Serikali ilitoa ruzuku ya shilingi bil. 153.7 kwa ATCL na shirika limepata hasara ya bil. 153 huku zaidi ya tril .1 ikitumika kununulia ndege

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
47,011
144,371
Taarifa hii ni kwa mujibu wa taarifa ya uchambuzi wa ACT Wazalendo wa taarifa ya CAG ya mwaka 2019/2020.

Je, hili shirika halijageuka "mchwa" kwa watanzania?

Hivi viongozi wa nchi hii wanaohusika na ufanyaji wa maamuzi wako mentalily fit na zaidi wako comfortable na hali hii?

Halafu bado katika Bajeti ya mwaka wa fedha wa 2019/2020, wakaomba Bunge liidhinishe shilingi bilion 500 kwa ajili ya kununulia ndege nyingine!!

Je, hawaoni au kuna 10% inahusika?

Wacha niishie hapa nisijeandika mengine yasiyofaa kuandikwa.

Very,very sad!
 
Kati ya maamuzi ya hovyo kabisa ni jinsi ATCL ilivyofufuliwa. Everything was done primitively. Kuanzia kununua ndege nyingi mara moja, jinsi zilivyonunuliwa (kwa cash), kununua ndege kubwa bila kujua zitakwenda wapi, na mwisho ule uamuzi wa kuwafukuza Fastjet.

Wakati wa fasjet, Dar - Mwanza return TZS 90,000. Leo TZS 400,000!
 
Wakati wa fasjet, Dar - Mwanza return TZS 90,000. Leo TZS 400,000!!
Kwani Mchungaji Msigwa alikosea kumuita marehemu shujaa wa zamani aliyeishi dunia ya sasa. RIP Kinjekitile wetu.
 
Kosa kulikuwa ni ndege ngapu zinunuliwe na zitaenda wapi lkn ninavyoifahamu biashara ya ndege si rahisi kutengeneza faida kea kipindi kifupi namna hiyo na kuna sababu nyingi za msingi ikiwepo ugonjwa wa corona ambao kea kiasi kikubwa umesambaratisha biashara ya utalii duniani pia na biashara zingine.La msingi ni tulikuwa na uhitaji na ulazima wa kuinunua madege yote hayo?
 
Taarifa hii ni kwa mujibu wa taarifa ya uchambuzi wa ACT Wazalendo wa taarifa ya CAG ya mwaka 2019/2020...
SHIRIKA NA WAKALA
Juzi nilimaikia mtaalam m'bobezi mmoja akisema kwamba ATCL haimiliki ndege bali shirika hilo linakodi ndege zinazomilikiwa na Wakala wa Ndege Tanzania. (/)

M'bobezi huyo aliendelea kusema kwamba ATCL yaani iliingia mkataba Wakala wa Ndege Tanzania kwa ajili ya kukodi ndege. Mkataba huo haukuwa na kipengele za kuilinda ATCL iwapo haitafanya Biashara, yaani ATCL ifanye au isifanye biashara lazima imlipe Wakala wa Ndege.

Mwaka jana mwanzoni akaingia mgeni CORONA na biashara nyingi ikiwemo ya ndege zikayumba. Mbali na myumbisho huo ATCL ikaendelea kumlipa Wakala.

Yaani ACTL ikaendelea kukonda wakati Wakala ananenepa.

Kwa maoni ya m'bobezi huyo, kwa vile ATCL (Shirika) na Wakala wote ni watoto wa Serikali basi hakuna hasara ambayo serikali imepata na hivyo taarifa ya harasa ya ATCL haiakisi uhalisia.

Yaani huyo m'bobezi anataka kutuaminisha kwamba pesa zitokanazo na kodi zetu zipo salama na biashara ya ndege uendelee.

Yaani, aaah we dogo kata dafu nishushie hasira. Yaani hawa timu Magu, we acha tu waendelee kukigawa chama tutafika tu, 2025 sio mbali panapo majaliwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kati ya maamuzi ya hovyo kabisa ni jinsi ATCL ilivyofufuliwa. Everything was done primitively. Kuanzia kununua ndege nyingi mara moja, jinsi zilivyonunuliwa (kwa cash), kununua ndege kubwa bila kujua zitakwenda wapi, na mwisho ule uamuzi wa kuwafukuza Fastjet.

Wakati wa fasjet, Dar - Mwanza return TZS 90,000. Leo TZS 400,000!
Fastjet Tanzania ilishaanza kujifia ila wengi tunaitolea mfano kiushabiki tu. Kaangalie mlima wa madeni uliokuwa unawamaliza.
Jiulize kwanini ndege zao wameshindwa kuziondoa kwenye ardhi ya Tanzania mpaka leo hii ninapoandika. Nadhani hujui hilo.
 
Back
Top Bottom