Serikali hii yenyewe ndio ilijisahau kuhusu bomoa bomoa kwa sababu kama watu waliachwa wakajenga halafu serikali hii hii inapeleka umeme, maji kwenye maeneo ambayo wananchi wamejenga maeneo hayaruhusiwi. Sasa ifike wakati serikali ipime maeneo yote kuokoa hii lawama na watu kuanza kuona serikali kama inawaonea. Ni mtizamo tu na watumishi wote wafanye kazi kwa weledi zaidi ili kuwasaidia watanzania ambao wengi wao bado masikini.