Serikali ilikuwa na chaguo mbadala kwa wakwepa kodi

kasinge

JF-Expert Member
May 22, 2011
1,259
319
Leo biashara nyingi zimefungwa sababu walilazimishwa kulipa kodi walizokwepa hapo nyuma. Ni sawa! Lakini Madhara yake yamekuwa makubwa kwa Raia maskini, waliokuwa wanategemea vibarua kwenye biashara hizi. Kosa lilishafanyika hapo nyuma kuwaendekeza wapiga deal (Wakwepa kodi). Tulitakiwa tutafute namna ya wao kulipa kodi bila kuathiri biashara zao. Ni biashara hizi zilizokuwa zinaipungizia serkali unemployment rate. Walipofilisiwa biashara zao, wananchi wa kawaida wamedhurika sana kuliko hawa wakwepa kodi. Siyo siri, biasharaa nyingi zimefungwa, kuna tetesi pia kwamba na hazina zetu zimeyumba.

Grace period aliyoitaja juzi Mh. Rais, ndo alitakiwa awape hawa wakwepa kodi ili walipe madeni yao kuliko kuwa-frastrate na matokeo tumeyaona. Mwalimu wangu wa uchumi alisema hivi: "Hakuna mtu duniani asiyependa kulipa kodi. Tatizo ni pale anapokuwa na wasiwasi kwamba kodi nailipa itaenda wapi". Ni dhahiri, awamu ya nne rushwa zilikithili na watu hawakuona umuhimu wa kulipa kodi. Kwa kuwa serikali hii (5th) imejitahidi kuweka pesa katika mambo yanayogusa watu wa chini na kati -Elimu bure na miundombinu, basi watu nadhani wangelikuwa kulipa kodi kwa hiari. Hatujachelewa, Private sector ndiyo mwajiri mkubwa hapa. Serikali iangalia ni jinsi gani ya kufanya kazi ni hizi sector za kati ambazo nyingi zimekufa, huku ikijaribu kutoa elimu ya kodi. Watu watalipa kodi. Do not frastrate the prive sector please. Tunaua watu wengi.
 
Hatujachelewa, Private sector ndiyo mwajiri mkubwa hapa. Serikali iangalia ni jinsi gani ya kufanya kazi ni hizi sector za kati ambazo nyingi zimekufa, huku ikijaribu kutoa elimu ya kodi. Watu watalipa kodi. Do not frastrate the prive sector please. Tunaua watu wengi.[/QUOTE]

Na bado bomoa bomoa nayo ipo kazini
 
Back
Top Bottom