Serikali ilipe fidia simu feki

kayandam

Member
Apr 20, 2013
52
18
Naiomba serikali itueleze watanzania mambo yafuatayo kuhusu uzimwajiwa simu feki.

1:Huo mtambo /teklojia ya kuzima simu feki imenunua wapi?

2:Na umenunuliwa kwa shilingi ngapi?

3:Je simu feki ziliingiaje nchini wakati TBS ipo?

4:Je mnaonaje kama serikali mkawajibika kwa kushindwa kusimamia ubora wa bidhaa zinazo ingia nchini kwa kuwalipa fidia wote waliouziwa simu feki.

5.Je zoezi la kuzima simu feki litachukua muda gani?

---Kayanda Henry---
 
Wewe utawaambia wa mlipe rayc kwasababu madawa yameingia nchini na kumuathiri wakati polis wapo. Sim zenyewe zilipitia mlango wa nyuma,au bandalini lakini zikiwa kwenye bidhaa nyingine, nakushauri ufute MAWAZO hayo
 
Sheri ya manunuzi ya bidhaa (Sale of goods act) ina clause inayosema, 'Buyer beware'... Yani mnunuzi uwe makini. Sheria haitambui fidia kwa mnunuzi ambaye hakuwa makini wakati ananunua bidhaa... Mathalani mtu anauziwa simu ya line mbili, ina androidi, ina kamera, blue tooth, watsapp na makochokocho kibao kwa sh elfu hamsini wakati mwenzako kanunua simu kama hiyo kwa laki saba nane, we hushituki kwa nini unauziwa bidhaa below the market price?
 
Hapa, serikali haina cha kujibu wala nini.
Wewe nenda Kariakoo kama upo Dar omba simu, mfanya biashara anakuambia kuna simu feki na orijino sasa wewe aliyekuambia ununue feki itakayozimwa ni nani?
Hukuziona zilizokuwa na ubora wa juu au nini kilikupelekea kununua feki?

Pia wewe huwaoni wafanya biashara wasio na utu na uzalendo walioagiza simu feki?

Pia, wakumbuka waziri wa China alivyowahi kutoa jibu hapo Dar, kuhusu bidhaa feki kutoka China? alisema, China kunabidhaa bora zinazouzwa dunia nzima ila tatizo ni wafanya biashara wenu[Watanzania] wanaoomba kutengenezewa au kuagiza bidhaa feki zilizochini ya viwango.

Dunia nzima/nchi zote pana bidhaa feki na bandia, je unafikiri kote huko hakuna serikali?

Ushauri wangu , kuwa tuwe na mamlaka binafsi za kuwashitaki wafanya biashara walagai, yaani hizi ni taasisi za kuwatetea walaji/watumiaji wa bidhaa zote.

Utakuwa umeelewa.

Asante.
 
Naiomba serikali itueleze watanzania mambo yafuatayo kuhusu uzimwajiwa simu feki.
1:Huo mtambo /teklojia ya kuzima simu feki imenunua wapi?
2:Na umenunuliwa kwa shilingi ngapi?
3:Je simu feki ziliingiaje nchini wakati TBS ipo?
4:Je mnaonaje kama serikali mkawajibika kwa kushindwa kusimamia ubora wa bidhaa zinazo ingia nchini kwa kuwalipa fidia wote waliouziwa simu feki.
5.Je zoezi la kuzima simu feki litachukua muda gani?
---Kayanda Henry---
Nenda kamfungulie case aliye kuuzia!
 
Back
Top Bottom