Serikali ilitoa maagizo ya maandishi kwa TFF maana isije kuwaruka

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
47,013
144,371
Serikali kwakuwa nyie ndio mmetajwa katika taarifa ya TFF kuwa mmeagiza mechi ya Simba na Yanga isogezwe mbele mpaka saa 1:00 usiku badala ya kuanza saa 11:00 jioni kama ilivyokuwa imepangwa awali, ni vema mkatoa maelezo kwa umma ili msije kuwaruka TFF ingawa nao hawakuwa makini kupokea maagizo hayo.

Na Raisi Samia kama agizo hili halina baraka zako, fukuza wahusika, na kama lina baraka zako, basi na wewe uombe radhi kwa niaba ya serikali yako.
 
Serikali kwakuwa nyie ndio mmetajwa katika taarifa ya TFF kuwa mmeagiza mechi ya Simba na Yanga isogezwe mbele mpaka saa 1:00 na si saa 11:00 kama ilivyokuwa imepangwa, ni bora mkaweka wazi agizo hilo
Rais akitoa maagizo kwa waziri katika vikao vyake, kazi ya waziri ni kutekeleza kwa kushusha maagizo chini, sio lazima hadi rais aonyeshe ushahidi kwamba alimwagiza waziri
 
Soka sio siasa.
Hakuna kitu kinachokwepa siasa. Hata nchi kuwa mwenyeji wa FIFA World Cup au AFCON and the like, lazima ipate baraka za kisiasa, maana kuna maandalizi makubwa lazima yafanyike. Ujenzi wa uwanja wa Mkapa ni utashi wa kisiasa, na hata ujio wa timu ya taifa ya Brazil, ni utashi wa kisiasa
 
Hakuna kitu kinachokwepa siasa. Hata nchi kuwa mwenyeji wa FIFA World Cup au AFCON and the like, lazima ipate baraka za kisiasa, maana kuna maandalizi makubwa lazima yafanyike. Ujenzi wa uwanja wa Mkapa na utashi wa kisiasa, na hata ujio wa timu ya taifa ya Brazil, ni utashi wa kisiasa
It is true politics is about everything, but everything is not politics and treating everything politically, amount to make everything a failure.
 
IMG-20210508-WA0252.jpg
 
Serikali kwakuwa nyie ndio mmetajwa katika taarifa ya TFF kuwa mmeagiza mechi ya Simba na Yanga isogezwe mbele mpaka saa 1:00 usiku badala ya kuanza saa 11:00 jioni kama ilivyokuwa imepangwa awali, ni vema mkatoa maelezo kwa umma ili msije kuwaruka TFF ingawa nao hawakuwa makini kupokea maagizo hayo.

Na Raisi Samia kama agizo hili halina baraka zako, fukuza wahusika, na kama lina baraka zao, basi na wewe uombe radhi kwa niaba ya serikali yako.
duuh Sasa Rais atakuwa ni wa kufukuza fukuza kila kitu? hata mtu akinya barabarani afukuzwe na Rais
 
Halafu mbona mechi ya Azam na Yanga ilisogezwa muda wa kuanza na Yanga mbona hamkugomea? taarifa ile nayo ilitolewa muda mchache kabla ya muda wa mechi kuanza.

TFF haina ubavu wa kuigomea Serikali. TFF haina viwanja, wenye viwanja ndio wameamua hivyo.
 
Kwan hii ni mara ya kwanza kuahirisha match? Kama sio, je why game nyingine walikubali muda kubadilishwa na hii waigomee???
 
Yanga washikilie hapohapo. Nchi haiwezi kwenda kwa huu ujinga kila mtu kutaka kukanyaga kanuni na taratibu left , right & center

Barua yenyewe ya TFF haijatoa sababu ya msingi zaidi ya kusema eti wameagizwa na Wizara. Kwanini TFF hawakuwaambia Wizara kwamba kuna kanuni zinazoendesha mpira hasa inapofika match day?

Japo Yanga wanaweza kuwa convinced kuingia uwanjani saa 1, jambo hili wasiliache lipite hivihivi ili TFF wajifunze na wasirudie tena hii michezo
 
Back
Top Bottom