa Mkataba baina ya TANESCO na RICHMOND uliorithiwa na Dowans, Serikali imesitisha Mkataba huo kuanzia tarehe 1 Agosti 2008. Vilevile, Serikali imesitisha malipo yote ya fedha zinazohusiana na Mkataba huo.


AZIMIO NAMBA 5:
"Kwa kuwa Mkataba kati ya TANESCO na Richmond Development Company LLC (sasa Dowans Holdings S.A) umesheheni makosa mengi ya kisheria yanayoashiria udhaifu mkubwa wa kitaalam katika Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali au ukosefu wa umakini katika kuiwakilisha Serikali; Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Wakili wa Serikali Donald Chidowu ambaye ushiriki wake katika GNT haukuwa na tija yoyote, wawajibishwe na Mamlaka ya juu ya Nchi kwa kuchangia kuiingiza Nchi katika Mkataba wa aibu."

HATUA ZILIZOCHUKULIWA:
(i) Kikatiba, Mwanasheria Mkuu wa Serikali ndiye Mshauri Mkuu wa Serikali katika masuala yote ya Sheria za Nchi. Hivyo, ana wajibu mkubwa wa kuishauri Serikali katika maeneo ambayo anaona yanakiuka Sheria, Taratibu na Kanuni za Nchi.

Kutokana na nafasi yake Kikatiba, Mamlaka yake ya Nidhamu ni Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania . Kwa hiyo, Mwanasheria Mkuu wa Serikali ambaye alikuwa miongoni mwa Watendaji Wakuu watatu waliokuwa wanaishauri Serikali, suala lake la kuhusishwa kwake katika Mchakato mzima wa Mkataba huo linashughulikiwa na Ofisi ya Rais, IKULU.

(ii) Kuhusu Wakili wa Serikali Bw. Donald Chidowu ambaye alikuwa ni miongoni mwa Wajumbe wa Kamati ya Majadiliano (GNT), akimwakilisha Mwanasheria Mkuu wa Serikali, amepelekewa barua ya kutakiwa ajieleze kwa kuzingatia Misingi ya Kanuni Asilia ya Haki ya Kusikilizwa Kwanza (Natural Justice) na kuzingatia Sheria za Utumishi wa Umma. Mtumishi huyu amewasilisha utetezi wake kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Sheria na Katiba ambaye ndiye Mamlaka yake ya Nidhamu katika muda wa siku kumi na nne zilizotakiwa. Hivi sasa, maelezo ya utetezi wake yanafanyiwa uchambuzi na Mamlaka yake ya Nidhamu ili hatimaye maamuzi yatolewe kwa kuzingatia Sheria, Kanuni na Taratibu za Utumishi wa Umma.


AZIMIO NAMBA 6:
"Katika kushughulikia Mikataba yote na Makampuni ya Nje, Serikali ihakikishe kuwa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) inatumika kikamilifu kupata Taarifa kamili za Makampuni haya. Aidha, Ofisi zetu za Ubalozi zilizo sehemu mbalimbali Duniani zihusishwe katika majadiliano na Makampuni yanayotoka nje ya Nchi, na vilevile katika kuyachunguza Makampuni hayo kwa lengo la kupata Taarifa zao za msingi na kuboresha nguvu ya hoja ya Serikali, kabla ya kuingia Mikataba husika."

HATUA ZILIZOCHUKULIWA:
Serikali imetafakari na kuzingatia kwa makini pendekezo hili. Hatua zilizoanza kuchukuliwa ni pamoja na zifuatazo:

(i) Kuanzia sasa, Balozi zetu zote za nje zitakuwa zinashirikishwa kikamilifu katika kufanya uchunguzi wa kina (due diligence) kwa Makampuni ya nje ambayo Serikali inatarajia kuingia nayo Mikataba katika manunuzi au katika miradi mikubwa. Serikali imeshatoa maelekezo haya kwenye Wizara zote. Aidha, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa nayo imetoa maelekezo kwa Balozi zetu zote ili zizingatie uamuzi huu.

(ii) Kama ilivyoelezwa katika Azimio Na. 1, Serikali itawasilisha mapendekezo kuhusu marekebisho ya Sheria ya Manunuzi ya Umma ili kuongeza Kifungu kinachohusu kufanya uchunguzi wa kina (due deligence) wa Wazabuni wa ndani na nje ya Nchi wanaoomba kuingia Mikataba na Serikali. Miongoni mwa mapendekezo hayo ni pamoja na kuwa na Kamati Huru ya Wataalam itakayofanya uchunguzi huu wa kina, pale itakapobidi.

(iii) Katika kuhakikisha kuwa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano inatumika ipasavyo katika masuala ya Manunuzi ya Umma, PPRA tayari imeanzisha Mfumo wa Habari na Mawasiliano katika Manunuzi ya Umma ujulikanao kama "Procurement Management Information System". Ni matumaini ya Serikali kuwa, Mfumo huu utatumika kurahisisha upatikanaji wa Taarifa mbalimbali za Manunuzi kati ya Mamlaka (yaani PPRA) na Taasisi za Ununuzi.


AZIMIO NAMBA 7:
"Wajumbe wote wa Kamati ya Serikali ya Majadiliano (Government Negotiation Team – GNT) ambao ni Maofisa Waandamizi wa Serikali wawajibishwe kwa manufaa ya Umma kwa kulitia hasara Taifa kutokana na kushindwa kutumia elimu na ujuzi wao kulinda maslahi ya Taifa".

HATUA ZILIZOCHUKULIWA:
Katika kushughulikia suala hili, (yaani katika mchakato mzima wa Zabuni pamoja na majadiliano ya Mkataba baina ya TANESCO na RICHMOND ), kulikuwa na Kamati za aina tatu.

Kwanza , ni Kamati iliyokuwa inaundwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mheshimiwa Johnson Mwanyika (Mb.), Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Bw. Arthur Mwakapugi pamoja na Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha na Uchumi Bw. Gray Mgonja. Kamati hii ilikuwa na jukumu la kutoa ushauri kwa Waziri wa Nishati na Madini na Serikali kwa ujumla.

Kamati ya pili, ilikuwa ni Timu ya Wataalam (Expert Team) iliyokuwa na Wajumbe kutoka Wizara na Taasisi zifuatazo:

1. Bw. Singi Madata - Fedha na Uchumi (Mwenyekiti);
2. Dkt. Lutengano Mwakahesya-Nishati na Madini (Mjumbe);
3. Bw. Theophilo Bwakea-Nishati na Madini, (Mjumbe);
4. Bw. Stephen Mabada - TANESCO (Mjumbe);
5. Bw. Athanas Mbawala - TANESCO (Mjumbe);
6. Bw. James Mwalilimo - TANESCO (Mjumbe);
7. Bw. Julius Sarota - Nishati na Madini (Sekretarieti).

Kamati hii ilikuwa na jukumu la kutathmini Wazabuni wote waliokuwa wameomba Zabuni ya mitambo ya kukodi ya dharura ya kufua umeme wa Megawati 105.6.

Kamati ya tatu ni ile ya Majadiliano baina ya Serikali na Wawakilishi wa Kampuni ya Richmond Development Company LLC. Wajumbe wa Kamati hii ni wafuatao:-

1. Bw. Singi Madata - Fedha na Uchumi (Mwenyekiti);
2. Bw. Theophilo Bwakea- Nishati na Madini (Mjumbe);
3. Bw. Stephen Mabada - TANESCO (Mjumbe);
4. Bw. Godson Makia - TANESCO (Mjumbe);
5. Bw.Donald Chidowu-Ofisi ya Mwanasheria Mkuu (Mjumbe);
6. Bw. Dick Thewa – Benki Kuu ya Tanzania (Mjumbe);
7. Bw. Gideon Nassari – CTI (Mjumbe);
8. Bw. Julius Sarota - Nishati na Madini (Sekretarieti);
9. Bw. Mwita Wangwe – TANESCO (Sekretarieti).

Kamati mbili za Wataalam (yaani Kamati ya pili na ya tatu) zote zilikuwa zinaripoti na kutoa ushauri kwa Kamati ya Makatibu Wakuu wawili wa Hazina, na Nishati na Madini pamoja na Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Kwa madhumuni ya utekelezaji wa Azimio hili, Wajumbe wote wa Kamati hizi tatu wamepelekewa barua za kutakiwa watoe maelezo kwa mujibu wa Sheria zinazohusu nidhamu katika Utumishi wao. Hatua hii inazingatia Misingi ya Kanuni Asilia ya Haki ya Kusikilizwa Kwanza (Natural Justice), kabla ya hatua nyingine kuchukuliwa.

Miongoni mwa maeneo ambayo Watumishi hawa wametakiwa kutoa maelezo ni jinsi walivyohusika katika mchakato mzima na kuiingiza Serikali katika Mkataba unaoonekana kutokuwa na Maslahi kwa Taifa. Maeneo hayo ni pamoja na:

(i) Kutotumia utaalam na uzoefu wao kikamilifu ili kutambua mapema kuwa Richmond Development Company LLC haikuwa na uwezo kitaalam, kifedha na kiuzoefu na hivyo kutokidhi matakwa ya Zabuni.

(ii) Kutozingatia kikamilifu Sheria ya Manunuzi ya Umma, ya mwaka 2004 katika mchakato mzima wa kutoa Zabuni hii.

(iii) Wajumbe kushindwa kuishauri Serikali kuhusu kuifanyia Kampuni ya Richmond Development Company LLC uchunguzi wa awali (due diligence) pamoja na ukaguzi baada ya tathmini ya Zabuni (post qualification);
(iv) Kutokuwa makini na hivyo kushindwa kutambua udanganyifu wa ubia/uhusiano wa kibiashara kati ya Richmond Development Company LLC na Kampuni ya Kimataifa ya Pratt & Whitney;

Watumishi wote wameshawasilisha utetezi wao katika muda wa siku kumi na nne zilizopangwa. Aidha, hivi sasa utetezi wao unafanyiwa uchambuzi wa kina na Mamlaka zao za nidhamu ili hatua muafaka zichukuliwe kwa mujibu wa Sheria, Kanuni na Taratibu zinazotawala utumishi wao.

Kwa upande wa Watumishi wa TANESCO ambao ni Bw. Stephen Mabada, Bw. Athanas Mbawala, Bw. James Mwalilimo, Bw. Godson Makia na Bw. Mwita Wangwe, Kamati Ndogo ya Nidhamu ya Bodi ya TANESCO tayari imekwishapitia maelezo ya Watumishi wao wote na mapendekezo ya Kamati hiyo yamewasilishwa kwenye Bodi ya Wakurugenzi ya TANESCO ambayo itatoa maamuzi yake na kuiarifu Serikali.


AZIMIO NAMBA 8:
"Waziri wa Nishati na Madini, Mhe. Nazir Karamagi (Mb.), aliyeshabikia sana uhaulishaji wa Mkataba kutoka kwa Richmond Develeopment Company LLC kwenda kwa Dowans Holdings S.A. awajibishwe"

HATUA ZILIZOCHUKULIWA:
Mheshimiwa Nazir Karamagi (Mb.), aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini alijiuzulu mwezi Februari 2008 kwa kuwajibika kutokana na suala hili. Hata hivyo, kwa lengo la Serikali kujiridhisha kuhusu ushiriki na ushauri wake katika suala hili, Vyombo vya Dola vinaendelea na uchunguzi wa kina kwa lengo la kutaka kujua kama kuna rushwa yoyote ambayo ilijitokeza katika mchakato huu inayomhusisha Mheshimiwa Nazir Karamagi (Mb.), katika suala hili. Taarifa ya uchunguzi huo itawezesha Serikali kuamua juu ya hatua zaidi zinazostahili kuchukuliwa dhidi yake.


AZIMIO NAMBA 9:
"Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU awajibishwe kwa ma@nufaa ya Umma na Maofisa wa TAKUKURU walioshiriki katika zoezi la uchunguzi na kuandaa Taarifa ya Richmond Development Company LLC iliyoficha ukweli nao pia wawajibishwe kwa manufaa ya Umma."

HATUA ZILIZOCHUKULIWA:
Zoezi la kufanya uchunguzi lililofanywa na TAKUKURU lilihusisha Watumishi wafuatao:

(i) Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Bw. Edward Hosea akiwa ndiye Msimamizi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), iliyohusika na uchunguzi wa mchakato mzima wa Zabuni ya umeme wa dharura, ulioipa ushindi Kampuni ya Richmond Development Company LLC.

(ii) Mkurugenzi wa Upelelezi Bw. Alex Mfungo ambaye ndiye aliyesimamia zoezi zima la uchunguzi na kuandaa Ripoti ya Uchunguzi ya TAKUKURU kuhusu suala hili.

(iii) Maofisa wanane wa TAKUKURU walioshiriki katika zoezi la uchunguzi na kuandaa Taarifa katika maeneo yao ya utaalam katika mchakato mzima wa Zabuni ya Ununuzi wa mitambo ya umeme wa dharura ulioipa ushindi Kampuni ya Richmond Develeopment Company LLC.

Ili kutekeleza Azimio hili, Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU amepelekewa barua ya kutakiwa kujieleza na Mamlaka yake ya Nidhamu ambaye ni Katibu Mkuu Kiongozi. Vilevile, Wasaidizi walio chini yake walioshiriki katika zoezi la uchunguzi, nao wametakiwa kutoa maelezo yao kwa Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU ambaye ndiye Mamlaka yao ya Nidhamu. Hii ni kwa kuzingatia Misingi ile ile ya Kanuni Asilia ya Haki ya Kusikilizwa Kwanza (Natural Justice).

Hata hivyo, kwa kuzingatia mazingira ya shauri hili, Katibu Mkuu Kiongozi ataamua juu ya utaratibu mzuri wa hatua za nidhamu dhidi ya Wasaidizi wote wa Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU waliohusika katika suala hili.

Baadhi ya maeneo ambayo Mkurugenzi Mkuu na Wasaidizi wake wamepelekewa barua wajieleze ni yafuatayo:

(i) Kushindwa kuona kuwa Taarifa ya Uchunguzi iliyofanywa na Wataalam wa Taasisi yake haikubainisha kuwepo kwa kasoro nyingi zilizokuwepo katika Zabuni hiyo kama zilivyoainishwa katika Taarifa ya Kamati Teule ya Bunge, badala yake Taasisi iliona kwamba:-

§ Mchakato mzima ulizingatia Sheria, Kanuni na Taratibu za Serikali;

§ Hayakuwepo mapungufu makubwa katika Zabuni hii;

Hakukuwa na hasara kwa§ Taifa kutokana na Zabuni hii.

(ii) Kushindwa kuona kuwa ushauri uliotolewa na PPRA kwa TANESCO kuhusu muda wa kutangaza Zabuni Kimataifa ulipuuzwa na hivyo kuvunjwa kwa Taratibu za Sheria ya Manunuzi ya mwaka 2004, na hivyo kutia shaka.
Hivi sasa, Watumishi wote tisa wameshawasilisha utetezi wao katika muda uliopangwa. Aidha, kwa kuzingatia Sheria, Kanuni na Utaratibu wa Utumishi wa Umma, Mamlaka yao ya Nidhamu inapitia utetezi wao ili kutoa uamuzi unaostahili.


AZIMIO NAMBA 10:
"Gavana wa Benki Kuu pamoja na Bodi ya Wakurugenzi wachunguze kwa makini uhalali wa malipo ya ziada (US$ 4,865,000) yaliyofanywa kwa Dowans Holdings A.S iliyorithi majukumu ya Richmond Development Company na kuwachukulia hatua waliohusika na uzembe huo."
HATUA ZILIZOCHUKULIWA:
Wizara ya Fedha na Uchumi na Benki Kuu ya Tanzania wamechunguza na kuona kuwa malipo ya US$ 4,865,000 yaliyolipwa kwa Kampuni ya Dowans Holdings S.A. iliyorithi majukumu ya Richmond Development Company LLC ni halali. Malipo hayo yalilipwa tarehe 2 Februari 2007 ikiwa ni gharama za ndege za usafirishaji wa mitambo ya kukodi ya umeme wa dharura, baada ya kupokea Invoice Na. EFD786675. Uchunguzi unaonyesha kuwa, taratibu zote za malipo zilifuatwa na malipo yalifanywa baada ya kuhakikiwa na TANESCO, Wizara ya Nishati na Madini na HAZINA baada ya kupata ushauri wa Kisheria kutoka kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwamba yanawiana na Mkataba husika.


AZIMIO NAMBA 11:
"Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma ya Mwaka 1995 (The Public Leadership Code of Ethics Act) ifanyiwe marekebisho makubwa ili kudhibiti utaratibu unaoonekana wa kawaida sasa wa Viongozi Waandamizi wenye dhamana ya kisiasa kuendelea na biashara zao binafsi wakiwa madarakani, jambo ambalo lina mgongano wa kimaslahi. Serikali ianze rasmi maandalizi ya majadiliano ya kina kuhusu suala hili ndani na nje ya Bunge kwa kuwashirikisha wadau mbalimbali."

HATUA ZILIZOCHUKULIWA:
(i) Kama alivyoeleza Mheshimiwa Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika Hotuba yake ya terehe 21 Agosti 2008 wakati akilihutubia Bunge lako Tukufu kwamba, Serikali inayo dhamira ya dhati ya kuangalia namna ya kutenganisha shughuli za biashara na uongozi katika Utumishi wa Umma katika ngazi za juu za Viongozi na Watendaji Waandamizi. Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, imeanza mchakato wa kushughulikia suala hili na tayari wamewasilisha mapendekezo yao ya awali Serikalini.

(ii) Hivi sasa Serikali imeunda Timu inayojumuisha Wajumbe kutoka Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, Tume ya Uchaguzi, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na TAKUKURU ili kufanya uchambuzi zaidi wa Mapendekezo hayo. Aidha, Timu hiyo itafanya uchambuzi wa Sheria za Nchi zilizofanikiwa kuweka utaratibu wa Viongozi wa Umma kuweza kutenganisha shughuli za biashara zao na Uongozi ili kuondoa mgongano wa kimaslahi.

(iii) Katika zoezi hili, Wananchi na Wadau mbalimbali watashirikishwa kikamilifu ili kupata maoni yao .

(iv) Baada ya hatua hizo, Serikali inatarajia kuwasilisha hapa Bungeni marekebisho ya Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma mwezi Aprili 2009.



AZIMIO NAMBA 12:
"Serikali ijiepushe kadri inavyowezekana na utaratibu wa kutumia Mawakala katika ununuzi wa Umma na kuhakikisha kuwa Wizara zote zina taarifa za bei halisi za mahitaji yao kila wakati ili kujiepusha na mchezo wa kawaida wa Mawakala kupandisha bei mara mbili au zaidi ya bei halisi."

HATUA ZILIZOCHUKULIWA:
Katika utekelezaji wa Azimio hili, Wizara zote, Wakala na Idara za Serikali Zinazojitegemea, Mikoa pamoja na Mashirika ya Umma zimeagizwa kuzingatia kikamilifu Taratibu za Manunuzi na Ugavi kama zilivyoainishwa katika Sheria ya Manunuzi ya Umma ya mwaka 2004. Pamoja na maelekezo hayo, hatua zifuatazo zitachukuliwa:

(i) Serikali imeamua kuwa, kila inapowezekana, Taasisi za Ununuzi zinunue vifaa moja kwa moja kutoka kwa watengenezaji wa bidhaa hizo. Ikibidi kununua kutoka kwa Wakala walioidhinishwa, ni lazima Taratibu za Manunuzi ya Umma zizingatiwe kikamilifu.

(ii) Katika hatua za awali, Wizara ya Fedha na Uchumi inaandaa Utaratibu wa kufanya Ununuzi wa pamoja wa bidhaa zinazoweza kutumika na Taasisi zaidi ya moja (Common use items). Utaratibu huo utakapokamilika, utawezesha bidhaa hizo kuagizwa kwa pamoja kupitia Wakala wa Serikali wa Huduma za Ununuzi na endapo itabidi, kununua moja kwa moja kutoka kwa watengenezaji kwa lengo la kupata unafuu wa bei.

(iii) Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma tangu mwezi Juni 2008, imempata Mtaalam Mwelekezi wa kuandaa Mfumo wa ununuzi wa pamoja na kupata takwimu za Bei Dira za bidhaa mbalimbali (Indicative Price) kutoka kwa Wazalishaji wa bidhaa na huduma. Kazi hiyo itakamilika mwezi Septemba 2008. Takwimu hizo zitawekwa katika mtandao wa Mamlaka na kwenye matoleo ya Jarida la Masuala ya Ununuzi Tanzania ili ziweze kutumiwa na Taasisi za Ununuzi pamoja na Wazabuni. Bei hizo zitafanyiwa mapitio ya mara kwa mara na PPRA.


AZIMIO NAMBA 13:
"Serikali izihusishe Kamati za Kudumu za Bunge kwenye hatua za awali za maandalizi ya Mikataba mikubwa ya kibiashara na ya muda mrefu ili kuondokana na utaratibu uliopitwa na wakati kwamba Mikataba ya Kibiashara ni siri, hata kwa walipa kodi wenyewe. Aidha, Serikali ihakikishe kuwa, Kamati zote za Bunge zinapitia Mikataba mikubwa ya kibiashara na ya muda mrefu chini ya Sekta zao ili kuliondolea Taifa mizigo isiyo ya lazima."

HATUA ZILIZOCHUKULIWA:
Tarehe 24 Aprili 2008, Ofisi ya Waziri Mkuu ilimwandikia barua Mheshimiwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kumfahamisha kuhusu utekelezaji wa awali wa baadhi ya Maazimio ya Kamati Teule yaliyopitishwa na Bunge. Katika barua hiyo, utekelezaji wa Maazimio Namba 13, 15, 16, 21 na 23 yalitolewa taarifa. Hata hivyo, kwa madhumuni ya Taarifa hii, ninapenda kurejea kwa muhtasari maelezo kuhusu utekelezaji wa Maazimio hayo.

Kuhusu Azimio Na. 13, Serikali imechambua Azimio hili kwa kina na imekubali kimsingi kwamba, Mikataba yote muhimu ya Serikali itakuwa inawekwa kwenye Maktaba Maalum ya Bunge ili Kamati za Bunge lako Tukufu ziweze kupata nafasi ya kupitia Mikataba mikubwa ya Kibiashara na ya muda mrefu chini ya Sekta zao na kushauri ipasavyo.

Kuhusu kuzihusisha Kamati za Kudumu za Bunge kwenye hatua za awali za maandalizi ya Mikataba mikubwa ya Kibiashara na ya muda mrefu, Serikali imeanza kufanya tafiti katika Mabunge ya Nchi za Jumuiya ya Madola ili kupata uzoefu zaidi utakaosaidia katika utekelezaji wa suala hili.


AZIMIO NAMBA 14:
"Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Ibrahim Msabaha (Mb.), na Katibu Mkuu, Ndugu Arthur Mwakapugi wachukuliwe hatua kali za kinidhamu kwa kuliingiza Taifa kwa makusudi kwenye Mkataba wa Kampuni ya Mfukoni. Aidha, Kamishna wa Nishati, Ndugu Bashir Mrindoko naye achukuliwe hatua za kinidhamu kwa kushindwa kumshauri Katibu Mkuu wake mpya kuhusu udhaifu wa Richmond Development Company LLC ambao ulijulikana dhahiri na Wizara mwaka 2004 kwenye Mradi wa bomba la mafuta. Ndugu Mrindoko ndiye aliyeiandikia barua Kampuni hiyo kusitisha Mkataba wake na Serikali mwezi mmoja tu kabla ya mchakato wa Zabuni ya umeme wa dharura haujaanza."

HATUA ZILIZOCHUKULIWA:
a) Mheshimiwa Dkt. Ibrahim Msabaha (Mb.), aliyekuwa Waziri wa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki alijiuzulu mwezi Februari 2008 kwa kuwajibika kutokana na suala hili. Hata hivyo, kwa lengo la Serikali kujiridhisha zaidi kuhusu ushiriki na ushauri wake katika suala hili, Vyombo vya Dola vinaendelea kuendesha uchunguzi wa kina. Lengo ni kutaka kujua kama kuna rushwa yoyote inayomhusisha Mheshimiwa Dkt. Ibrahim Msabaha (Mb.), ambayo ilijitokeza katika mchakato huu, ili hatimaye uamuzi stahiki dhidi yake uweze kuchukuliwa.

b) Kuhusu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Bw. Arthur Mwakapugi ambaye alikuwa miongoni mwa Wajumbe watatu wa Kamati iliyoundwa na Makatibu Wakuu wa Fedha na Uchumi, Nishati na Madini pamoja na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, naye amepelekewa barua ya kutakiwa ajieleze katika maeneo ambayo Kamati Teule ya Bunge ilibaini kuwa hakuyazingatia kwa maslahi ya Taifa. Hatua hii imechukuliwa kwa kuzingatia Sheria na Kanuni za Nidhamu katika Utumishi wa Umma na Misingi ya Kanuni Asilia ya Haki ya Kusikilizwa Kwanza (Natural Justice), kabla ya hatua nyingine kuchukuliwa.

Bwana Mwakapugi amekwishawasilisha maelezo yake kwa Katibu Mkuu Kiongozi ambaye ndiye Mamlaka yake ya Nidhamu katika muda uliotakiwa.

Baadhi ya maeneo ambayo Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini ametakiwa kujieleza ni yafuatayo:

(i) Kutozingatia maagizo ya Baraza la Mawaziri kuhusiana na suala la ununuzi wa mitambo ya umeme wa dharura.

(ii) Kutozingatia ushauri wa kitaalam uliotolewa na PPRA kuhusu kufuata Sheria ya Manunuzi ya Umma ya mwaka 2004 na Kanuni zake za mwaka 2005.

(iii) Kutoishauri Serikali ipasavyo kuhusu umuhimu wa kuifanyia uchunguzi zaidi Kampuni ya Richmond Development Company LLC ili kujiridhisha na uwezo wake kifedha, kiutendaji, kiutaalam na kiuzoefu ili kulinda maslahi ya Taifa.
Hivi sasa, Mamlaka yake ya Nidhamu ambaye ni Katibu Mkuu Kiongozi, inafanya uchambuzi wa maelezo yake aliyoyawasilisha ili hatimaye maamuzi yatolewe kwa kuzingatia Sheria, Kanuni na Taratibu za Utumishi wa Umma.

c) Kwa upande wa Kamishna wa Nishati Bw. Bashir Mrindoko ingawa hayupo kwenye Kamati zote tatu zilizotajwa awali, Kamati Teule iliona kuwa, Bw. Mrindoko kwa kuzingatia nafasi yake kama Kamishna wa Nishati, naye achukuliwe hatua za nidhamu kwa kushindwa kumshauri Katibu Mkuu wake mpya kuhusu udhaifu wa Richmond Development Company LLC. Kwa kuzingatia Azimio hili la Kamati Teule, Bw. Mrindoko amepelekewa barua ya kutakiwa ajieleze kwa kuzingatia Misingi ya Kanuni Asilia ya Haki ya Kusikilizwa Kwanza (Natural Justice) na pia kulingana na Kanuni za Nidhamu katika Utumishi wa Umma.

Miongoni mwa maeneo ambayo Kamishna wa Nishati ametakiwa kujieleza ni kushindwa kutumia utaalam na uzoefu wake kumshauri ipasavyo Katibu Mkuu wake kuhusu uwezo wa Kampuni ya Richmond Development Company LLC. Hii ni kwa kuzingatia kuwa, Kamishna huyu ndiye aliyehusika kuandika barua ya kusitisha Mkataba uliosainiwa tarehe 30 Juni 2004 baina ya Wizara na Kampuni ya Richmond Development Company LLC wa ujenzi wa bomba la mafuta la km. 1,150 kutoka Dar es Salaam kwenda Mwanza, kutokana na Kampuni hiyo kukosa uwezo wa kifedha.
Bw. Mrindoko amewasilisha maelezo ya utetezi wake kwa Mamlaka yake ya Nidhamu katika muda wa siku kumi na nne uliotakiwa. Hivi sasa, Mamlaka yake ya Nidhamu inayafanyia uchambuzi maelezo yake ili hatimaye maamuzi yatolewe kwa mujibu wa Taratibu, Kanuni na Sheria ya Utumishi wa Umma ya mwaka 2002.


AZIMIO NAMBA 15:
"Utaratibu wa kuteua Wakurugenzi na Makamishna katika Wizara kuwa Wajumbe wa Bodi za Wakurugenzi wa Mashirika yaliyo chini ya Wizara zao unazua mgongano wa kimaslahi na kudhoofisha usimamizi pamoja na uwajibikaji, hivyo Serikali iupige marufuku mara moja."

HATUA ZILIZOCHUKULIWA:
Ni kweli kuwa huenda katika baadhi ya maeneo, mfumo huu wa uteuzi wa Wakurugenzi au Makamishna kuwa Wajumbe wa Bodi za Mashirika ya Umma unaweza kuwa na matatizo. Hata hivyo, baada ya Serikali kuzingatia Azimio hili, imeona pia kwamba, zipo pia faida za baadhi ya Wakurugenzi au Makamishna kuwa Wajumbe wa Bodi hasa katika kusaidia kutoa msimamo na ufafanuzi wa Sera na Mipango mbalimbali ya Serikali. Kwa kuzingatia umuhimu huo, Serikali inaona ni vyema utaratibu huo uendelee lakini kila Bodi itaangaliwa kipekee. Pale itakapodhihirika kuwa ni kwa maslahi ya Taifa kuwateua baadhi ya Wakurugenzi au Makamishna kuwa Wajumbe katika baadhi ya Bodi, Serikali itafanya hivyo kwa maslahi ya Taifa letu.


AZIMIO NAMBA 16:
"Kwa kuzingatia umuhimu wa nafasi aliyonayo Mheshimiwa Waziri Mkuu katika uendeshaji wa shughuli za Serikali na Uongozi wa Nchi kwa ujumla, ni wajibu wake yeye mwenyewe kupima uzito wa matokeo ya uchunguzi huu na wajibu wake Kikatiba ndani na nje ya Bunge. Vilevile, ni wajibu wa Bunge ambalo linathibitisha uteuzi wake kwa mujibu wa Ibara ya 51 ya Katiba kuangalia kama matokeo ya uchunguzi huu hayataathiri hadhi na uzito wake ndani ya Bunge".

HATUA ZILIZOCHUKULIWA:
Azimio hili lilitekelezwa mwezi Februari 2008 kwa kuwa aliyekuwa Waziri Mkuu aliamua kujiuzulu kwa kuwajibika kisiasa kwa maslahi ya Taifa.


AZIMIO NAMBA 17:
"Msajili wa Makampuni (BRELA) aifute Kampuni ya Richmond Development Company (T) Ltd. mara moja kutoka kwenye orodha ya Makampuni halali Nchini."

HATUA ZILIZOCHUKULIWA:
Serikali imefanya uchunguzi juu ya Usajili wa Kampuni ya Richmond Development Company LLC pamoja na Richmond Development Company (T) Limited ili kubaini uhalali wake na kutaka kujiridhisha kama usajili wake uliofanywa na BRELA ulikuwa kinyume cha Sheria za Nchi. Uchunguzi huo umebaini yafuatayo:

(i) Kampuni ya Richmond Development Company (T) Limited ni Kampuni iliyosajiliwa na BRELA hapa Tanzania tarehe 12 Julai 2006 na kupewa Certificate of Incorporation Namba 57014 ili kuiwezesha kupatiwa leseni ya biashara ya uzalishaji wa umeme. Hata hivyo, uchunguzi wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Masoko unaonyesha kuwa Richmond Development Company LLC haikuwa imesajiliwa na BRELA.

(ii) Hakuna taarifa ndani ya BRELA zinazoonyesha kuwa, Richmond Development Company LLC iliyoshinda Zabuni husika, ilikasimu jukumu lake la kuzalisha umeme wa dharura kwa Richmond Development Company (T) Limited ambayo ndiyo ilisajiliwa Nchini kwa kusudio hilo.

(iii) Kutokana na utata huo uliojitokeza, Mwanasheria Mkuu wa Serikali ametoa ushauri juu ya Mamlaka ya BRELA ya kuifuta Kampuni ya Richmond Development Company (T) Limited kwa kuzingatia Sheria ya Makampuni (Sura ya 212). Hivyo, kwa mujibu wa kifungu cha 215 cha Sheria hiyo, BRELA imekwishatoa notisi ya siku thelathini kwa Kampuni ya Richmond Development Company (T) Limited kuwasilisha utetezi wake kabla ya hatua za kuifuta kampuni hiyo kuchukuliwa. Taarifa hiyo ya notisi iliyotolewa na BRELA haijajibiwa.


AZIMIO NAMBA 18:
"Wamiliki wa Richmond Development Company LLC na Richmond Development Company (T) Ltd wafunguliwe kesi ya jinai mara moja kwa udanganyifu na ujanja wa kuiibia Serikali"

HATUA ZILIZOCHUKULIWA:
Awali, Serikali ilimuagiza Mwanasheria Mkuu wa Serikali kupitia kwa makini Taarifa ya Kamati Teule ya Bunge; pamoja na kumbukumbu zote za Mjadala wa suala hili Bungeni, ili kubaini maeneo yenye Makosa ya Jinai ambayo yangewezesha Serikali kuwafungulia mashtaka Wamiliki wa Kampuni ya Richmond Development Company LLC na Richmond Development Company (T) Ltd na Wawakilishi wao.

Baadhi ya maeneo ambayo yaliangaliwa ni pamoja na yafuatayo:
(a) Kampuni ya Richmond Development Company LLC kuwasilisha Taarifa za udanganyifu Serikalini kwamba wana uwezo wa kifedha, kiutendaji na utaalam katika kuzalisha umeme, jambo ambalo halikuwa kweli.

(b) Kuwasilisha Hati na Vielelezo vya udanganyifu kwa Kamati ya Serikali ya Majadiliano kuwa Kampuni ya Richmond Development Company LLC ina Mkataba wa Ubia (Consortium Agreement) baina yake na Kampuni ya Pratt & Whitney ambayo inajulikana kuwa na uwezo mkubwa Kimataifa.

Baada ya zoezi hilo kufanyika, Mwanasheria Mkuu wa Serikali alishauri kuwa, pamoja na mambo mengine ipo haja kwa Serikali:

(i) Kufanya uchunguzi wa kina ili kuthibitisha kuwa Kampuni ya Richmond Development Company LLC haina uhai wa Kikampuni (Corporate Personality) na hivyo kujiridhisha kuwa, mambo yote yaliyofanywa kwa jina la Kampuni hii, yalikuwa batili. Hii ni kwa kuzingatia fungu la 320 la Sheria ya Makampuni (Sura ya 212).

(ii) Kufanya uchunguzi wa kina katika makosa yanayoonekana kuwa ya jinai kwa watu waliohusika katika uwasilishaji wa baadhi ya nyaraka na vielelezo vingine vya udanganyifu vilivyowezesha Kampuni ya RICHMOND kupata ushindi wa Zabuni hii.

(iii) Kwa kuwa Makosa ya Jinai hupelelezwa na Polisi, TAKUKURU, Mamlaka ya Mapato na Vyombo vingine ambavyo vimepewa Mamlaka hayo Kisheria, Serikali iagize Vyombo hivyo vya Dola vilivyopewa Mamlaka ya kufanya upelelezi na kukusanya ushahidi vifanye kazi hiyo. Hii ni kwa mujibu wa Sheria ya Mwenendo wa Mashtaka ya Jinai - (The Criminal Procedure Act Cap. 20 R.E. 2002);
Lengo la zoezi hili ni kujiridhisha na kupata ukweli na ushahidi wa kutosha unaoweza kupokelewa na kukubalika Mahakamani kwa kuzingatia masharti ya Sheria ya Ushahidi (The Evidence Act, Cap 6. R.E.2002).

Hivyo, hivi sasa Vyombo vya Dola ikiwemo Idara ya Polisi vimepewa kazi hiyo na vinaendelea kufanya upelelezi na uchunguzi wa kina wa nyaraka na hati mbalimbali zilizowasilishwa na Wahusika kabla ya kuchukua hatua nyingine dhidi ya Wamiliki wa Kampuni ya Richmond Development Company LLC na Richmond Development Company (T) Ltd na Wawakilishi wao kwa kuzingatia Sheria, Kanuni na Taratibu zilizopo.


AZIMIO NAMBA 19:
"Serikali ichukue hatua za kuviboresha na kuvitumia ipasavyo Vitengo vya Utabiri wa Hali ya Hewa na Kitengo cha Maji - TANESCO ili kuiepusha Nchi na Maamuzi ya zimamoto, ambayo uzoefu unaonyesha yanaiingiza Nchi kwenye hasara kubwa."

HATUA ZILIZOCHUKULIWA:
Hatua zifuatazo zinaendelea kuchukuliwa na Serikali kama mkakati wa utekelezaji wa Azimio hili:

(i) Serikali imeanza kuimarisha Wakala wa Hali ya Hewa Nchini kwa kutoa mafunzo na kuwapatia vifaa vya kisasa kama kompyuta, vifaa vya kupimia mvua na ununuzi wa mitambo ya kisasa ya mawasiliano na ya kuchambua takwimu za hali ya hewa. Mfano, hadi sasa Serikali imekwishanunua mitambo ya mawasiliano ya kisasa iitwayo Retin 4 na Snergie kwa ajili ya kuimarisha Utabiri wa Hali ya Hewa nchini.

(ii) Kuhusu ushirikiano baina ya Kitengo cha Utabiri wa Hali ya Hewa na TANESCO pamoja na Mabonde ya Maji ni mzuri, kwani kila siku TANESCO inapokea Taarifa za utabiri wa hali ya mvua na kuziingiza katika Takwimu za Msingi (data base) zinazoonyesha Mfumo wa uzalishaji umeme wa kila siku.

(iii) Vilevile, Serikali kupitia Mradi wa Maendeleo ya Sekta ya Maji (Water Sector Development Program) itaimarisha Ofisi za Mabonde ya Maji ili kuwezesha upatikanaji wa taarifa muhimu kwa Vitengo vya Maji vya TANESCO. Hii ni pamoja na kutoa mafunzo kwa Watumishi na kununua zana za kufanyia kazi kama vile magari na vifaa vya kupima kina cha maji, na wingi wa maji kwenye mito na mabwawa. Vifaa vingine ni vya kupimia mvua, maji chini ya ardhi, kupima ardhi na kuanzisha Mtandao wa Mawasiliano kwa njia ya kompyuta.


AZIMIO NAMBA 20:
"Serikali iendeshe uchunguzi maalum ili kubaini ukweli kama Taarifa rasmi ya TAKUKURU iliyotoa matokeo ya uchunguzi kuhusu mchakato wa Richmond ilikataliwa na kuharibiwa na kutolewa nyingine na kama jalada halisi linalohusu Kampuni ya Richmond lililokuwa BRELA liliharibiwa na kuwekwa lingine kwa lengo la kuficha ukweli"

HATUA ZILIZOCHUKULIWA:
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kwa kushirikiana na Vyombo vingine vya Dola wanaendelea na uchunguzi wa kina kuhusu suala hili.


AZIMIO NAMBA 21:
"Ofisi ya Bunge ianzishe Maktaba Maalum itakayohusika na utunzaji wa Mikataba yote inayoingiwa na Serikali."

HATUA ZILIZOCHUKULIWA:
Serikali inakubali utaratibu huo na itatoa ushirikiano ili kufanikisha utekelezaji wa Azimio hili kama nilivyoeleza katika Azimio Na. 13.


AZIMIO NAMBA 22:
"Miswada yote inayowasilishwa Bungeni hasa Miswada ya Umeme na Mafuta, (The Electricity Bill, 2007 na Petroleum Supply Bill, 2007) izingatie changamoto zilizoonekana wakati wa mjadala wa Taarifa ya Kamati Teule".

HATUA ZILIZOCHUKULIWA:
Miswada ya Sheria ya Umeme na ule wa Sheria ya Mafuta ilijadiliwa Bungeni mwezi Aprili 2008 na kupitishwa. Wakati wa Mjadala huo, ushauri uliopo katika Azimio hili ulizingatiwa kikamilifu.


AZIMIO NAMBA 23:
"Serikali iyafanyie kazi Mapendekezo ya Kamati Teule na kuliarifu Bunge kuhusu utekelezaji wake ndani ya miezi mitatu kuanzia tarehe 15/2/2008."

HATUA ZILIZOCHUKULIWA:
Hali halisi inaonyesha kuwa, jitihada zimefanywa na Serikali kuhakikisha Maazimio ya Bunge yanatekelezwa ndani ya miezi mitatu kuanzia tarehe 15 Februari 2008. Muda huo uliisha tarehe 14 Mei 2008. Hata hivyo, katika utekelezaji, imedhihirika kuwa, baadhi ya Maazimio yanahitaji muda mrefu kukamilisha mchakato wake wa utekelezaji hasa yale yanayohusu marekebisho ya Sheria na Mifumo mbalimbali ndani ya Serikali; na pia yale yanayohitaji kufungua mashtaka ya jinai au mashtaka ya makosa ya nidhamu.


HATUA ZA NIDHAMU KWA WATUMISHI:

7. Mheshimiwa Spika, kabla ya kumalizia naomba kutoa angalizo kwamba, katika kushughulikia suala hili, Kamati Teule ya Bunge katika baadhi ya Maazimio yake yanayohusiana na kuwachukulia hatua za kinidhamu baadhi ya Watumishi wa Umma waliohusika katika mchakato mzima wa Mkataba baina ya TANESCO na RICHMOND, imetumia maneno mbalimbali kama ifuatavyo:

Azimio Namba 5:
"………wawajibishwe na Mamlaka ya juu ya Nchi kwa kuchangia kuiingiza Nchi katika Mkataba wa aibu."

Azimio Namba 7:
"……Maofisa Waandamizi wa Serikali wawajibishwe kwa manufaa ya Umma…..".

Azimio Namba 9:
"…….wawajibishwe kwa manufaa ya Umma."

Azimio Namba 14:
"……. wachukuliwe hatua kali za kinidhamu kwa kuliingiza Taifa kwa makusudi kwenye Mkataba wa Kampuni ya Mfukoni".


8. Mheshimiwa Spika, Katika kutafsiri maana ya maelekezo haya, Serikali imeona kwamba, yanaweza kuwa na maana ya kushtakiwa Mahakamani kwa Makosa ya Jinai; ama kutumia Mamlaka ya Rais ya kuwastaafisha kwa manufaa ya Umma; ama kuchukua hatua za kinidhamu kwa mujibu wa Sheria ya Utumishi wa Umma na Kanuni zake.

Serikali baada ya kutafakari kwa kina suala hili, imeona kuwa, katika mazingira ya suala hili, ni busara kutumia utaratibu wa hatua za mashtaka ya Nidhamu chini ya Sheria ya Utumishi wa Umma. Utaratibu huu ni mwepesi na unaweza kusimamiwa kwa haraka zaidi, lakini bila ya kuathiri Misingi ya Haki Asilia (Natural Justice) ya Mtu Kupewa Haki ya Kusikilizwa Kwanza. Hii ni hatua muhimu sana kwani hata chini ya Mamlaka ya Rais ya kumstaafisha Mtumishi kwa manufaa ya Umma, taratibu zinataka Mtumishi apewe fursa ya kutoa maelezo ya kujitetea kabla ya hatua yoyote kuchukuliwa. Hii inatuondolea hatari ya Serikali kushtakiwa kwa kutofuata Sheria, Kanuni na Taratibu kama ilivyowahi kutokea huko nyuma, ambapo baadhi ya Viongozi na Watendaji walistaafishwa kwa manufaa ya Umma kimakosa, na baadaye Serikali ikalazimika kuingia gharama kubwa ya kuwalipa fidia. Vilevile, hatua hii inaipa nafasi Serikali kupitia utetezi utakaotolewa kuona ni Watumishi gani wanaoweza kustahili kushtakiwa kwa Makosa ya Jinai kwa mujibu wa Sheria za Nchi.


HITIMISHO:

9. Mheshimiwa Spika, napenda kusema kuwa, yapo mambo mengi ambayo sisi kama Taifa tumejifunza kutokana na mapungufu yaliyojitokeza katika mchakato wa Zabuni ya Mkataba baina ya TANESCO na RICHMOND, lakini pia na Mikataba mingine. Kwa kuzingatia hali hiyo, Serikali imeanza kulifanyia kazi suala la kuimarisha Mfumo na Uwezo wetu wa ndani wa Majadiliano ya Mikataba hasa ile mikubwa ya Kibiashara na Kiuchumi na ya muda mrefu yenye maslahi makubwa kwa Taifa letu kwa kuchukua hatua mbalimbali. Ofisi yangu tayari imepata maoni ya Wanasheria mbalimbali wakiwemo Mheshimiwa Andrew Chenge, Mbunge wa Bariadi Magharibi na Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mstaafu; Mheshimiwa Johnson Mwanyika - Mwanasheria Mkuu wa Serikali; na Mheshimiwa Nimrod Mkono Mbunge wa Musoma Vijijini. Maoni yao yatatusaidia sana katika kuimarisha Mfumo wetu wa Majadiliano ya Mikataba. Naomba nitumie nafasi hii kuwashukuru Waheshimiwa Wabunge hawa kwa maoni na ushauri wao mzuri sana.

Vilevile, nimepata nafasi ya kuzungumza na Mheshimiwa Dkt. Harrison Mwakyembe Mbunge wa Kyela, ambaye pia alinipa ushauri mzuri kuhusu namna mbalimbali za kuimarisha majadiliano katika Mikataba baina ya Serikali na Vyombo vingine vya Uwekezaji. Naomba kutumia fursa hii naye kumshukuru sana kwa mawazo yake.

Aidha, Ofisi yangu kwa kushirikiana na Wizara ya Sheria na Katiba kwa kushirikiana na Shirika la Mpango wa Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), tunaendelea kulifanyia kazi jambo hili. Serikali inatarajia kwamba, jitihada hizi zitatuwezesha kubaini kwa kina mapungufu yaliyopo na kushauri njia bora zaidi za kuimarisha majadiliano yanayohusu Mikataba.

10. Mheshimiwa Spika, mwisho, natoa Wito kwa Watumishi wote wa Umma kufanya kazi kwa Uadilifu, Bidii, Uzalendo na kuwa makini katika kila kazi kwa kuzingatia Sheria, Kanuni na Taratibu za Serikali. Kwa upande wake, Serikali itajitahidi kuhakikisha kuwa Viongozi na Watendaji wote katika ngazi zote za Utumishi wa Umma wanafanya kazi kwa umakini na kuwatumikia Wananchi kwa kutanguliza mbele Maslahi ya Taifa letu.


11. Mheshimiwa Spika, naomba kuwasilisha.
 
Nini itakuwa nafasi ya Hosea,Mwanyika ,Mwakapugi et all?

Pinda anaweza kuandika historia ya kudhubutu?ama atakuwa sawa na JK na hotuba yake ya masaa matatu ambayo spika aliijibu kwa dk 3 na kuwa na maana kuliko masaa 3?

Oh!! gosh,

Best naona ulikuwa umesha soma akili yake.

Hii ni nchi ya kulindana bwana! Kama hawa watendaji walimshauri Pm wa wakati ule vibaya pamoja na mawaziri kadhaa wakatema unga, how comes waandikiwe barua za uchumba kujieleza!!!!! Basi wamrudishe na ex Pm ili nae apewe barua ya kujieleza.

Mimi nashindwa kuelewa hawa viongozi wako kwa ajili ya nani??? Ni bora kukaa bila viongozi kuliko hawa ambao wanatuongoza kwa kulindana/kuogopana. Wasipoangalia kuna siku vizazi vijavyo vitaamua kuchimba makaburi yao ili wakapime akili zao kama zilikuwa ok.

Mungu Ibariki Tanzania, na laani viongozi wanafiki.
 
Hivi kuna hatua za kumchukulia EL? mbana kama sikusikia kitu kama hicho
 
Jana, waziri Mkuu aliwasilisha Bungeni taarifa ya utekelezaji wa mapendekezo 23 ya kamati teule iliyochunguza mchakato wa kuipata kampuni ya Richmond kufua umeme wa dharura.
Awali, katika kikao hikihiki, Dk. Mwakyembe aliwahi kusema Bungeni, tena kwa ukali, kuwa kuna watu wanakiuka kanuni kwa kuendelea kulizungumza suala la Richmond bungeni wakati mjadala huo ulishafungwa kwa mujibu wa kanuni za Bunge.
Baada ya Pinda kumaliza kuwasilisha, naibu Spika alieleza kuwa taarifa hiyo ya Pinda itajadiliwa katika kikao kijacho kwa sababu sasa hivi hakuna muda wa kufanya hivyo.
Je, huku si kukiuka kanuni kama alivyoonya Mwakyembe? Bunge linapata wapi tena nguvu ya kulijadili suala suala ambalo lilishajadiliwa na kuamuliwa?
naomba wajuziw a sheria, na hasa kanuni za Bunge walifafanue hili.
 
hivi hizi kamati za Rais, au serikali wakati inafanya uchunguzi mara ya pili, uliomba taarifa kwa wabunge wa tume ya mwakyembe? manake walihifadhi mambo mengi kuwastahi.
Je watatumika kama mashahidi katika kesi za hao watuhumiwa?
manake serikali yetu kama ninavyoijua vema, wanaweza kuignore kila kitu na kuanza upya, pia kufuata mkondo mwingine kabisa, japo wanajua kuna uchunguzi wa kina upo sehemu na proof na vinoti vipo tu sehemu. wanaweza wasihangaike navyo kwani havikusomwa kwenye taarifa ya kina mwakyembe
 
Ni kweli hata mimi nilikuwa nalifikiri hilo!! Mimi nilidhani baada ya pinda kumaliza ndo kwaheri, kumbe kuna moto mwingine utawashwa November?
Any way, sio mtaalam wa Sheria, hebu wajuzi tupeni...
 
Hivi kuna hatua za kumchukulia EL? mbana kama sikusikia kitu kama hicho

Kwa kosa gani alilofanya? Lowasa alipanic tu siku alipotangaza kujiuzulu. Mmasai yule hasira na mori mara moja. Angetulia kwa nusu saa asingejizulu, na angetoa majibu super. Tatizo lingeangukia kwenye mapungufu ya sheria zilizopo ambazo ndio ahadi kubwa iliyotolewa na PM ya kuzirekebisha. Majibu ya wote walioandikiwa barua za kujieleza yataelekezwa kwenye mapungufu hayo ya sheria mbalimbali.

Huo ndio uzuri wa mabadiliko ya utawala. Siku hizi kinachozungumziwa ni kumpa fursa mtumishi kujieleza kabla ya kumchukulia hatua. Nakumbuka mwaka 1996 wakati TRA inaanzishwa jinsi watumishi zaidi ya 600 walivyofukuzwa kazi kwa agizo la Raisi kwa manufaa ya umma bila kupewa fursa hiyo ya kujieleza tena bila kutuhumiwa kwa lolote.
 
Back
Top Bottom